CAG: Uwanja wa Ndege Chato ni mradi usio na faida

CAG: Uwanja wa Ndege Chato ni mradi usio na faida

Hivi uwanja wa ndege wa Chato unatofauti gani na Uwanja wa Ndege wa Musoma unaojengwa? Au wa Mtwara? Hizo faida anazotaka CAG ni zipi? Zionekane baada ya mda fani? Maana nina hakika ata ujenzi wa terminal 3 Mwaimu Nyerere bado hatujaanza kupata faida

Sent using Jamii Forums mobile app
Uwanja wa ndege Musoma ni uwanja mdogo tu hivyo hata gharama zake za ujenzi nazo ni ndogo vilevile, uwanja wa ndege Chato ni uwanja mkubwa kwa vigezo vya viwanja vya ndege Duniani.

Hata matumizi yake yanapaswa kuwa madege makubwamakubwa ili uingize kipato jambo ambalo kiuhalisia halipo.

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
Tofauti ni kuwa viwanja vya Musoma na Mtwara vimejengwa miji mikuu ya mikoa sehemu ambazo kuna watu na biashara nyingi wakati uwanja wa Chato umejengwa kijijini kwenye watu wachache ni biashara chache!
Hujui kama chato ipo mkoa geita? Nani alikudanganya ni kijijini?

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Uelewa wako ni mdogo huwezijua kitu hapo. Endelea na comment za udaku tu!

Magufuli alijenga huo uwanja usiokuwa na faida kiuchumi wala kiulinzi. Alikuwa na "umimi kwanza" sasa nyie wajinga wake mliopewa fursa kwa ukabila na ukanda, mmebaki kutetea Utumbo.

Huo uwanja ni pipa na mfuniko na uwanja aliojenga mabutu kijijini kwao
 
Na kila mtu atalipwa kwa aliyoyatenda.Usisahau hilo. Ni Allah huyohuyo aliyemtaja vibaya Firaun mpaka kwenye vitabu vya dini ili watu wajao wajue kuwa Farao alikuwa mbaya. Na Allah kawataja vema watu wema.

So, ukiishi vibaya utataja vibaya na ukiishi na watu vizuri utataja vizuri.tujitahidi tuishi vizuri na tusiumize watu kwasababu ya vyeo vyetu,vitaondoka na sisi tutaondoka
Allah ndo nani? Mimi simwamini Allah's wako mimi namwamini Jehova! Mungu wa Isaka!
 
Magufuri akufanya maamuzi sahihi kujenga uwanja wa ndege kwenye eneo lisilo na any economic potentiality
 
Tangu wakati wa mwinyi, serikali iliacha rasmi kujihusisha na biashara, ilibinafsisha hoteli zote, ikaachana na mambo ya kuanza kupikia wateja chai, kuwafulia mashuka na kuwatandikia vitanda.

Muda huu tunapoongea, Kuna magofu ya hoteli ambayo haijaisha yenye, magofu hayo yana thamani ya bilioni 11 na hayajamalizwa kujengwa!

Ghafla, bila wananchi kuambiwa kuhusu mabadiliko ya sera, na bila uchambuzi yakinifu, serikali ya JPM ilienda katikati ya mapori yaliyokimbiwa na wanyama tangu enzi za Nyerere na kujenga hoteli ya nyota tano ikitarajia watalii wataenda kulala humo. Hoteli ninayoongelea hapa ili nitoe picha kwa msomaji, ni kama kilimanjaro hoteli

Ni wazi kwamba watalii huja kuangalia wanyama, lakini pori lile halikuwa na wanyama kabisa, na ilibidi Simba wabebwe juu juu kutoka makazi yao ya asili na kupelekwa Chato ambako haikujulikana hata wangepata wapi wanyama wa kuwinda kwa ajili ya chakula Chao. Uwezekano mkubwa itakuwa wamekufa kwa kikatili kutokana na njaa.

Kulifanyika uchambuzi gani wa kina kuona haja ya serikali kuweka mabilioni kujenga hoteli ya kitalii Chato tena ya nyota tano wakati hata mikoa inayoizunguka Chato kama Geita na Kagera hawakuona mahitaji ya hoteli ya nyota tano?

Chato na Biharamulo zimejaa vigesti vya elfu tano na elfu kumi, Je Kuna mtu aliona watalii wanajazana katika vigesti hivyo kwa kukosa makazi? Au ndege kutoka mwanza zilihangaika kupeleka watalii huko? .

Kwa kuwa majengo haya ya bilioni kumi na moja na hayajaisha, na hakuna mtalii anayetarajiwa kukanyaga huko, kwa nini serikali isikigeuze chuo Cha utalii japo mazingira yake si rafiki? Maana yakikaa hivi hivi popo na panya wataharibu majengo hayo?

Tenda ya ujenzi alipewa nani ? Mayanga ? Kampuni ya JPM?.

Je itakula TSH ngapi mpaka iishe? Bilioni 50?

Screenshot_20220417-070713.jpg
 
Back
Top Bottom