Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Hoja ya awali ~ Matokeo ya CBE Dodoma Mwaka 2018/19 na 2019/20 hayajawekwa katika Mfumo wa NACTVET
YAH: UFAFANUZI KUHUSU MATOKEO YA WANAFUNZI KUTOPANDISHWA KWENYE MFUMO WA NACTVET
TAREHE: 20/10/2026
Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Kampasi ya Dodoma, kimeona taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii tarehe 20 Oktoba 2026. Taarifa hiyo inaeleza kuwa matokeo ya baadhi ya wanafunzi wa miaka ya masomo 2018/19 na 2019/20 hayajawekwa kwenye mfumo wa NACTVET. Chuo kinapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:
1. Chuo kilibaini kuwepo kwa jumla ya wanafunzi 452 waliokuwa na changamoto ya matokeo yao kutopandishwa kwenye mfumo wa NACTVET.
2. Ili kutatua changamoto hii, Chuo kilishirikiana na Maafisa kutoka NACTVET kuanzisha kituo cha huduma kwa pamoja kwa siku tano, kuanzia tarehe 05 hadi 09 Oktoba 2026, ili kushughulikia changamoto za wanafunzi husika.
3. Kupitia kituo hicho:
Changamoto za wanafunzi 429 zimeshughulikiwa kikamilifu na Chuo.
Kati ya hao, wanafunzi 100 wanasubiri hatua ya mwisho ya uhakiki (verification) kutoka NACTVET Chuo kinashirikiana na NACTVET kuhakikisha changamoto hii inaisha.
Wanafunzi 21 imebainika kuwa walikuwa na usajili wa NACTVET kupitia taasisi nyingine za elimu ya juu hata hivyo Chuo kinafanya mawasiliano baina ya wanafunzi na taasisi husika ili kutataua changamoto hiyo.
Wanafunzi 2 waliobaki walikuwa na changamoto ya kubadirishiwa programu za masomo ambapo Chuo kinashirikiana na NACTVET kutatua changamoto hiyo kwa wakati.
4. Aidha, Chuo kinatoa rai kwa mwanafunzi yeyote ambaye bado ana changamoto inayohusu matokeo yake kuwasiliana na Chuo kupitia:
Ofisi ya Udahili na Mitihani au Mkuu wa Idara husika, CBE Kampasi ya Dodoma
5. Chuo kimeimarisha utaratibu wake wa ndani ili kuhakikisha matokeo yote yanapandishwa na kuthibitishwa kwenye mfumo wa NACTVET kwa wakati, ili changamoto kama hii isijirudie.
Georgina Addo Misama
Kaimu Mkuu wa Kitengo Mawasiliano na Masoko
Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)
Kaimu Mkuu wa Kitengo Mawasiliano na Masoko
Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)