Tangu wakati wa mwinyi, serikali iliacha rasmi kujihusisha na biashara, ilibinafsisha hoteli zote, ikaachana na mambo ya kuanza kupikia wateja chai, kuwafulia mashuka na kuwatandikia vitanda.
Muda huu tunapoongea, Kuna magofu ya hoteli ambayo haijaisha yenye, magofu hayo yana thamani ya bilioni 11 na hayajamalizwa kujengwa!
Ghafla, bila wananchi kuambiwa kuhusu mabadiliko ya sera, na bila uchambuzi yakinifu, serikali ya JPM ilienda katikati ya mapori yaliyokimbiwa na wanyama tangu enzi za Nyerere na kujenga hoteli ya nyota tano ikitarajia watalii wataenda kulala humo. Hoteli ninayoongelea hapa ili nitoe picha kwa msomaji, ni kama kilimanjaro hoteli
Ni wazi kwamba watalii huja kuangalia wanyama, lakini pori lile halikuwa na wanyama kabisa, na ilibidi Simba wabebwe juu juu kutoka makazi yao ya asili na kupelekwa Chato ambako haikujulikana hata wangepata wapi wanyama wa kuwinda kwa ajili ya chakula Chao. Uwezekano mkubwa itakuwa wamekufa kwa kikatili kutokana na njaa.
Kulifanyika uchambuzi gani wa kina kuona haja ya serikali kuweka mabilioni kujenga hoteli ya kitalii Chato tena ya nyota tano wakati hata mikoa inayoizunguka Chato kama Geita na Kagera hawakuona mahitaji ya hoteli ya nyota tano?
Chato na Biharamulo zimejaa vigesti vya elfu tano na elfu kumi, Je Kuna mtu aliona watalii wanajazana katika vigesti hivyo kwa kukosa makazi? Au ndege kutoka mwanza zilihangaika kupeleka watalii huko? .
Kwa kuwa majengo haya ya bilioni kumi na moja na hayajaisha, na hakuna mtalii anayetarajiwa kukanyaga huko, kwa nini serikali isikigeuze chuo Cha utalii japo mazingira yake si rafiki? Maana yakikaa hivi hivi popo na panya wataharibu majengo hayo?
Tenda ya ujenzi alipewa nani ? Mayanga ? Kampuni ya JPM?.
Je itakula TSH ngapi mpaka iishe? Bilioni 50?