Hii hali kitaalam hujulikana kama serodiscordant couple, ambapo Mwenza mmoja anakua na maambukizi ya HIV lkn mwengine Hana hata kama wamekua wakifanya Ngono bila kutumia Kinga.
Nini hasa kinachotokea? Je HIV ni kitu cha kufikirika?? HAPANA..... jambo pekee hapa ni BAHATI BAHATI BAHATI yaaan uwezekano wa kupata HIV ikiwa ataendelea kufanya ngono zembe nahuyohuyo mtu kuna siku angepata maambukiz.
HIV ni kirusi kirusi kigumu kukipata , Hii inamanisha Exposure moja tu haitoshi kukupa maambukizi, lkn bado ukweli nikwamba itakuchukua mara moja tu kupata HIV.
Je Mwanaume na Mwanamke nani yupo ktk hatari zaidi ya kupata maambukizi hata mara moja tu toka siku alalae na mwathirika???? .
Jibu hapa ni Moja...MWANAMKE . Kwann?? Kwa sababu ya anatomia ya maungo ya mwanamke yanamfanya awe ktk risk kubwa sana. Kivipi?? Kuta za uke ni mucosal membrane ambayo kutoka na uundwaji wke inaruhusu HIV kupita , so mwanaume Mgonjwa anapomwagia shahawa mwanamke, uwezekano wahuyo mwanamke kukwaa ni mkubwa.. lkn pia Mwanamke mgonjwa kumpa mwanaume , kutokana na umbile la mwanaume basi nilazima MICHUBUKO iwepo kwenye uume, au itokee majimaji ya uke yamepenya kupitia mlango wa kutolea shahawa kwa mwanaume.
Sasa kwann Ndugu yako hakupata???? Ni sababu kwanza ya Bahati,, Sababu za kimaumbile, aina ya ngono alokua anafanya , lkn huwezi amini kama angendelea kumgegeda kavukavu kuna siku angeukwaa tu hamna namna.( mwanamke mgonjwa anaweza gegedana na wanaume 10 asiwape maambukizi, lkn mwanamke mzima akugegedwa na mwanaume mmoja wawili wagonjwa wakampa maambukizi)namaanisha ivi Suala la nani mwenye maambukizi kati ya anayegegeda au anayegegedwa ? Pia lazima lizingatiwe.
Kwann mtoto aliupata?? Watoto wengi wanapata maambukizi wakati wa kuzaliwa tena tena hasa kwa mama asotumia Dawa, na kwa maendeleo ya Dawa hizi zakupunguza makali, kwasasa maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto yamepungua sana kiasi kwamba kama MJAMZITO ANATUMIA DAWA vizuri ,kwa usahihi na kwa muda sahihi , Basi ni uzembe wa watoa huduma wa afya ndio utakaopelekea mtoto kupata maambukizi.
NINI FAIDA YA UTUMIAJI WA DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI YA HIV???
Mtumiaji wa Dawa hizi aliyezitumia kwa miezi zzaidi ya sita nakuendelea, kiwango cha viral load huwa kinakua undetectable , na pindi pindi kinapokua undetectable basi mtu huyu hana uwezo wakuambukiza kwa njia ya Ngono (au upo lkn kwa kiwango cha chini sanaaaaa) naivo anakua ktk nafasi yakua mwenye Afya zaidi, aliyenawiri .
Bila shaka nimejibu namengineyo.
Inakuaje ndugu yangu mke wake kafa kwa ngoma na ana mtoto wa miaka 21 naye ana ngoma,lakini baba hana?