SINA PESA ZA KUURUDISHA MWILI WA MWANANGU, NILIKOPA BANK MWANANGU ASOME, NILIJUA NIMEUACHA UMASIKINI.
[emoji24][emoji24] Familia ya muuguzi wa Kenya aliye aga dunia nchini Canada wakati akiogelea katika swimming pool huku akijirekodi live kwenye ukurasa wake wa Facebook, familia yake imesema imeshindwa kuurejesha mwili wa mpendwa wao kwa ajili ya hafla na mazishi.
Ikiongozwa na baba yake Jonh Nyabuto,familia ya Hellen Nyabuto maarufu kama Wendy imezungumzia kuhusu kumpoteza mtoto wao imesema kuwa bado ina ng'ang'ana kukubali kifo cha binti yao.
Kwa mujibu wa baba yake bado wanahangaika kupata pesa za kuurejesha mwili wa mpendwa wao ili aweze kupumnzishwa.
"Nimelia sana tangu nilipopata hii taarifa, rafiki zake wamekuwa wakinipigia simu na kufafanua kilichotokea, ninashindwa jinsi gani nitauleta mwili wake nchini, nimepoteza binti yangu na hakuna kitu ninachoweza kufanya sijui gharama ya kuusafirisha mwili wake kuja nchini uchungu ni mwingi, naomba msaada,
Yeye ndiyo alikuwa mwanga wangu nimemsomesha kwa shida nyingi sana" mzee Nyabuto ameliambia gazeti la the Standard .
View attachment 2331269