TANZIA Captain John Komba afariki Dunia

TANZIA Captain John Komba afariki Dunia

Nasikia jamaa alifikia hatua ya kutembea na masista(makasisi) wa kanisa katoliki ambao alipewa na parokia za Mbinga kama waalimu wenye weledi na taaluma ambao aliwaomba ili wafundishe kwenye shule yake ya Bakili Muluzi! Huyu Komba alijichumia laana!!
Pia kule Kimara kamjengea Lulu nyumba ambayo vijana wake wameapa kuirejesha hata ikibidi afe mtu!! Tutasikia mengi!!

Mkuu ndio maana huwa nasema unafiki hautakiwi. Nilikuwa nasubiri sana mtu aanze kusema alikuwa mtu mwema, shujaa, mpenda chama. Lakini ukweli ni kuwa jamaa was bogus as ever. Mpaka leo inaniuma sana jamaa kutumia fedha za dawa za kulevya kuiendesha TOT,...
 
Rip comrade.mshumaa umezimika wakati muhimu nani km capt komba?cc sote tumavumbi na kwake tutarejea
 
Siasa chafu msibani hzifai ndugu kwani licha ya kuwa wote twaweza kufa lakini wafiwa waweza kuwa wafuasi wa upinzani sasa au baadae kama tukiwashawishi positively kujipambanua na CCM ya mabavu na kila namna ya ubaya. Usiuige ubaya wao ukatuletea sisi wastaarabu. Ukiweza omba radhi au huwezi basi kaa kimya kwani Mungu yu kazini asikukumbuke nawe bure.

Mmmmmm uwatoe watoto wa komba Ccm?
 
Mimi sijaweka hisia wala sitawaliwi na hisia ndiyo maana nimekuwa politically neutral tangu utoto wangu, umeongelea habari za ndugu zako kama vile hawana kasoro kwamba Capt. Komba angekuwa ndugu yako hangeweza kujisahau na kujitoa ufahamu kwa kiasi kile cha kumtukana Jaji Warioba, simama na kuongelea habari zako usiongelee habari za ndugu zako maana ukweli wa ndugu zako unaujua wewe mwenyewe hapa unaongea tu kwa sababu sikufahamu(na pengine hata ID yako siyo realistic) na inawezekana ndugu zako wamejisahau sana kuliko! ila ukweli hauwezi kuusema, sijamtetea Capt. Komba kwa kauli yake dhidi ya Jaji Warioba ndiyo maana nikasema kila mtu ana mapungufu yake lakini pamoja na mapungufu yetu tusifikie mahali pakufurahia kifo cha mtu, mwenyewe unakiri kwamba kila mtu ana uhuru wa kutoa hisia zake either positively or negatively hivyo bado ukweli wa KILA MTU NA MTAZAMO WAKE UTABAKI PALEPALE! Na ulipomalizia hapo umeonyesha na kuni term mimi kama mCCM(mtazamo wako which is deadly wrong)! Mimi naongea hapa sina upande kisiasa nimezaliwa Karatu na kukulia Karatu na sasa hivi naandika hii comment nikiwa Karatu jimbo la upinzani nikikushukia nondo za ufisadi wa CHADEMA hapa Karatu kwenye Ardhi, Bodi ya maji, kiwanda cha ushirika cha maziwa nk utalia machozi, mimi sitaki kuwa mnafiki wala ku take side na kuona ufisadi wa upande ule na kufunika wa upande huu! Naongea as a politically non-aligned man mtafute mtu yeyote wa Karatu hata walioko humu kama yuko atakayepinga hayo niliyosema hapo juu, naongea facts, I'm not a politician!

