Case study Havard University: Ni kwanini kuna wasomi wachache kutoka mataifa ya kiarabu kwenye vyuo bora duniani?

Case study Havard University: Ni kwanini kuna wasomi wachache kutoka mataifa ya kiarabu kwenye vyuo bora duniani?

wanapuuza elimu ?
uwezo mdogo wa darasani ?
hawataki elimu dunia ?

Sio kwamba waarabu hawapo kabisa hivyo vyuo lakini idadi yao ni ndogo

Mfano mdogo ni idadi ya mataifa yanayoongoza kwa wahitimu kwa mwaka jana 2022/23 chuo cha Havard, hii ni kutoka moja kwa moja kwenye tovuti ya Havard

Havard Alumni

View attachment 2929507
Badala ujiulize kwani i waafrika hatumo wewe unawaza waarabu?
Yani badala usikitike tanzania haimo wewe umeenda na waarabu.
Wenzako wameanza kuamka sana na wana ela. Saudia sasa hivi wamejipanga kuwa na vyuo bora, wanachukua wakufunzi na kuwalipa mishahara minono toka duniani kote.
Sisi ndio kwanza tuko kwenye kujenga madarasa kila mwaka na kuchonga dawati.
Charity begins at home. Kabla ya kuwasema wao tujiulize kwanza sisi tuko wapi.
 
Wataiwan sio wachina ndugu yangu umeshasema wataiwan. Ukikaa na mtaiwan na mchina utajua kuna tofauti hata katika uwezo wa kufikiri.
Kwamba hapa wewe unaweza kuniambia hapa yupi ni mchina na yupi sio mchina ?
1200px-Yang_Liwei.jpg
1196d126-d852-47a9-a7b0-d10bc31d963c_efabfafa.jpg
 
Unaongelea uvumbuzi wa miaka ya zamani China hakuna uvumbuzi mpya wanafanya nakubali walivumbua gun-powder na karatasi. Mimi naongelea tafifti zinanoleta teknolojia mpya katika wakati uliopo.
Vipi 5G kuna kampuni gani ya Marekani ina 5G? Vipi china wanayo ama hawana? Unaweza ukatuekea kampuni zinazoongoza kuwa na patents nyingi za 5G?
 
Yale mafuta wanachimba makafir. Tena wanachimba huko uarabuni kwao wamahifadhi tu kwanza. Waulize wametengeneza machine ngapi sisi waarabu. Kama Gold inavyochimbwa huku na sisi weusi hatuna lolote angalau waarabu wana pata pata si haba.

Wenye akili huwa hawafanyi kazi ngumu. Bali wanawafanyisha wasomi kazi. Hata kina bakhressa wao hawafanyi kazi ngumu.

Ukiona umeajiriwa kuwafanyia watu kazi ngumu. Tambua huna akili ndio maana unafanyishwa kazi ngumu
 
Havard huingii tu kwa sababu una pesa, pia wayahudi wanahusika Sana na hicho chuo na ndio wafadhili wakuu.
Baada ya Hamas kushambulia Israel Kuna matamko yalitoka kwa wanafunzi wa.kiarabu kuunga mkono matokeo yake kampuni nyingi zinazoisaidia havard zilijisitisha ugadhili wao.
 
Kafuatilie innovations kama za electric trains,railway technology hususan Maglev railways,electric vehicles n.k n.k.
Asante sana umegusa ninapopataka treni ya kwanza ya umeme ilitengenezwa Ujerumani na majaribio yalifanyika mwaka 1979 berlin na Ernst Werner Siemens. Kwa sasa kuna technology ya hydrogen fuel cell trains inayofanywa na Daniel Ding na Xiao-Yu Wu kutoka chuo cha waterloo Canada. Hii research italeta maboresho katika treni za umeme.

Maglev trains lilikuwa tafiti(research) ya miaka 30 iliyofanywa na Injinia wa umeme Eric Roberts Laithwaite alikuwa proffesor wa chuo cha Imperial College London, Treni ya kwanza kutumia teknolojia ya Maglev ilianza kutumika mwaka 1984 Birminhgham Uingereza. Ilitumika katika kipande kifupi cha reli cha mita 600 kati ya uwanja wa ndege wa biringaham´na stesheni kuu ya reli. Nchi ambazo zinaongoza kwa tafiti kwenye teknolojia ya maglev ni 1. Japan, 2. China, 3. Marekani, 4. Korea Kusini, 5. Urusi, 6. Uswisi na 7. Ujerumani

Uvumbuzi wa Magari ya Umeme ulianza na Prof Stratingh wa chuo cha University of Groningen mwaka 1835 huko Uholanzi. Kwa sasa tafiti katika kuongeza ufanisi wa magari ya umeme zimefocus kwenye teknolojia ya betri. Tafiti iliyo juu kwa sasa ni kutoka kampuni ya saft kushirikiana na kampuni ya Total Energies iliyopo Ufaransa. Kuhusu mauzo china ndio inaunguza kwa mauzo ya magari ya umeme. Japo kuna watu wanaopinga na kudai viwanda vinazalisha magari mengi ya umeme kuliko yanayouzwa. Inayopelekea magari mengi kutekelezwa.
 
