Catherine Ruge ameuita mfumo mpya wa uongozi wa CHADEMA kuwa ni mfumo dume "patriarchy"

Catherine Ruge ameuita mfumo mpya wa uongozi wa CHADEMA kuwa ni mfumo dume "patriarchy"

Catherine Ruge ameuita mfumo mpya wa uongozi wa CHADEMA kuwa ni mfumo dume baada ya picha iliyoonyesha wanaume tu wakiwa wamesimama kwenye jukwaa kuu katika mkutano uliomalizika jana Mlimani city. Picha hiyo iliwekwa na Janeth Rithe ambaye ni mwenyekiti wa ngome ya wanawake wa chama cha ACT Wazalendo ambapo Catherine alisema huo ni mfumo dume.

Kauli hiyo imepokelewa vibaya na wananchi mbali mbali waliomkumbusha kuwa yeye aliwaongoza BAWACHA kwenda kumchukulia fomu ya kugombea uenyekiti Freeman Mbowe baadala ya kuhakikisha kuna mwanamke kutoka BAWACHA anayeweza kugombea nafasi hiyo ya juu.

View attachment 3211395
Hao wanawake waligombea? Sikuwaona
 
Patriarchal - sio mfumo dume Ila ni ile hali mwanaume anakuwa decision maker mfanya maamuzi.

Ukileta maswala ya gender balance utazalisha jamii ya watu wajinga na wapiga majungu .

Wao wakomae na UWT , BAWACHA n.k

Unafikiri ni mwanamke gani angeweza kumuondoa Mbowe hapo Chadema?

Mnadai kitu ambacho hata mkipewa hamuwezi kukifanyia Kazi
Umenena ukweli kabisa mzee.
 
Nina uhakika hujamsikiliza au hata kufuatlia story yake, uchaguzi wa Njombe, Kanda ya Nyasa.

Hana mpinzani Njombe, lakini hata kura ya kupigiwa yeye kama mgombea pekee ndio au hapana ulivurugwa na watu walioletwa kufanya fujo.
Team Lisu huwa hamuishiwi double standard, Yani mnapinga kila siku mgombea kupita bila kupingwa nchi yenye wananchi milioni 60, halafu anajitokeza mtu anaongea kama chiriku, mankubali bila hata kijiuliza inakuwaje Njombe nzima awe yeye tu?

Chama kama chadema huwezi kukosa mtu wa kushindana naye huo ni ubabaishaji, hata ningekuwa mimi ningekataa.

Mgombea anapotengeneza mikakati ya kupita bila kupingwa ndani ya chama lazima achunguzwe, hatuwezi kuwa na taasisi inamsikiliza mtu mmoja bila kufanya utafiti halafu inatoa maamuzi.

Chadema tunapinga swala la mgombea kupita bila kupingwa nchi hii yenye watanzania milioni 60, halafu anjitokeza mtu mmoja humo humo anatengeneza mazingira ya yeye kupita bila kupingwa akubaliwe.

Nawewe unakubali yeye ndiye mtu pekee anauwezo huko Njombe?

Wanachama wengine ni vilaza sanaaa, au hawajitambui hadi yeye pekee ndiye awe mgombea , na apigiwe kura za Ndiyo au Hapana?

Muache double standard, au la, CCM inapofanya michezo michafu ya kutengeneza mgombea kupita bila kupingwa muwe mnakaa kimya.
 
Mimi sina Chama, Mimi ni chama changu ni Tanzania.

Uwe unafuatilia vitu kwa kina kabla ya kuungia kwenye mijadala.. Ameshinda mara ya kwanza kwa mujibu wa sheria pamoja na figisu nyingi, uchaguzi ukafutwa. Uchaguzi wa pili rushwa ikatembea sana, warecord na kupeleka evidence kwa wahusika, mgombea mtoa rushwa akapatwa na hatia. Ndio ukaja uchaguzi wa tatu, nao watu wakaja kufanya fujo. Ni uchaguzi pekee nchi nzima ambao haujakamilika.

Wataenda kufanya uchaguzi wa nne. Huu uchaguzi wa Mwenyekiti Chadema Taifa, ungekuwa na hizi figisu kila mtu angeona sio sawa. Kwanini unabisha na unapata shida kuona kitu kilicho wazi kabisa bila hata kufuatilia mchakato ulivyofanyika.
 
Back
Top Bottom