Mkuu unaweza ukawa umeandika kwa ufupi sana lakini mimi naona hii hoja yako ni kubwa sana sana kuliko ulivyoiweka.
Nimeona umeweka heading inayogusa hisia za wanasiasa wakongwe na wanaharakati wa siasa nchini. Kurudi kwa old gang maana yake ni kupanga safu za watakaokuja kuweka wagombea kwenye nafasi za dola.
Ninaona CCM inajimega kwa nguvu kubwa kuliko ilivyotarajiwa. Ukiondoa ukatili wa kisiasa wa awamu ya tano, ninaiona safu ya CCM asili wakikosa hata dawati ndani ya CCM Maslahi.
Ninaiona Siasa ya ushindani mkali sana ikirejea kwa nguvu zote na hili litatokana na karata watakaypicheza wapinzani kuelekea uchaguzi mkuu 2025 na zijazo. Uwepo wa CHADEMA kwenye siasa za nchi hii unajengq uwiano wa mwenendo wa siasa na ushindani wa sera.
Kitendo cha kuukandamiza upinzani ni makosa makubwa sana. Ninatamani kuona siasa za ushindani zinashika kasi ili kuharakisha maendeleo ya nchi.
Kataa CCM uliokoe Taifa