CAG: Stendi ya Magufuli, Kibamba itaongeza foleni ya magari

CAG: Stendi ya Magufuli, Kibamba itaongeza foleni ya magari

Wajinga watabisha,ila watu wenye maono wameshaliona mapema sana
 
sasa kama repoti ya CAG imebainisha hayo, inatakiwa sasa MAMLAKA husika kama TANROAD na TARURA kufanyia kazi changamoto hizo ili kuepusha tatizo la foleni.

Naaamini kabisa Mkurugenzi wa tanroad na wa tarura watalifanyia kazi kitaalamu na kuepusha foleni ktk eneo la mbezi, halo sasa kinachotakiwa ni utaalamu utumike.

Eng. Mfugale na timu yako shughulikieni changamoto hiyo haraka badala ya kusubiri iwe kero kubwa.
 
Hii nchi Kuna watu wanaichezea Hivi mie nilidhani office ya CAG Kuna watu wanajua hesabu tuu kumbe hata Mambo ya mipango miji aisee hii nchi hii ngumu sana
 
Mwenda zake mwanasayansi, injinia, chemist, IGP, gavana wa BOT, msanifu wa barabara na majengo, mkemia mkuu, daktari mkuu, spika wa bunge, jaji mkuu, kamanda wa polisi,sheikh na paroko in short mwenda zake alikua anamudu sekta zote, ona sasa matokeo yake
Haaahaaaahaaa[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 

CAG amesema stendi ya mabasi ya Magufuli iliyopo Kibamba manispaa ya Ubungo haikuwemo katika usanifu wa ujenzi wa barabara ya njia 8 kutoka Ubungo hadi Kibaha.

Kwa maana hiyo stendi ya Magufuli itaongeza msongamano wa magari tofauti na lengo la mradi huo wa barabara la kuondoa kabisa foleni kati ya Ubungo na Kibaha.

Ukinizingua Nitakuzingua!
huyu CAG atakuwa chadema achunguzwe hawa wametuchelewesha sana ndugu zangu
 
Mojawapo na solution ni ujenzi wa njia Mbezi shule mpaka Bunju via mabwepande ili mabus yote yaendayo kaskazini yapite hapo bila kurudi Morogoro road,

Pili njia ya Kibamba mpiji Magoe makabe njia panda ya Goba hii itakuwa Kama Mbezi bypass.

Lakini pia kutoka mloganzira kwenda kisarawe au kinyerezi hizi ziwe Kama bypass au ring road na mwisho ujunzi wa daraja mbezi
Kwahiyo CAG ni mkaguzi wa mipango miji? Duuh
 
Kwani stendi imejengwa ndani ya hifadhi ya barabara? Tunafahumu mbezi - kimara kulikuwa na bomoabomoa, sasa inakuwaje wenyewe wanajenga ndani ya hifadhi.
Stendi za daladala huwa zinakengwa nje ya hifadhi ya barabara? Hivi huwa mnapata faida gani hasa pale mnapotoa ubongo kichwani na kujaza funza?
 
Mwenda zake mwanasayansi, injinia, chemist, IGP, gavana wa BOT, msanifu wa barabara na majengo, mkemia mkuu, daktari mkuu, spika wa bunge, jaji mkuu, kamanda wa polisi,sheikh na paroko in short mwenda zake alikua anamudu sekta zote, ona sasa matokeo yake

tunasubiri mrekebishe uwanjq ndio huu sasa.
 
Duuuuuu sa itakuwaje ndugu wajumbe gharama zote zilizotumika. Itakuwa ushauri ulitolewa ukakataliwa
Hii nchi ilikuwa ikiendeshwa na mtu mmoja tu, kilichofanyika hapa ni kuwa Tamisemi, haikuwashirikisha Tanroad kwenye ujenzi huo, wakati wakijua ndio wasimamizi wa hiyo barabara inayojengwa!!
 
Hivi Kibamba kuna stendi nyingine tena? Au ni hii ya Mbezi? Au Kibamba umekusudia Jimbo la uchaguzi la Kibamba ambapo na Mbezi Luis imo ndani?
 
Hesabu pamoja na uhalali wake wa kutumika hizo fedha
Mradi wa umeme kujengwa kwa upembuzi uliofanywa miaka 50 nyuma ni bomu jingine pia.

kifupi CAG anamaanisha hakuna kilichofanywa kwa utaratibu kufuatwa.

na hapo ndipo watakapojicahanganya sasa.
maana kwa kufuata taratibu wakishindwa kufanya jambo lolote wataonekana ni wapuuzi kuliko.
 
Mimi nadhani siyo kila kitu Lazima Serikali iwe inaongea. Kama Hili halikuwa na sababu ya kulitamka, maana wanaweza kulirekebisha vizuri tu, sitaki kuamini kuwa hiki kituo no tatizo kubwa Sana kiasi hicho. Ila shida kila mtu msemaji

tukisema kuna harakati za chini chini kumzima mwendazake wajuha wanapiga yowe.
 
Back
Top Bottom