CC YA CCM: Hata kama tozo zimejenga vituo vya afya 234 na shule za Sekondari 214 bado wananchi wana hoja, zitazamwe upya

Natamani nione hii orodha ya hivi vituo vipya vya afya na hizo sekondari mpya zilizojengwa na tozo mwenye kujua aorodheshe hapa
Kuna uzi upo humu ,wameweka list..
 
Nilidhani angesema "tozo inatuumiza"...kusema "Wananchi wana hoja", ni kama vile wanaongelewa Watu wa ng'ambo ya pili.

Nchi hii Viongozi na Matajiri ni meli moja alafu kuna Wananchi, hivyo Viongozi huweza kuamua kuwasemea au kukaa kimya akiendelea kufaidi asali.
 
Hongera sana chama kubwa
Tunasema kaz iendelee.usikivu huu ni wa kiwango cha hali ya juu sana
Hata vijana wa ufipa nipo nao wanasema kazi iendelee
 
Ft hbd xx v b mnatengeneza tatizo halafu mnajifanya kulitatua gdjdjdhu hi okdhsuxxxxx
 

Chama cha majizi ya kura kazi mnayo. Mnaweka idadi ya vituo 234 kuwa ni matokeo ya tozo, wakati hivyo vituo vilikuwepo kabla ya tozo! Hapo ndio utajua pesa inayokusanywa sio kwa ajili ya ujenzi wa chochote, bali kulipia madeni aliyokopa Magufuli. Kwa sasa hakuna wajinga wa hivyo.
 
Hongera sana chama kubwa
Tunasema kaz iendelee.usikivu huu ni wa kiwango cha hali ya juu sana
Hata vijana wa ufipa nipo nao wanasema kazi iendelee
Sasa sikiliza wewe bwege...

Aliyebuni, kuunda na kusimamia wizi ni CCM
Anayetafuta namna ya kumaliza wizi ni CCM


Ngoja sasa nikutafsiriye maana ya nukuu hiyo...

Hatuwezi kutatua matatizo yetu
kwa fikra zile zile tulizotumia kuyaunda!
 
CCM chama cha wanyonge na walalahoi kamwe wasingekubali Wananchi waendelee kulalamika,

VIVA CCM VIVA

VIVA SAMIA VIVA

VIVA KINANA VIVA

VIVA CHOGOLO VIVA

VIVA SHAKA VIVA

VIVA......... VIVA
Hahahahah.........CC ambayo Mwenyekiti wake ni SSH yaelekeza Serikali kuangalia upya tozo. Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais SSH yaanzisha tozo na kuunga mkono kwa nguvu zote Na kuamuru wananchi ambao hawapo tayari kwa tozo wahamie Burundi.
Nani anamwelekeza nani kati ya SSH wa CC na SSH Rais wa Serikali inayokamua wananchi kupitia tozo?
 
Habari za siku nyingi, Mkuu.
 
Salama TUJITEGEMEE, tumeruka m*, tunajitahidi tusikanyage m*, je tutaweza kukwepa? Naona kama vile hatuponi!
Mkuu, Ninaamini uwepo wenu na kuendelea kutoa maoni ama ushauri na wakati mwingine kukemea inaweza kusaidia tukakwepa kukanyaga ***i.

Kibaya, Baadhi yenu mnakaa kimya Hata bila kusema chochote kiasi wengine tunashuku labda 'mnakula chakula cha nyuki'. Ingawa wakati mwingine nafikiria labda baadhi yenu mpo kimya kwa aibu baada ya kugundua makosa mliyofanya kuwezesha kukwepa m* wakati mbele mnaona kabisa mguu unapelekwa kwenye mwelekeo wa *****si.

Kwa hiyo Nina shauri tuungane Pamoja kuhakikisha tunapona wote bila kujali tofauti zetu. Mkuu Nina imani kubwa tutapona, tutimize tu wajibu wetu.
 
Zitazamwe upya Zina Nini? Hapa makelele haya ni kwa sababu tozo za banks zinawagusa watu wa mjini ambao wamekuwa Wanufaika wa jasho la watu wa Vijijini miaka na mikaka..

Naomba niwe wazi.kabisa ikiwa hizo tozo zitafutwa au vinginevyo na zikaathiri Kasi ya miradi Vijijini mjue kabisa kwamba hamna kura yangu..

Hakuna mwanakijiji ana account banki hayupo na ni Wana Vijijini ndio husafiri mamia ya kilomota kutafuta huduma..

Sasa nyie sikilizeni makelele ya watu wa mjini harafu sie wa mashambani tuendelee kutumia then tukutane 2025..

Hata hizo ziara zenu mnaishia Mijini Wala hamuendi Vijijini Kwa sabaymnakwepa Vumbi.
 
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM) imeielekeza Serikali kuchukua ushauri wa wananchi kuhusu tozo sambamba na kujielekeza katika kubana matumizi ya serikali na kutanua wigo wa kodi.
Hakuna lolote hapa ni baada ya kuona kamnpuni kubwa kama Vodacom zimeanza kupoteza faida hivyo kuogopa kudodoresha uchumi wa nchi.
hawa ccm sio wa kutuonea huruma kabisa na wasitudanganye kwani tunawajua sana!
 
Chama ndiyo mwenye mali, kwa hiyo lazima tuimamie serikali,"

Wananchi ndiyo wenye mali, chama cha siasa kinashawishi sera tu.

CCM iondokane na udiktekta kwa kuwafanya wananchi mateka. Kupewa ofisi ya kisiasa kwa muda wa miaka mitano hakuwapi CCM na serikali yake kuwanyima uhuru walipa kodi kuuliza maswali au wakae kimya huku wakiona mali yao yaani kodi wanazolipa pamoja na tozo zikitumiwa kiufujaji kwa kununua magari ya VX8, ziara zinazokuwa na misururu ya makumi ya magari ya kifahari kwa kisingizio cha kuchaguliwa ndiyo maana CCM na serikali yake inatumia vibaya rasilimali za wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…