CAG: Shirika la Ndege ATCL limepata hasara Tsh Bilioni 191.91. Ni ongezeko la 108% ndani ya mwaka mmoja

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Akizungumza leo CAG Charles Kichere alisema

"Mheshimiwa Rais, niongee sasa hivi kuhusu kampuni yetu ya ndege. Mheshimiwa Rais, Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imeendelea kupata hasara, ambapo kwa mwaka wa fedha 2024/2025, ilipata hasara ya shilingi bilioni 191.19, ikiwa ni ongezeko la 108%"

67132.jpg
Mbona ni kidogo sana TSH 191.91 tu?? 🤔 🤔
 
Wakuu,

Akizungumza leo CAG Charles Kichere alisema

"Mheshimiwa Rais, niongee sasa hivi kuhusu kampuni yetu ya ndege. Mheshimiwa Rais, Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imeendelea kupata hasara, ambapo kwa mwaka wa fedha 2024/2025, ilipata hasara ya shilingi bilioni 191.19, ikiwa ni ongezeko la 108%"

Samia Huwa akiagiza hiyo ndege ibebe hizo timu zake Huwa anakodi au mkubwa kasema!?
 
Hasara ya 191.91 Bilioni ni wastani wa bilioni 15.99 kila Mwaka

Ingekuwa huku uswahilini kwetu, ningekuwa nimeshafunga hiyo biashara

Nafikiri ni muda sasa wa kuajiri CEO wa ATCL kwa kuzingatia merits na kumfanyia interview kabisa

Haiwezekani upate hasara zaidi ya bilioni 16 kila mwaka wakati mtu huyo huyo hilo shirika lingekuwa ni biashara yake binafsi sidhani kama angechekelea hizo hasara
 
Traxtion njoo uone wanaondesha hilo shirika wote wana elimu za kizungu...😅😅Elimu ya kizungu ndio unafundisha wizi na survival of the fittest...Maadili ya mwafrika wizi ni mwiko na ukishika ni kipigo .

Kaangalie Mkurugenzi hapa itakuwa kasoma huko nje kwa wazungu.
 
Wakuu,

Akizungumza leo CAG Charles Kichere alisema

"Mheshimiwa Rais, niongee sasa hivi kuhusu kampuni yetu ya ndege. Mheshimiwa Rais, Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imeendelea kupata hasara, ambapo kwa mwaka wa fedha 2024/2025, ilipata hasara ya shilingi bilioni 191.19, ikiwa ni ongezeko la 108%"

Wafanya kazi ni wengi kuliko idadi ya ndege?
 
Traxtion njoo uone wanaondesha hilo shirika wote wana elimu za kizungu...😅😅Elimu ya kizungu ndio unafundisha wizi na survival of the fittest...Maadili ya mwafrika wizi ni mwiko na ukishika ni kipigo .

Kaangalie Mkurugenzi hapa itakuwa kasoma huko nje kwa wazungu.
Sasa mkuu bila elimu hata hatutafika mbali
Kumbuka hata kuzuia hizo hasara tunahitaji elimu pia
 
Serikali ilitakiwa ijenge miundombinu, halafu ivutie wawekezaji binafsi kuendesha haya mashirika ya ndege, reli, mwendokasi, barabara, nk. Yenyewe ingejikita kwenye kukusanya kodi tu na kuiboresha hiyo moumdombinu.
Hii mambo ya kutengeneza hasara kila mwaka, haina afya hata kidogo kwa Taifa.
 
Wakuu,

Akizungumza leo CAG Charles Kichere alisema

"Mheshimiwa Rais, niongee sasa hivi kuhusu kampuni yetu ya ndege. Mheshimiwa Rais, Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imeendelea kupata hasara, ambapo kwa mwaka wa fedha 2024/2025, ilipata hasara ya shilingi bilioni 191.19, ikiwa ni ongezeko la 108%"

Moderator badilisha heading
Sidhani kama Tsh 191 ni kiasi sahihi

Yani hasara ya shirika la ndege haijafika hata aftatu kweli?
 
Sasa mkuu bila elimu hata hatutafika mbali
Kumbuka hata kuzuia hizo hasara tunahitaji elimu pia
😅😅 Kujiongeza mzigo hiyo ni mifumo ya wazungu ,kwa kweli tunafanya ila haiendani na sisi tunabaki kukopa ili kununua ndege na sisi tuonekane tunaenda kwa wakati ila sio asli yetu.
 
Hasara inaweza kupungua iwapo menejimenti wakipewa sekta binafsi, watumishi wote waondolewe kisha sekta binafsi waliendeshe hilo shirika kibiashara kwa kuajiri watu watakaoleta faida.​
 
😅😅 Kujiongeza mzigo hiyo ni mifumo ya wazungu ,kwa kweli tunafanya ila haiendani na sisi tunabaki kukopa ili kununua ndege na sisi tuonekane tunaenda kwa wakati ila sio asli yetu.
Sababu sio wazungu
Wapo ambao wanajua kufikiria nje ya box lakini hawana nafasi kwenye serikali ya Tanzania
 
Hakuna huyo Tz ,hawa wapiga kelele hasa wanasiasa waogope kama UKIMWI ... Mashirika hayo ukitaka wawe successful lazima kuwe na ngozi nyeupe kwenye management ; hizo ni biashara zao..

Kubali ukweli hizo sio biashara za wabongo 😅
 
Back
Top Bottom