Well,sikubaliani na Captain Komba kwa mwenendo wake kisiasa miaka ya hivi karibuni,lakini nakumbuka jinsi mfalme Daudi alivyoomboleza kifo cha mfalme Sauli(aliyetaka kumwua) na kumzika kwa heshima zote.Kuna somo la kimaadili natoa hapa Jf.Tulimkosoa sana Komba humu alipokuwa hai.This time hatusikii tena.Nitaufundisha mabaya moyo wangu mwenyewe iwapo nitatumia nafasi hii ya kutoa pole kwa kumtusi marehemu.Mtu akiwa hai tunaweza ku-attack personality pia,lakini akishakufa,ni vema kukosoa yale aliyoyafanya tena kwa wakati mwingine,katika mijadala mingine,sio hapa pa kutolea pole.Tuwe na uungwana wadau.JF is so big!Baada ya kusema hayo,kofia yangu nikiivua,nasema,I SALUTE YOU CAPTAIN!Thank you for your service.Goodbye.