Kama mtu alikuwa threat...let them dance..let them drink..let them enjoy..wamekufa wengi lakini sijawah ona hali kama hii...mungu anaonyesha mifano...jaman tufanye mema wakati tukiwa hai..huo ndo mtaj wetu tukimaliza maisha ya dunia.Matendo yako tuu ndo yatakuokoa tusifundishane unafki hapa.Komba alikuwa wakala wa wanyonyaji..mwenye ushawishi mkubwa.Hakuwahi kuimba kwa kuikosoa serikali yake hata kwenye rehasal...ametumika vya kutosha na siku zake zimeisha..nadhan huu ni mpango wa mungu juu ya maajabu ambayo anakwenda kututendea ndani ya mwaka huu(2015).MSILAZMISHE asemwe vizur.
 
hamna jipya hapa pia. kifo kwa kiumbe hai yoyote. nani kakamilika kiumbe hai hapa duniani asie kosea ? komba kama kiumbe alimkosea mh. warioba. sasa yuko.mbele ya haki. SISI TULIOHAI.MDA HUU WAJIBU TUMUACHIE MUUMBA WAKE NDIE ATAEUHUKUMU. WW.NA MM WATARAJIWA WA KUZIMU. TUNAMUELEZA NANI ? AU TUNAHADHI GANI YA KUHUKUMU KIUMBE HAI ? AU MFU ?

Mkuu hapa hatumuukumu hapa tunaombeleza..sasa kma unajua msiba wa shoga hauna matanga, jiulize msiba wa mnyonyaji unakuwaje?
 
hamna jipya hapa pia. kifo kwa kiumbe hai yoyote. nani kakamilika kiumbe hai hapa duniani asie kosea ? komba kama kiumbe alimkosea mh. warioba. sasa yuko.mbele ya haki. SISI TULIOHAI.MDA HUU WAJIBU TUMUACHIE MUUMBA WAKE NDIE ATAEUHUKUMU. WW.NA MM WATARAJIWA WA KUZIMU. TUNAMUELEZA NANI ? AU TUNAHADHI GANI YA KUHUKUMU KIUMBE HAI ? AU MFU ?

Hii habari kusema tumuachie mungu kila kitu itatucost kama alivyotutukana kama taifa ni wajibu wetu kutupa maiti yake iliwe na mamba hana hadhi ya kuzikwa he deserves hell
 
Watanzania tuache unafiki....Hivi kweli mtu kama Chenge akifa mimi nitasikitika nini?

Ni bora nifanye sherehe.
 
Jana tuliokuwa msibani tulijaa simanzi kuu baada ya mgombea urais mmoja aliyebadili hali ya msiba kilio chake kuongeza simanzi kuu.Baadaye jioni mgombea huyo aliyeapa kuingia Magogoni kwa njia yeyote alifatwa na Wandishi wa habari wakampa pole naye akwa wazi akisema amesikitika sana na msiba huu Mungu angesubiri kura za CC na NEC ziishe kwanza kwani hapo amepoteza kura yake moja ya uhakika
 
sasa mbona hakulia saaana hiyo unasema ila kaonyesha masikitiko yake tu
 
hakika ni pigo kuu kwa ccm nyimbo za huyu ndg zilikuwa zina tu inspire wengi ndg zangu / kiasi nathubutu kusema kama ktk gari basi ni propeller limekatika / tunawaomba wenye nyimbo zake wasaidie kuzi-UPLOAD HAPA
 
Jana tuliokuwa msibani tulijaa simanzi kuu baada ya mgombea urais mmoja aliyebadili hali ya msiba kilio chake kuongeza simanzi kuu.Baadaye jioni mgombea huyo aliyeapa kuingia Magogoni kwa njia yeyote alifatwa na Wandishi wa habari wakampa pole naye akwa wazi akisema amesikitika sana na msiba huu Mungu angesubiri kura za CC na NEC ziishe kwanza kwani hapo amepoteza kura yake moja ya uhakika

Seriously???!
 
​
Wakuu,

Kwa wale wanaofuatilia kwa makini vyeti vya vifo, au wameshiriki kwenye tafiti zinazohusu vifo au sababu za vifo watakuwa wamekutana na maneno haya "underlying and immediate cause of death". Kwa tafsiri isiyo rasmi ni kuwa immediate cause of death ni ile sababu ya moja kwa moja iliyopelekea kufa, wakati underlying cause of death ni zile sababu zilizopelekea ugonjwa/tatizo liliopelekea au kuchangia kifo.

Taarifa zilizonukuliwa na vyombo vya habari ni kuwa Kapt. John Komba amefariki kutokana na shinikizo la damu (i.e Immediate cause), lakini kwa wale waliofuatilia kwa makini mwenendo hadi mauti ya mwanamuziki, kipenzi cha watanzania, kada na mwanachama mwaminifu wa CCM marehemu Komba waatakubaliana nami kuwa chanzo cha hilo li presha kilikuwa ni kuzidiwa kwa madeni, madeni yaliyopelekea kupigwa mnada nyumba zake na mali zake mbali mbali.


