Naamini hii issue imesukumwa na kina Mdee, Bulaya na Matiko, kama palikuwa na resistance yoyote ndani ya vikao vya chama naamini hao watatu ndio walikuwa vinara wa kutaka waende bungeni.
Tatizo linalokuja hapa kwanini kuwe na kauli za kuchanganya, huku Mdee aseme bungeni anamshukuru Mbowe kuwaruhusu waende, na upande mwingine Mnyika aseme hawajapeleka majina?
Jibu la hayo maswali nalipata pale naposkia hao kina Bulaya, Mdee, na wenzao wamepewa ulinzi na TISS, na zaidi wanafikiriwa wapewe nafasi nyingine serikalini kama uwaziri au unaibu.
Hili linathibitisha bila shaka kwamba wamenunuliwa na CCM, kama ilivyokuwa kwa Dr. Slaa, wale wanawake narudia kusema tena ni WASALITI.
Anyway, kama ni ya kweli hiyo tweet, hongera kwa Catherine kwa kukataa kwake kuwa sehemu ya hiyo laana waliyojitafutia hao wenzake.