Na mimi nililelewa kwa staili hii lakini nilipokuja kuona tunaishi tofauti na jamii nilimkaidi mzee na ndio ponea yangu, (nilishaweka uzi huu).
Ipo hivi yani, Mzee ni mtu ambae alikuwa anatulea katika mtindo ambao ulitufanya tuwaone watu nje ya familia kama vile hawahitajiki.
- Kufungiwa ndani, yani geti kali hakuna kutoka.
- Hakuna kucheza na watoto wengine hata uwanja wa karibu ama nje ya geti
- Hakuna kuingiza marafiki ndani,
- Kila mara kutuasa kwamba watu ni wabaya hawaaminiki bila kutuelimisha ni vipi tunakabiliana na huo ubaya zaidi ya kufungiwa ndani tu.
Kaka alikuwa anatii sana hizi, binafsi sikuona faida nilianza kutoka sana nje mzee akaanza kupewa taarifa mtoto wako tulimuona anacheza mpira nje, tulimkuta anacheza na wenzake nyumba flani, n.k basi nilikuwa nachapwa sana, gari iliyokuwa inatufata niliigomea maana ni watu wanne tu tulikuwa tunafatwa na magari darasa zima lenye watu 40, niliona iko poa zaidi kuongozana na wenzangu wengine wakiwa majirani, n.k.
Basi kaka yangu alikolezwa sana na hayo malezi kiukweli kawa hawa mnaowaita ma introvert, ni mtu wa kupenda sana kukaa peke yake, Nyumbani kwake hakunaga wageni kabisa labda iwe ni wale wa upande wa mke wake tu.
Ugeni katika kuishi na watu kwa kukosa mwanya huo akiwa mtoto umemfanya apitie mengi mazito, katika kujaribu hivi ukichanganya na ugeni wa urafiki kajikuta mara kadhaa akigeuzwa kuwa ngazi bila kujua anatumika tu, mbaya zaidi alipopata hata rafiki alikuwa ni kunganganizi sana hata rafiki yake wakigombana yeye anatumia nguvu sana kumbembeleza na kuomba msamaha, hii ilifanya wahuni kumtumia kirahisi
vitu vinahitaji kiasi chake, ukizidisha unaharibu,
Maisha ni kama baiskeli, unapomfundisha mtoto kuiendesha kuna muda unamshika kuna muda unamwachia kidogo, akitaka kudondoka unamshika, ivo ivo mpaka huku ukubwani tayari anajua kuendesha baiskeli bila kushikiliwa,