CAG: Uwanja wa Ndege Chato ni mradi usio na faida

CAG: Uwanja wa Ndege Chato ni mradi usio na faida

Bora uwe na asset nyingi kuliko uwe hauna na ulivyonavyo umevifanya kama dhamana.
Mwendazake ameacha asset nyingi sana.hebu vuta picha mwaka 2005 tulikuwa na uwanja wa ben mkapa, mwaka 2022 bado hauna hata matangazo ya kidigital kama ule wa azam complex.
 
Hivi uwanja wa ndege wa Chato unatofauti gani na Uwanja wa Ndege wa Musoma unaojengwa? Au wa Mtwara? Hizo faida anazotaka CAG ni zipi? Zionekane baada ya mda fani? Maana nina hakika ata ujenzi wa terminal 3 Mwaimu Nyerere bado hatujaanza kupata faida

Sent using Jamii Forums mobile app
Politics tupu. Kuna mtu ameshauri ofisi ya CAG ifungwe kuwe na kandarasi ya ukaguzi wa mahesabu ya serikali kupitia Deloitte au KPMG
 
Politics tupu. Kuna mtu ameshauri ofisi ya CAG ifungwe kuwe na kandarasi ya ukaguzi wa mahesabu ya serikali kupitia Deloitte au KPMG
Jiwe aliifanya Tanzania kuwa mali yake
 
Politics tupu. Kuna mtu ameshauri ofisi ya CAG ifungwe kuwe na kandarasi ya ukaguzi wa mahesabu ya serikali kupitia Deloitte au KPMG
huo ushauri ni wa hovyo. CAG yupo kikatiba na anafanya kazi yake vizuri. Sukuma Gang mmetomaswa kidogo tu mnasisimka. Tulieni mpigwe show
 
Kipindi kile alisemaje ?

Kama kipindi kile alikaa kimya kwa kuogopa Mamlaka tunajuaje kama kipindi hiki hasemi kila anachotakiwa kusema ili mradi tu kuridhisha mamlaka ?

Hii nchi unafiki mwingi sana kwamba ingebidi aombe wananchi msamaha na ajiondoe kwenye hio kazi sababu inaonyesha ni bendera fuata upepo
kwa utaratibu CAG anatoa ushauri baada ya kufanya ukaguzi. Nakumbuka CAG wa sasa aliteuliwa mwezi November ama December 2019 na kwa mujibu wa taarifa, uwanja ulianza kujengwa mwaka 2016. Na kwenye ripoti yake ambayo nimeisoma anasema amekagua viwanja vya Geita, Songea, Shinyanga, JNIA, Dodoma, nk.
Kwenye ripoti hiyo kuna mambo mengi. Hata hapo kwenye Geita/Chato nimeona kuna tofauti kati ya mkataba na pesa ambayo imelipwa hadi leo. Ungesoma ripoti
 
Tulisema tukaitwa wapinzani tuna wivu.

Sasa wenye mamlaka wa kusema wamesema.

--
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema gharama za ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita zilizidi bajeti iliyotengwa kwa sababu ulifanyika bila upembuzi yakinifu.

CAG alisema kutofanyika kwa upembuzi yakinifu kunaongeza hatari kwa Serikali kuwekeza katika mradi usio na tija na uwezekano wa kuwapo gharama zisizodhibitiwa na ongezeko la muda katika utekelezaji wake.

“Mpatio yangu yalibaini Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) hawakufanya upembuzi yakinifu kabla ya kuanz aujenzi,” amesema Kichere.

CAG Kichere amesema Sh3.62 bilioni za mradi huo zilitolewa kwenye miradi mingine kwa matarajio kwamba zingerejeshwa baada ya Hazina kutoa fedha zake, jambo ambalo halikutekelezwa kwa wakati hivyo kusimamisha miradi mingine iiliyopangwa.
CAG anawalaumu bure TAA na TANROADS kwa ujenzi wa kiwanja cha ndege CHATO.
CAG awe na ujasiri wa kusema aliyetoa amri uwanja ujengwe bila matayarisho yoyote ni Rais Magufuli.
CAG dont beat around the bush.
 
