CAG: Stendi ya Magufuli, Kibamba itaongeza foleni ya magari

CAG: Stendi ya Magufuli, Kibamba itaongeza foleni ya magari

Sasa mmeo mbona kala hasara kwa akili zako alafu unatako gumu [emoji1].
Kwahiyo tusiiamini report ya CAG, we mama VP

hiyo ya kusema stand itasababisha foreni!!!

si afadhali hizo akili ukaweke mbolea sasa!!!
 
Mojawapo na solution ni ujenzi wa njia Mbezi shule mpaka Bunju via mabwepande ili mabus yote yaendayo kaskazini yapite hapo bila kurudi Morogoro road,

Pili njia ya Kibamba mpiji Magoe makabe njia panda ya Goba hii itakuwa Kama Mbezi bypass.

Lakini pia kutoka mloganzira kwenda kisarawe au kinyerezi hizi ziwe Kama bypass au ring road na mwisho ujunzi wa daraja mbezi
Madaraja yatakua mangapi sasa hizi hela
 
tukisema kuna harakati za chini chini kumzima mwendazake wajuha wanapiga yowe.
Sahihi Mkuu, wamekazana kumchafua mwenda zake utadhani wao walikuwa pembeni. Kimsingi wanajivua nguo wenyewe. Wangekaa kimya waendelee kupiga kazi. Penye shida wanarekebisha. Kuna lipi baya alilolifanya mwenda zake ambalo wao hawahusiki? Walikuwepo na walikuwa watekelezaji wa haya yote.
 
Madaraja yatakua mangapi sasa hizi hela
Mkuu daraja peke yake sio solution.

Mfano Sasa hivi asubuhi na jioni njia ya kinyerezi, njia ya Goba jioni hazipitiki maana magari ni mengi yaendayo na yatokayo mbezi stand.

Daraja litapunguza tu msongamano waingiao au watokao Morogoro Road lakini load ya magari bado ni kubwa.

Mabus yote yaendayo kaskazini yanaingia Goba road ambayo ni nyembamba lakini muda huo wanaoenda kazini wanaitumia njia hiyo hiyo ama warudi. Ama mabus yarudi Hadi ubungo mwenge ndio yaende huko yaendako lakini mbezi Bunju ni 21km hakuna daraja hivyo ni around TZS25b, kibamba makabe Goba road ni 14km hakuna daraja.

Point yangu ni kwamba hata daraja likiwepo bado load ni kubwa kwa njia zote za kuingia mbezi hivyo kupunguza hiyo traffic load ni hizo njia zijengwe Kisha daraja.

Ubungo zilijengwa njia nyingi Sana kupunguza load mfano, njia ya chuo kikuu, makongo, maji chumvi kupitia external, na tuliona matokeo.

Hivyo hivyo kwa mbezi
 
Kwahiyo CAG ni mkaguzi wa mipango miji? Duuh
CAG ni mkaguzi wa shughuli zote za serikali. Popote pale serikali imetumia pesa CAG lazima akague.

Na haji na vigezo vyake Bali vigezo vyenu mlivyoweka na mlivyotumia kujustify huo mradi. Maana mlipewa pesa kwa sababu mtakwenda kutatua changamoto fulani Sasa CAG akija anavichambua hivyo vigezo vyenu ili kuona value for money.
 
Mimi sio saizi yako usijilinganishe na mimi,uwe na adabu inaonekana umeanza maisha kipindi cha Magufuli ndio maana ulikuwa unamuona mungu mtu.
Usihofu ata kinamaa walioenda eji kama mm napiga tu....usione soo
 
Eng. Mfugale pamoja na timu yako tumieni utaalamu wenu kutatua changamoto hiyo iliyo ibuliwa na CAG,
tutashangaa kama mtaamua kukaa nakusubiria tatizo hilo lijitokeze.
 
Hapo ndio nilikua cag amenunuliwa na awamu ya msoga
 
CAG ni mkaguzi wa shughuli zote za serikali. Popote pale serikali imetumia pesa CAG lazima akague.

Na haji na vigezo vyake Bali vigezo vyenu mlivyoweka na mlivyotumia kujustify huo mradi. Maana mlipewa pesa kwa sababu mtakwenda kutatua changamoto fulani Sasa CAG akija anavichambua hivyo vigezo vyenu ili kuona value for money.
Niambie ni kituo kipi katika nchi hii ambapo gari zikiingia na kutoka hazisababishi foleni
 
Vita ya uchumi ni ngumu mn unapigana na usiowajua
 
CAG alibase kwenye kukagua miradi ya hayati tuuh au maana kila anachokitolea kasoro ni kile kilichoanzishwa au kilichokua kinapiganiwa na hayati...sielewi kama amepania vile kubomoa legacy ya mtu
 
Niambie ni kituo kipi katika nchi hii ambapo gari zikiingia na kutoka hazisababishi foleni
Issue sio kusababisha foleni scope ya foleni ndio Jambo la msingi.

Standa ya mbezi mabus makubwa tu yanayotoka na kuingia stand ni zaidi ya 1500 kwa siku na kila moja linaondoka na zaidi ya watu 50 sawa na watu 75,000. Shida ni kwamba wengi wao wanaondoka karibu muda unaofanana na wengi wanaingia pia karibu muda unaofanana. Sasa pressure ya watu kuingia na kutoka kwa wakati mmoja nibkubwa

Tatu muda ambao hiyo pressure inayokea ni aidha muda we watu kwenda kazini au kutoka kazini hivyo kufanya shughuli nyingi kukwama.

Huwezi lingajisha mbezi na makumbusho, tegeta nyuki, mbagala n.k scope ya foleni ya mbezi ni kubwa kuliko zote na Zina madhara kwa uchumi na ndio maana unatazamwa kwa hicho tofauti.

Upo hapo?
 
Back
Top Bottom