Mkuu nani hapendi kuishi!Ila CAG huyu huyu ingekuwa enzi za Magufuli, asingethubutu kutoa maoni kama haya. Na huu ndiyo ukweli mchungu.
JPM alikuwa fisadi sanaUwanja wa ndege chato ni uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita acheni uzushi wenu.
🤣🤣🤣🤣🤣 umenuna?Badala ya kuona jinsi gani uwanja huo utatumika kuinua utalii wa buruji na nduguze wao wamekalia kuangalia mapungufu. Kama ni kujengwa umesha jengwa hawana chakufanya ili kuzuia usijengwe.
Politics tupu. Kuna mtu ameshauri ofisi ya CAG ifungwe kuwe na kandarasi ya ukaguzi wa mahesabu ya serikali kupitia Deloitte au KPMGHivi uwanja wa ndege wa Chato unatofauti gani na Uwanja wa Ndege wa Musoma unaojengwa? Au wa Mtwara? Hizo faida anazotaka CAG ni zipi? Zionekane baada ya mda fani? Maana nina hakika ata ujenzi wa terminal 3 Mwaimu Nyerere bado hatujaanza kupata faida
Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo kashajengaWatu walimshtaki kwa Mungu tu
huo ushauri ni wa hovyo. CAG yupo kikatiba na anafanya kazi yake vizuri. Sukuma Gang mmetomaswa kidogo tu mnasisimka. Tulieni mpigwe showPolitics tupu. Kuna mtu ameshauri ofisi ya CAG ifungwe kuwe na kandarasi ya ukaguzi wa mahesabu ya serikali kupitia Deloitte au KPMG
kwa utaratibu CAG anatoa ushauri baada ya kufanya ukaguzi. Nakumbuka CAG wa sasa aliteuliwa mwezi November ama December 2019 na kwa mujibu wa taarifa, uwanja ulianza kujengwa mwaka 2016. Na kwenye ripoti yake ambayo nimeisoma anasema amekagua viwanja vya Geita, Songea, Shinyanga, JNIA, Dodoma, nk.Kipindi kile alisemaje ?
Kama kipindi kile alikaa kimya kwa kuogopa Mamlaka tunajuaje kama kipindi hiki hasemi kila anachotakiwa kusema ili mradi tu kuridhisha mamlaka ?
Hii nchi unafiki mwingi sana kwamba ingebidi aombe wananchi msamaha na ajiondoe kwenye hio kazi sababu inaonyesha ni bendera fuata upepo
CAG anawalaumu bure TAA na TANROADS kwa ujenzi wa kiwanja cha ndege CHATO.Tulisema tukaitwa wapinzani tuna wivu.
Sasa wenye mamlaka wa kusema wamesema.
--
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema gharama za ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita zilizidi bajeti iliyotengwa kwa sababu ulifanyika bila upembuzi yakinifu.
CAG alisema kutofanyika kwa upembuzi yakinifu kunaongeza hatari kwa Serikali kuwekeza katika mradi usio na tija na uwezekano wa kuwapo gharama zisizodhibitiwa na ongezeko la muda katika utekelezaji wake.
“Mpatio yangu yalibaini Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) hawakufanya upembuzi yakinifu kabla ya kuanz aujenzi,” amesema Kichere.
CAG Kichere amesema Sh3.62 bilioni za mradi huo zilitolewa kwenye miradi mingine kwa matarajio kwamba zingerejeshwa baada ya Hazina kutoa fedha zake, jambo ambalo halikutekelezwa kwa wakati hivyo kusimamisha miradi mingine iiliyopangwa.
Na kashajenga utamfanya nnNa mungu kashafanya hukumu yake
Alikuwa swahiba wa mchatoBongo unafiki umetawala sana. Kama ingekuwa ni miaka miwili nyuma, kamwe asingejaribu kutoa maoni ya aina hii.
Naona kama hufahamu vizuri haya mambo. Mimi napitia taarifa hizi mara kwa mara. Kuna taarifa humu mitandaoni kwamba uwanja huo ulianza kujengwa mwaka 2016. Huyu CAG wa sasa nadhani aliteuliwa 2019 mwishoni. Kuanzia mwaka 2015 sijaona taarifa ya CAG ya ukaguzi wa viwanja vya ndege, mwaka jana ndio kakagua. Siamini kwamba huko nyuma kuanzia Prof Assad na yeye walificha bali walikuwa hawajakagua. CAG hawezi toa maoni bila kukagua, sasa kakagua katoa maoni.Unaweza ukaleta hata Post moja humu niliyoshawahi kumsifia JPM ?
Mimi sio cheerleader kama mtu anafanya mazuri ni kazi yake ndio aliyochaguliwa kufanya kuanza kwangu kumpigia makofi kwangu naona ni kupoteza rasilimali muda..., kwa yoyote anayekosea mimi huwa nipo critical sababu ninamlipa kwa kutumia kodi yangu hence nahitaji value for my money...
Sasa huyu (siongelei Assad huyu jamaa) kama aliweza kuficha huu uchafu kipindi cha JPM ni mangapi anaficha sasa ili aje kuyaongea awamu ijayo ?
Kipindi kile rais alikuwa dikteta, nani hapendi kuishi kama kina Lissu walijaribu kusema wakapigwa kitu,kina Mbowe wakabomolewa biashara na kufilisiwa,wabunge wakanunuliwa kama bidhaa. Kama tunapigana risasi CAG yeye hapendi kuishi. Sio hapo tu Assad aliondolewa kama beki tatu. Huoni tishio hapo?Kipindi kile alisemaje ?
Kama kipindi kile alikaa kimya kwa kuogopa Mamlaka tunajuaje kama kipindi hiki hasemi kila anachotakiwa kusema ili mradi tu kuridhisha mamlaka ?
Hii nchi unafiki mwingi sana kwamba ingebidi aombe wananchi msamaha na ajiondoe kwenye hio kazi sababu inaonyesha ni bendera fuata upepo
Amina, Mwenyezi Mungu amtunze Mama SamiaMungu ni mkubwa sana
Ukweli ni kwamba huo uwanja hata ukikamilika kwa 200%, kama hauna faida za kiuchumi, ni hasara tu kwa Taifa. Utafifia mwaka baada ya mwaka kwa kukosa ndege na wasafiri, na mwisho utakufa.Mkuu uwanja uko karibu kukamilika kwa 100% ukiwa na majengo mazuri ya standard ya juu kabisa duniani. Sasa nakushauri unywe sumu ufe lasivyo utakufa na stress bure. Na sisi wanakanda ya ziwa tunautumia sana tukiwa tunaenda Chato. Kwahiyo wewe bibi kizee tuliza mshono!