Akili zingine zilikua za ajabu sana sasa kule kijijini watu waende kufuata nini?
 
Unaweza ukaleta hata Post moja humu niliyoshawahi kumsifia JPM ?

Mimi sio cheerleader kama mtu anafanya mazuri ni kazi yake ndio aliyochaguliwa kufanya kuanza kwangu kumpigia makofi kwangu naona ni kupoteza rasilimali muda..., kwa yoyote anayekosea mimi huwa nipo critical sababu ninamlipa kwa kutumia kodi yangu hence nahitaji value for my money...

Sasa huyu (siongelei Assad huyu jamaa) kama aliweza kuficha huu uchafu kipindi cha JPM ni mangapi anaficha sasa ili aje kuyaongea awamu ijayo ?
Naona kama hufahamu vizuri haya mambo. Mimi napitia taarifa hizi mara kwa mara. Kuna taarifa humu mitandaoni kwamba uwanja huo ulianza kujengwa mwaka 2016. Huyu CAG wa sasa nadhani aliteuliwa 2019 mwishoni. Kuanzia mwaka 2015 sijaona taarifa ya CAG ya ukaguzi wa viwanja vya ndege, mwaka jana ndio kakagua. Siamini kwamba huko nyuma kuanzia Prof Assad na yeye walificha bali walikuwa hawajakagua. CAG hawezi toa maoni bila kukagua, sasa kakagua katoa maoni.
 
Kipindi kile alisemaje ?

Kama kipindi kile alikaa kimya kwa kuogopa Mamlaka tunajuaje kama kipindi hiki hasemi kila anachotakiwa kusema ili mradi tu kuridhisha mamlaka ?

Hii nchi unafiki mwingi sana kwamba ingebidi aombe wananchi msamaha na ajiondoe kwenye hio kazi sababu inaonyesha ni bendera fuata upepo
Kipindi kile rais alikuwa dikteta, nani hapendi kuishi kama kina Lissu walijaribu kusema wakapigwa kitu,kina Mbowe wakabomolewa biashara na kufilisiwa,wabunge wakanunuliwa kama bidhaa. Kama tunapigana risasi CAG yeye hapendi kuishi. Sio hapo tu Assad aliondolewa kama beki tatu. Huoni tishio hapo?
Hivi hujawahi kumsikia Assad akisema alinyimwa nyaraka za ununuzi wa ndege na Jiwe?
 
Mkuu uwanja uko karibu kukamilika kwa 100% ukiwa na majengo mazuri ya standard ya juu kabisa duniani. Sasa nakushauri unywe sumu ufe lasivyo utakufa na stress bure. Na sisi wanakanda ya ziwa tunautumia sana tukiwa tunaenda Chato. Kwahiyo wewe bibi kizee tuliza mshono!
Ukweli ni kwamba huo uwanja hata ukikamilika kwa 200%, kama hauna faida za kiuchumi, ni hasara tu kwa Taifa. Utafifia mwaka baada ya mwaka kwa kukosa ndege na wasafiri, na mwisho utakufa.

Ni sawa ukajenge uwanja mzuri wa mpira wa miguu kama wa Arsenal Nyarugusu, itakiwa ni uharibifu wa pesa, uwanja hautageuka kuwa timu, mashabiki au wachezaji wa mpira. Mambo kama hayo yanafanywa na watu wajinga, watu waliokosa uelewa.

Tatizo inaonekana huelewi ni nini kinasababisha kingine. Fikiria, marehemu alilazimisha jengo kubwa zuri la CRDB bank kujengwa Chato, je, kutokana na jengo hilo, kwenye potifolio ya CRDB bank, Tawi la Chato limepanda kwa sababu ya jengo kubwa?
 
Cag aaminiki hata kidogo. Je angekuwepo Magu angesema hayo?
 
Back
Top Bottom