CAG: Shirika la Ndege ATCL limepata hasara Tsh Bilioni 191.91. Ni ongezeko la 108% ndani ya mwaka mmoja

Ila Tanganyika bana. Nakumbuka ule mradi wa Bashe sijui BBT? Nowadays hakuna anayeuzungumzia tena, ni kama vile haukuwahi kuwepo na hakuna anayewajibika.
Sio kuzungumziwa ni umeshakufa kifo cha mende. Tatizo la kukurupuka kwa viongozi wasio na utaalamu wowote…!!
 
Niliwahi kuwaza hivihivi, ATCL, TRC, MWendo kasi nk, atafutwe CEO Kwa njia ya kushindanisha kwenye public interview...na isiwe lazima awe Raia.....na awe kijana 45 or lower.
Mbona fasjet aliweza japo kwa ndege za kukodi?
 
Niliwahi kuwaza hivihivi, ATCL, TRC, MWendo kasi nk, atafutwe CEO Kwa njia ya kushindanisha kwenye public interview...na isiwe lazima awe Raia.....na awe kijana 45 or lower.
Mbona fasjet aliweza japo kwa ndege za kukodi?
 
Wanasiasa wanavuruga nchi zetu ..Wanawekana yaani chama kimoja kinaendesha watu milion zaidi ya 60 ..😅😅Wanachagua wao mpaka wakurugenzi
Sema wanachaguana mpaka wanarudiana tena! Miaka nenda ni wale wale. Full kujilimbikizia mali na madaraka.
 
Ila watanganyika sisi sijui ni wapole au ni upole ulio changanyika na ujinga🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
K
Kwani hizi ndege zilipatikana kisiasa au kibiashara tuanzie hapo kwanza.
 
Mkuu rekebisha hesabu zako, hiyo 191.. ni kwa mwaka mmoja, sawa na hizo 15.99 kila mwezi.(Sio kila mwaka), hasara 16bil Kwa mwezi sawa na 4bil Kwa week +/-
 
Wanatuona mabwege sana
 
Hakika waagaji ni walewale KILA mkoa
 
unaweza kua na biashara inayokupa hasara hata kwa miaka 10, lakini kwa kujipanga vema biashara hiyo hiyo ikakupa faida miaka 50.

hivyo ndivyo biashara ilivyo unless hujui biashara. gentleman
tatizo uwajibikaji Gentleman… pesa za walipakodi zinapitea,zitumike kuboresha huduma zinazogusa maisha ya kila siku maji, barabara, afya n.k ..
 
unaweza kua na biashara inayokupa hasara hata kwa miaka 10, lakini kwa kujipanga vema biashara hiyo hiyo ikakupa faida miaka 50.

hivyo ndivyo biashara ilivyo unless hujui biashara. gentleman
Yaani wewe unahisi kuna siku ATCL itatengeneza faida? Shirika linaloendeshwa kisiasa na CCM!! Never, unaota gentleman amka utajikojolea.

Labda watangaze faida ya uongo ili kufurahisha jamii, lakini faida ya kweli kwa ATCL katika kipindi hiki cha ushindani wa kimataifa kwa mashirika ya ndege, shirika linaloongozwa kisiasa haliwezi kutoboa, NEVER
 
Yani mimi naona solution ni kuajiri wataalam tena wazungu. Chukua watu wanne kutoka hata emirates huko walete wape shirika waweke mifumo ya operations vizuri ninaamini hasara itaanza kushuka kwa kasi...kuendelea kujaza wabongo hawawezi kubadili chochote kama wanajua wakiiba wanaishia kuzomewa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…