Nijibu haya maswali kadhaa
1. Je condom inapitisha virus vya ukimwi kama watu wanavyo dai?
2.je nikimla au kula denda na mtu mwenye virusi vya ukimwi naweza kuambukizwa?
3.je ni baada ya muda gani mtu huanza kuona dalili za ugonjwa wa ukimwi?
4. Virus vya ukimwi hukaa kwenye shahawa?
5.virusi vya ukimwi hukaa kwenye mate?
6.vidonge vya kupunguza makali ya virusi vya ukimwi (ARV) humezwa kila baada ya muda gani?
7.je mtu aliye ambukizwa virusi vya ukimwi asipo tumia vidonge vya kupunguza makali ya virusi hata kwa siku moja hupata madhara gani?
8.je ikitokea mtu ametambua kuwa kwa namna moja au nyingine ameambukizwa virusi vya ukimwi muda mfupi ulio pita anatakiwa afanyaje ili kujiokoa (namaanisha uwezekano wa kujiokoa upo?)
9. Muda sahihi wa kupata majibu ya mtu kama ameambukizwa ukimwi ni baada ya siku ngapi?
10. Mtu anaye tumia ARV huweza kuishi kwa muda gani?
Nijibu hiyo top ten yangu kwanza kisha mengine nitakuuliza mdogo mdogo.
1-Kondomu haipitishi virusi, in fact utumiaji sahihi wa kondomu huzuia maambukizi kwa zaidi ya asilimia 85.
2-kama mtu huyo hana vidonda wala michubuko nawewe huna, basi busu na kunyonya mate hakuwez kukupa maambukizi..kwa ufupi lita 20 za mate ndizo zinaeza kukuweka kwa risk .
3-Dalili za maambukizi ya VVU zimegawanyika kutokana na hatua ya maambukizi na zinatofautiana mtu namtu . Ila mtu anapopata leo maambukizi , dalili za awali zinazotokana na Reaction ya mwili kupambana na kirusi huanza kuanzia wiki ya pili mpaka ya nne ,wengine huwahi hata siku ya tatu tuu... dalili hizi hudumu kwa wiki moja mpaka mbili kisha hutoweka, lkn kuvimba tezi inaweza kubakia kwa miezi hata miwili au isiwepo pia.
4-Virusi hukaa pia kwa shahawa
5-Mate yana enzymes ambazo kazi yake nikulinda kinywa naivo kufanya mazingira magumu kwa HIV , hata ivo kiwango kidogo ambacho ni negligible ndicho kinaweza patikana kiasi kwamba ni mpaka mate kuanzia lita 20 ndo unaweza kuta kiwango toshelezi cha kusababisha maambukizi.
6-Hutegemea na daraja na aina ya dawa mgonjwa, kwa mfano wapo wanaomeza kila baada ya masaa 12 asubuh jion...wapo wanaomeza kila baada ya saa 24 usiku tu.... mfano first line yasasa TLD unameza kimoja kila siku usiku.. na kwasasa mpango uliopo ni wagonjwa wote wa first line kutumia TLD.
7--madhara ya kutokumeza dawa kwa siku moja yanaweza kua madogo kiasi chakutoonekana mfano mtu kujisikia uchovu, tumbo kuuma , lkn ya kwa siku nyingi anafanya virusi vijenge usugu wa dawa naivo hazitamsaidia, hali itakayofanya vrusi kuzaliana kwa kasi na kushusha kinga ya mwili haraka.
8-uwezekano upo wakujiokoa, huku hosp wahudumu wanajichoma sindano za waathirika n.k , unachotakiwa ni kuwahi kituo cha Afya chenye huduma za CTC na kupewa PEP ndani ya masaa 72 .
Kuna Jamaangu keshajichoma.mara mbili sindano ya mwathirika namoja akiwa anamshona ,lkn mara zote alimeza PEP na yuko vzuri wakati mwingine ni Bahati ya Mungu.
9-vipimo vya HIV kwasasa tunavyotumia ni vile vinavyodetect antibodies wanaozalishwa nakinga kupambana na HIV.. sasa kuna sababu nyingi zinazopelekea antibodies kuwahi au kuchelewa kuzalishwa, namara mtu anapozalisha antibodies tu basi vipimo hivi huweza kugundua maambukizi yake.
Mfani mtu wakisukari, kansa ,atachelewa kuzalisha antibodies wakupambana na HIV sababu apo alipo tu kinga yake ipo chini... kwaiyo huyu humchukua karibu mwezi mpaka miezi mitatu ndipo atagundulika...lkn ww mzm wa afya, mwili huzalisha antibodies kuanzia wiki ya pili na kiendelea ivo ndani ya mwezi mmoja mtu atagundulika nahii pia hutegemea sensitivity na specificity ya kipimo kilichotumiwa. Kwaujumla ndani ya mwez mpaka miezi mitatu mtu husoma... kwawale ambao kinga ipo chini sababu ya maradhi yao wengine huenda hadi miezi sita ingawa ni nadra sanaaa.
10-kwa kuzingatia utumiaji mzuri wa dawa, kula lishe bora, mazoezi na maisha yasokua namsongo wa mawazo, ARVs humwongezea mtu miaka 25---35 .
Kwa bongo bongo ,msosi, kupenda ulevi, ngono, nakukaribisha maambukizi mapya, huishia kufanya miaka 20 tu.