Wataiwan sio wachina ndugu yangu umeshasema wataiwan. Ukikaa na mtaiwan na mchina utajua kuna tofauti hata katika uwezo wa kufikiri.
Sasa mtanzania mwenzangu, hufahamu kuwa Taiwan nchi yao wanaiita Republic of China (ROC)? na ndivyo inavyofahamika hivyo?

Hujui hata lugha wanayozungumza ni Mandarin Chinese?

Hii iliyochini ya Xi Jinping inaitwa People's Republic of China (PRC).
 
NIkikaa nao ndani ya dakika kumi naweza kukuambia yuoi mchina, mtaiwan na mhongkong. Hawa ni watu watatu watofauti kabisa.
Nimekupa picha hapo uniambie yupi mchina na yupi sio mchina unaruka ruka.

Hivi unaelewa hata neno mchina linawagusa watu gani unapo liandika.
 
Hivyo vitu vyote navijua ndugu yangu, nimekaa na MTaiwan, Mchina na MHongkong nakuhakikishia ni watu tofauti kabisa.
 
Nimekupa picha hapo uniambie yupi mchina na yupi sio mchina unaruka ruka.

Hivi unaelewa hata neno mchina linawagusa watu gani unapo liandika.
Hauwezi kumtofautisha mtu kwa picha unakuwa limbukeni kama wazungu wa Texas ambao wanadhani watu weusi wote wanatoka katika nchi mmoja ya Afrika. Ukikaa na mtu ndio unajua anatoka nchi gani. Ninaweza kuwatofautisha kwa kuongea nao bila ya hata kuniambia wanatokea nchi gani.
 
Sasa mtanzania mwenzangu, hufahamu kuwa Taiwan nchi yao wanaiita Republic of China (ROC)? na ndivyo inavyofahamika hivyo?

Hujui hata lugha wanayozungumza ni Mandarin Chinese?

Hii iliyochini ya Xi Jinping inaitwa People's Republic of China (PRC).
Huyu ana tatizo lake kwa asilimia kubwa limeathiriwa na report za vyombo vya habari kutokana na mambo ya kisiasa yanayoihusu China na mataifa shindani ya magharibi namna wanavyo elezewa wachina wa Hongkong na Taiwan as if ni wazungu wale.

Huwezi kusema kwamba kuna mchina, mhong Kong na mtaiwan kuwa ni watu watu tofauti anacho shindwa kuelewa kuwa ni wachina wanao ishi maeneo matatu tofauti ndani ya China.
 
NIkikaa nao ndani ya dakika kumi naweza kukuambia yuoi mchina, mtaiwan na mhongkong. Hawa ni watu watatu watofauti kabisa.
Ndugu mtanzania, hujui kwamba Hong Kong ni sehemu ya nchi ya China?

Umeshawahi kusikia kitu kinachoitwa one country two systems? Kwamba Hong Kong ina sheria zake za kujitawala lakini ni sehemu ya nchi ya China? Unafahamu kwamba Hong Kong na China jeshi ni moja tu?

Au unatuigizia ndugu mtanzania?
 
Hamna cha asili au DNA mtazamo wa maisha wa MHongkong, MTaiwan na Mchina ni tofauti kabisa kama maji na mafuta.
Mtazamo katika nini ?

Nakukumbusha mfumo wa maisha wa jamii ya kichina umeathiriwa na tamaduni zao kwa asilimia kubwa pasipo kujali yupo ndani ya China au nje ya China/mataifa ya mbali
 
Hivyo vitu vyote navijua ndugu yangu, nimekaa na MTaiwan, Mchina na MHongkong nakuhakikishia ni watu tofauti kabisa.
Tofauti inaweza ikawa kwenye mtazamo, kifikra na kadhalika na hii kutokana na aina ya life style ni tofauti ambazo zimechangiwa kutokana na aina ya mfumo wa kiutawala.

Lakini hao wote ni jamii moja, ni wachina. Tamaduni yao wote ni moja.
 
Back
Top Bottom