Mkuu ngoja nikuambie kitu kimoja. Ni kweli inawezekana hawa wanaoleta hizi habari hawana uthibitisho wa moja kwa moja (mfano cheti cha daktari) kuonyesha hao wasanii wana ngwengwe.
Ila kumbuka unapokua msanii, au mtu maarufu, ni vigumu sana kuficha siri! Hii ni kwasababu mambo mengi unayoyafanya lazima kuna watu watakuona tu. Mfano ukienda hospitali, kuanzia madaktari, manesi, wahudumu kila mtu atakua interested kujua unaumwa nini? Na katika hao wote mmoja tu akishajua ni rahisi kuvujisha taarifa kwa marafiki, mke/mume, nk na hapo ndio habari kama hizi zinafika mitaani na huku JF. Au mfano unakula ARV, hata ufiche vipi lakini kumbuka lazima kuna daktari/nesi anajua, kuna mtu anaekuletea hata kama huendi kupanga foleni, so mmoja wapo anaweza kuvujisha siri.
Mfano mzuri angalia stori za wasanii waliokua wanakula unga. Nyingi zilianzia mitaani na humu JF miaka mingi sana kabla hawajaanza kuugua na kuonyesha dalili zozote. Watu wanajua vitu mkuu, japo hawana hard evidence.