Chimbuko la Neno "Allah"
Kwa ujumla: Neno "Allah" ni kifupi cha neno la kiarabu La-ilah, ambalo maana yake ni "mungu". Wakristo wa kiarabu na wapagani walitumia neno Ilah kwa maana ya Mungu. Hata Biblia za kiarabu na kiindonesia leo hii hutumia neno "Allah" kwa maaana ya Mungu. Wakati wa nyuma neno linalofanana na hilo el lilimaanisha "mungu" wa kweli au uongo katika lugha za mashariki ya kati kama kiugariki, kikaanani na kiebrania. Kabla ya Muhammad, kaaba jengo lililotunza sanamu 360 liliitwa Beit-Allah, au "Nyumba ya Allah".
Baba yake Muhammad ambaye alifariki kabla ya Muhammad kuzaliwa, aliitwa Abdullah maana yake, mtumwa wa Mungu. Pia kabila la Wayahudi liliitwa 'Abdullah bin Salam kwenye Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 59 sura ya 13 na. 362 uk.241.
Kwa udhahiri: miongoni mwa sanamu/miungu iliyoabudiwa Maka uliitwa "Allah."
Huyu alikuwa mungu maalum wa kabila la Wakureshi naye alikuwa na mabinti watatu maalum. Ukilinganisha na nguzo 4 kati ya 5 za Uislam, watu wa Maka kabla ya Muhammad walifunga kwa pamoja siku moja, walitoa sadaka kwa maskini wao, walisali wakielekeza nyuso zao Maka, na walifanya hija ('Umrah) Maka. Kulikuwa na tofauti nyingi pia, lakini inashangaza kuona muendelezo wa matendo yasiyobadilika yaliyokuwa yakifanyika kwenye ibada za kipagani za kikureshi.