21 November 2024
Mbozi, Tanzania
CHADEMA YAZINDUA KAMPENI ZA TAMISEMI 2024 KWA KUSHINDO
View: https://m.youtube.com/watch?v=lfl269gZ4X8
Mji mdogo wa Mlowo jimbo la Mbozi Tanzania mambo yalikuwa moto
Mbunge wa mioyoni Paschal Haonga na viongozi wa CHADEMA wakiwa Mlowo Songwe waongea na wanachama, wapenzi na wananchi kuelekea uchaguzi wa tarehe 27 November 2024
Mbozi kwa mujibu wa
takwimu za
sensa ya watu na makazi ya 2022 ina jumla ya watu 510,599, hii ikiwa sawa na
asilimia 40 ya wakazi wote wa mkoa wa Songwe ambao kwa takwimu hizo ni 1,344,687
[1]
Miji wilayani ni
Mlowo, penye
viwanda vya kahawa vitatu vya GDM, Mbozi MCCO na LIMA (watu 37,000-50,000). Aidha
Vwawa ndiko
makao makuu ya wilaya ambapo idadi ya wakazi wake ni zaidi ya 60,000. Miji mingine miwili iko kando ya
barabara kuu ya
TANZAM kutoka
Dar es Salaam kupitia
Mbeya kwenda Zambia.
Reli ya
TAZARA inapita vilevile wilayani na kuna vituo huko Vwawa na Tunduma.
Katika wilaya hii kuna kata 29 za Vwawa, Mlowo, Ihanda, Ukwile, Ipunga, Kilimampimbi, Isalalo, Msia, Ruanda, Mahenje, Nanyala, Iyula, Hezya na Nyimbili. Nyingine ni Ichenjezya, Ilolo, Hasanga, Igamba, Nambinzo, Itaka Halungu, Isansa, Itumpi, Shiwinga, Mlowo, Magamba, Mlangali na Bara.
Ramani: Mahali pa Mbozi (kijani cheusi) katika
mkoa wa Mbeya kabla haujamegwa