CAG wa kwanza Mtanzania kutokuongezewa mkataba baada ya miaka yake yake mitano ya kwanza kumalizika

CAG wa kwanza Mtanzania kutokuongezewa mkataba baada ya miaka yake yake mitano ya kwanza kumalizika

Miaka mitano ya mwanzo ikiisha unaweza kuongezewa tena term nyingine. Ludovick aliongezewa na Jayaya Kikwete. Sijui Assad alikosea nini hadi kaweka historia ya kuwa CAG wa kwanza mzalendo kutokuongezewa muda.
Mkuu katiba ni hio hapo wapi wamezungumzia swala la kipindi cha miaka mitano? Swala la msingi ni kufikisha miaka 60 huyu mtu ana miaka 58 inakuaje?
 
Attachments

  • Screenshot_20191103-181536_Adobe Acrobat.jpg
    Screenshot_20191103-181536_Adobe Acrobat.jpg
    254.7 KB · Views: 1
Mjomba Magu sio kila kitu anaweza.Mambo mengine yanamshinda wazee wa chama wamemkalia kooni
 
Alikuwa mtu anayeita moja ni moja, mbili ni mbili, sasa Mzee Baba jiwe anataka uwe mtu uliyeokotwa jalalani, jua uliite mvua, baridi uiite joto nk, now prof Assad was a definition of a professional kitu ambacho Mzee Baba hakubaliani nacho. Ndo mana kaamua kusigina katiba akijua Kuwa bongo sasa hivi hamna wa kumnyooshea kidole.Bunge ndo Hilo la yule mgogo na Yule dada wa kinyakyusa asiejielewa,aka wazee wa maagizo kutoka juu, mahakama ipo hoi e.g kesi za wahujumu uchumi zimeendeshwa Kwa maagizo kutoka kwenye muhimili uliojichimbia Chini zaidi kama Ile ya vyanzo vya maji.nachoweza kusema Kwanza sindano ituingie ndo kuna siku labda watz tunaweza amua fate yetu. but for now acha jiwe atambe afanye vile anaona itampendeza yy na waimba mapambio wake, period.
 
Kwa mujibu Wa katiba Assad alipaswa kustaafu 2024, baada ya hapo rais angeweza kumuongezea kama angeridhika Na utendaji wake, kumuondoa sasa rais kavunja katiba...
 
Labda aliamua kumsifu na kumtukuza Mungu mmoja tu.

Ukiwa na maadili yako katika maisha ni vigumu sana kufanya kazi na wakola!! Inanikumbusha mama mmoja alikuwa kiongozi wa mkoa wa Iringa enzi ya Mkapa; mama huyu alikuwa muadilifu sana lakini kulikuwa na Viongozi wenzie [ wabunge] ambao walikuwa wanataka kufanya ufisadi kwenye mashamba ya chai na yeye akawawekea ngumu wakashindwa kuwadhulumu wananchi!! Wale wabunge wakafanya fitina kuwa aondolewe ikabidi ahamishiwe ofisi ya Waziri mkuu hata hiivyo dhamira yao hawakufanikiwa na mpaka wengine walipoitwa mbele ya haki!! Ukiishi kwa maadili Mungu anakuepusha na balaa.
 
Haahaa tatizo rais kavunja katiba waziwazi mpaka mangumbaru wanajua
Tatizo tuna viongozi wa upinzani ambao hawajui hata kutafsiri vyema katiba, wanaishia kupotosha umma.

Huoni hiyo hatari??

Halafu , hao wasioweza kusoma Ibara moja ya Katiba na Kuielewa wanataka tuwape dhamana ya hii nchi.

Tutakuwa hatuipendi nchi hii tukiwapa dhamana ya kutuongoza watu wa aina hiyo.
 
Hao viongozi wako Wa upinzani pambana nao, umri Wa kustaafu CAG ni miaka 60, Assad ana miaka 58, rais kavunja katiba waziwazi.Assad alipaswa kustaafu 2024.Rais angeweza kuteua mwingine muda huo au kumuongezea muda usiozidi miaka mitano.
 
Karudie kusoma tena Ibara ya 144 ya katiba, labda unaweza kuja na mtazamo tofauti na huu.
 
Back
Top Bottom