Team Lisu huwa hamuishiwi double standard, Yani mnapinga kila siku mgombea kupita bila kupingwa nchi yenye wananchi milioni 60, halafu anajitokeza mtu anaongea kama chiriku, mankubali bila hata kijiuliza inakuwaje Njombe nzima awe yeye tu?
Chama kama chadema huwezi kukosa mtu wa kushindana naye huo ni ubabaishaji, hata ningekuwa mimi ningekataa.
Mgombea anapotengeneza mikakati ya kupita bila kupingwa ndani ya chama lazima achunguzwe, hatuwezi kuwa na taasisi inamsikiliza mtu mmoja bila kufanya utafiti halafu inatoa maamuzi.
Chadema tunapinga swala la mgombea kupita bila kupingwa nchi hii yenye watanzania milioni 60, halafu anjitokeza mtu mmoja humo humo anatengeneza mazingira ya yeye kupita bila kupingwa akubaliwe.
Nawewe unakubali yeye ndiye mtu pekee anauwezo huko Njombe?
Wanachama wengine ni vilaza sanaaa, au hawajitambui hadi yeye pekee ndiye awe mgombea , na apigiwe kura za Ndiyo au Hapana?
Muache double standard, au la, CCM inapofanya michezo michafu ya kutengeneza mgombea kupita bila kupingwa muwe mnakaa kimya.