Watu wa karibu na Marehemu komba wanakiri kuwa tokea sakata la madeni lilipoanza hali ya komba imekuwa ni yenye utata mkubwa,amekuwa akikumbwa na mshituko wa mara kwa mara, amehangaika sana hadi ofisi ya PM kuomba msaada na ama kutoka patupu au kupata msaada kiduchu, amehaha ama peke yake bila msaada wa maana…..nk ..nk.

Swali ninalojiuliza hadi sasa ni kuwa "Wako wapi Marafiki wa Lowasa" kumsaidia huyu komba hadi adhalilike kiasi kile? Kwanini afe kwa kuzidiwa na madeni wakati rafiki yake mkuu anagawa rushw kla kukicha? Kwa nini ilishindikana kumsaidia wakati tunajua fika kuwa pesa alizokopa alizipeleka kujengea shule, kununulia vitabu, kukarabati ofisi za shule? N.k

Pole sana wanafamilia, Kapt Komba amefariki katika hali ya upweke mno na kutokujaliwa.

Kama livyo ada kwa EL, na bila kuona aibu jana ameutumia msiba wa komba kujitafutia umaarufu kama tulivyoona jana, aliwaandaa waandishi eti wagombanie kumuhoji, amepigwa picha nyingi kuliko zile alizopigwa rais….nini hii?

Wapambe wa EL ni wakati wa kujipima sasa.

Nawapongeza sana Uongozi wa CCM kuendelea kumuweka kwenye "mabano EL" hasa kipindi hiki cha kujipanga na kutangaza nia.


Wenu.

Tume ya katiba,

Mwanachama mtiifu wa ADC

 
MACCM hovyo sana. chuki mmezipanda wenyewe mioyoni mwa watanzania lakni mnategemea eti wawe na upendo, utoke wapi upendo? mnaotesha mapapai halafu mnategemea kuvuna mahindi kama si ujuha ni nn hiyo sasa?!! vichwa vyeti mnavipasua kwa marungu ya mapolisi, marafiki zetu mnawapasua utombo kwa mabomu ya mapolisi, ndugu zetu albino mnawakatakata viungo, meno na kucha zetu mnaving'oa bila ganzi, mali zetu mnakwiba na kwenda kuzificha uswizi huku sisi tukiteketea kwa njaa na magonjwa yanayozuilika....i mean mnatufanyia kila aina ya dhulumati halafu cha ajabu mnategemea eti tuwe na upendo nanyi. tufanyieni dhulumati lakini jueni nanyi pia ni binadamu, hata kama itachelewa lakni kwa kuwa ninyi nanyi ni binaadamu siku yenu itafika tu one day....

chuki mlizotujaza zimejaa vifuani mwetu lakin kuna siku ya siku chuki hizo zitalipuka.


Umesema sahihi kabisa CCM wana matatizo kibao. Hoja yangu kubwa je tuna mbadala? Kwa upande wangu naona hatuna mbadala.
 
​
Wakuu,

Kwa wale wanaofuatilia kwa makini vyeti vya vifo, au wameshiriki kwenye tafiti zinazohusu vifo au sababu za vifo watakuwa wamekutana na maneno haya “underlying and immediate cause of death”.

....... lakini kwa wale waliofuatilia kwa makini mwenendo hadi mauti ya mwanamuziki, kipenzi cha watanzania, kada na mwanachama mwaminifu wa CCM marehemu Komba waatakubaliana nami kuwa chanzo cha hilo li presha kilikuwa ni kuzidiwa kwa madeni, madeni yaliyopelekea kupigwa mnada nyumba zake na mali zake mbali mbali.
Kwaiyo Postmortem report yako inasema komba kafa kwa madeni?......Hizi bangi msipende kuzivuta kavukavu wenzenu huwa wanachanganya na fegi na wanasokotea rizla ili kupunguza makali sasa wewe unavuta kavu nzima nzima lazima ikuchanganye medula oblangata
 
  • Thanks
Reactions: Bob
Back
Top Bottom