CAG: TANESCO wanadaiwa Tsh. Bilioni 238 na IPTL – Deni la Tsh. Bilioni 111, Tsh. Riba Bilioni 127

CAG: TANESCO wanadaiwa Tsh. Bilioni 238 na IPTL – Deni la Tsh. Bilioni 111, Tsh. Riba Bilioni 127

Nilidhani hayati Magu alimalizana na Kalasinga juu ya IPTL ,sasa kama wamerudishwa tena kutafuta ESCROW nyingine tunakumbuka aliyesema sio fedha za serikali na sioni wa kumkemea na kumdhibiti.
Pesa za watu hizo zinakuzwa kwa kuchelewa kulipwa ilizipigwe nyingi kama wameweka kwenye kububu vile,unafikiri kwanini singa singa aliachiwa huru baada ya kifo cha jpm,mtu wao.

Nchi ngumu sana
 
Nyuma ya singasinga wapo raia feki na waislamu wasio wazalendo ndiyo wenye hiyo miradi ...tatizo jpm akuwa real dictator hao watu bila ya kuuliwa nchi itazama ndiyo hao hao wameanzisha PPP
Wanamtumia Kafulila hii nchi ndo wanamtumia Tumbili hii nchi .R.I.P Magu
 
Ndio mara ya kwanza kusikia riba imepita deni, Mimi nashauri hawa wenye IPTL wasakwe walio sign mkataba wakamatwe wafunguliwe kesi ya uhujumu uchumi ndani bila dhamana mwisho wa siku kama wanataka yaishe wafute kila kitu ila waliohusika na huu mkataba wasiachwe.
 
Nilidhani hayati Magu alimalizana na Kalasinga juu ya IPTL ,sasa kama wamerudishwa tena kutafuta ESCROW nyingine tunakumbuka aliyesema sio fedha za serikali na sioni wa kumkemea na kumdhibiti.
Yule mkurupukaji hakulipa deni la watu na Sasa limekua mara 2
 
Ana halalisha ufisadi tu

Hayo madeni ya IPTL kayatoa wapi kama kwenye vitabu vya TANESCO hayapo?

CAG anakagua vitabu vya mashirika, sasa madeni ambayo hayapo kwenye list ya debt za shirika yeye kayatoa wapi, iwapo TANESCO wenyewe wanasema hilo swala lilishamalizwa na mahakama.

Mahakama iliyowapa ushindi PAP na Rugemalila; kwa dhamana ya kuwa akija mdeni mwingine wao ndio watakaolipa hela walizopewa Tegeta Escrow na mwaka uliofuata IPTL ikafungwa rasmi.

Leo kuna madeni gani tena.

Hawa watu hawana huruma kabisa, hao wananchi wanaowatumikia walivyo na hali ngumu sasa, wakati wenyewe wanawaza kuiba tu.
 
CCM ina mbinu nyingi, wanaweza kuchepusha hiyo riba wakaitumia kwenye kampeni
 
Eeee! Mungu , Nawashauri Viongozi wangu muwasikilize mnaodhani hawawaheshimu kuliko kuwasikiliza wanaowaheshimu ili washibe.Tusipinge kukosoana kwa kuwakosoa wanaokosoa.
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amebainisha kuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linadaiwa jumla ya shilingi bilioni 238 na kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL). Kati ya kiasi hicho, bilioni 111 ni deni la msingi, huku bilioni 127 zikiwa ni riba.

Uwasilishaji wa ripoti ya CAG > Rais Samia akipokea Ripoti ya CAG kwa Mwaka 2023/2024 Ikulu Dar, Machi 27, 2025

Ripoti ya CAG inaendelea kufichua mzigo wa madeni unaolikabili shirika hilo la umma.

Tanesco kuna madudu ya kila aina miaka yote kidogo magufuli aliweza kupambana na huu upuuzi
 
Back
Top Bottom