CAG: TSh. milioni 140 ambazo Wizara ya Maliasili na Utalii iliilipa kampuni ya Wasafi hazikuwa na Mkataba uliosainiwa

CAG: TSh. milioni 140 ambazo Wizara ya Maliasili na Utalii iliilipa kampuni ya Wasafi hazikuwa na Mkataba uliosainiwa

WAKATI WA KAMPENI JAMAA ALIGAWA BODA BODA ZENYE THAMANI YA SHS MIL 200 JIMBONI KWAKE.SO UNADHANI HIZO PESA JAMAA ALIZIPATA WAPI MZEE BABA?
Hii ni baada ya kunyimwa mkopo wa pikipiki na MO
 
Hapa Diamond ameingia katika kashfa nzito sana kama iyo,kumbe kule kujidai kwako maendeleo niliyonayo mimi na wasanii wangu ni jitihada za kujituma kumbe ni wizi mtupu,Matajiri wengi nyuma ya hela zao ni wizi tu kwa kwenda mbele
 
Hata mimi nakubaliana nawe , kwa ahadi kuwa watapewa dili lingine,katibu mkuu na waziri wote wapo na sasa katibu mkuu ni waziri na aliyekuwa waziri kawa mchunga ng'ombe,hawa wote wapo na Wasafi nao wapo ,mahakama zipo, tuanzie hapo .
Naunga mkono hoja mkuu,na kipimo changu cha kwanza kwa mh. Rais ni hatua atakazochua kwa watuhumiwa wa kwny report hii.

Asipofanya chochote hakika tumeula wa chuya big time.
 
Huyu jamaa alikuwa wpi kipindi cha marehemu JPM? Mbona anataka kutuchonganisha na mwenda zake .
Magufuli alikuwa anayajuwa yote hayo lakini alikuwa anajifanya kama hakuna kitu kwa sababu yeye mwenyewe na mpwa wake walikuwa wapigaji huon assad alipoweka wazi matumizi ya ovyo ya ndugai huko India alimfukuza kazi kinyume ya katiba.
 
wizi wa fedha za wananchi walipa kodi wanyonge sijui utakoma lini.
 
cha kushangaza hata takukuru bado wametulia mpaka walekezwe....hii nchi ikoje jamani....CAG kashasema watu wamepiga....wizara hiyooo...hivi kazi yao ni nini haswa.....????? 😡 😡
 
Waziri mwenye dhamana bila shaka alikuwa ni Hamis Kigwangala. Ni vyema akachukuliwa hatua pamoja na hao wahuni wenzake ili wazirejeshe hizo fedha za serikali.

Wakileta ujuaji, wafilisiwe tu mali zao. Muda wa kucheka na nyani umekwisha.
Mmh
 
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imeeleza kuwa Sh140 milioni ambazo Wizara ya Maliasili na Utalii iliilipa kampuni ya Wasafi hazikuwa na mkataba wowote uliosainiwa.

Wizara hiyo ililipa fedha hizo kwa ajili ya wasanii ambao wangetangaza utalii wa ndani katika mikoa sita nchini Tanzania.

Akizungumza leo Alhamisi Aprili 8, 2021 katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma CAG, Charles Kichere amesema, “Wizara ililipa Sh140 milioni kwa kampuni ya Wasafi kwaajili ya wasanii ambao wangetangaza utalii wa ndani katika mikoa sita, hata hivyo hakukuwa na mkataba wowote uliosainiwa baina ya wizara na kampuni ya Wasafi na kushindwa kuhakiki wigo na huduma iliyotolewa na kampuni ya Wasafi.”

Amesema kiasi hicho cha fedha kilicholipwa kwa Wasafi hakiendani na sheria za matumizi ya fedha za umma.

Amebainisha upungufu uliobainika katika uanzishwaji wa tamasha la Urithi haukuwa na nyaraka zilizowasilishwa kwa ajili ya ukaguzi kuhusu matumizi hayo pamoja na Sh487 milioni zilipelekwa kwenye taasisi saba na kwamba hakukuwa na nyaraka zilizowasilishwa kudhibitisha matumizi hayo.

“Matumizi ya Sh585 milioni yaliyolipwa na mhasibu wa mfuko wa tozo ya maendeleo ya utalii hayakuwa na nyaraka toshelezi na kushindwa kudhibitisha uhalali wa malipo hayo,” amesema

Chanzo: Mwananchi Online
One man army has never won a war, only in movies. A state with dumb institutions.
 
Back
Top Bottom