TANZIA Captain John Komba afariki Dunia

TANZIA Captain John Komba afariki Dunia

Rip John komba sina utani kwenye kifo hap sio kwetu hatukuja na kitu na tutaondoka bila kitu nyie watoto acheni nyodo zenu za utani
 
Komba inadaiwa amefariki Baada ya kupandwa na sukari Baada ya Kifo cha Rodha George .
Huu ni msiba wa pili mkubwa kwa wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma Baada ya Jana aliyekuwa katibu wa wilaya ya Nyasa ambae inadaiwa alikuwa shabiki na msaada mkubwa kwa mbunge Kombea Rhoda George kufariki dunia katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa

Taarifa zaidi zitaendelea kujia hapa
 
Dah Maisha safari yenye mwisho wake, pumzike captain, sijui TOT itaongozwa na nani tena.

Japo ungetuambia zile nyimbo za kifo cha baba wa taifa Nyerere uliwezaje kuzitunga kwa muda mfupi vile au ulijuaje.

Msitu umekukataa Mungu amekupenda zaidi, pengine kwa kauli zako za bungeni juu ya kwenda msituni Mungu ameona yafaa mmoja afe ili wengi wapone.

Pumzika ulipojiandalia ukiwa duniani.
Mungu awape nguvu familia ya marehemu

Msalimie Baba taifa akikuuliza kama watz wanahoji kuwa uliwezaje kutunga nyimbo za kuwafariji watanzania ktk muda mfupi baada ya kufa kwake, usipepese macho mwambie baada ya ufisadi kuzidi sasa watz wanaanza kuhoji hats juu ya kifo chako.

See you one day km ninapojiandaa kwenda ndipo ulipo
 
Mkuu kweli tunatembea tukiwa wafu...!!!!

Huyu mzee juzi hapa alidai ati kama katiba mpya itatumbua uwepo wa serikali tatu "Yupo tayari kuingia msituni kupigania serikali mbili"..

Tena juzi pale Songea akawaimbia ccm wimbo wa "kuwaaga" huku Kikwete akimsifu ati haishishiwi nyimbo...!!!!! Leo ndo hivyo tena..!!!

Nadhani mstuko wa kupigwa mnada nyumba na shule alizokuwa akimiliki zimechangia mzee kuondoka mapema... Aaaaah alale anapostahili....!!!!!!!!

BACK TANGANYIKA

Hapa ndio Mafisadi wote wakumbuke kwamba Binadamu duniani tunapita,Mali zote tunaziacha hapa na hukumu inafuata.
 
Taarifa ni nitaarifa tu haijalishi munguamlaze mahalapemapeponi AMINA.
 
duh..komba ndo kafariki?...kama ni kweli...r.i.p komba
 
R.I.P Komba mbunge wetu ingawa hukututendea haki katika katiba pendekezwa.
Jimbo liko wazi sijui kampeni zinaanza lini
 
TANZIA:

Mbunge wa Mbinga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Kapteni John Damian Komba amefariki dunia ktk Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam leo saa kumi jioni.

CCM na EATV(East Africa Television) Wameandika kwenye twitter yao.
Hii kitu mbaya sana!RIP mwanaccm damudamu.Pole sana familia yote na wana mbinga.
Naona kama yale madeni ya crdb yamechangia hii kitu. Mtumeeeeee!
 
Wacha niwe mnafiki kidogo....


RIP Komba, tutakukumbuka kwa maovu uliyokwisha yafanya nchi hii....


Ulisema chadema itakufa, ukasahau Mungu hadhihakiwi



Mungi.........huyo huyo marehemu komba akadiriki kabisa kutunga nyimbo special kwa ajili ya Mwalimu Nyerere wakati hajafa ingali anajua kifo ya Mwalimu ilitengenezwa! Daaaadeki.......kufa hakuna brekiiiiii!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom