Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Mpo salama!
1. CCM ni chama Dola, kikongwe na ambacho kimefanyia mambo mengi mazuri nchi yetu ikiwemo Umoja wa kitaifa tangu 1961 mpaka hivi karibuni ambapo kidogo mambo ndio yameanza kukorogana. Umoja wa kitaifa hapa tunazungumzia kiwango kidogo cha Ubaguzi wa kikabila na udini. Kwa hilo CCM imefanya kazi nzuri.
2. Miundombinu na ujenzi wa huduma za kijamii pia wamejitahidi ingawaje zipo kasoro kadhaa lakini wanajitahidi ukilinganisha na nchi nyingi za Afrika.
3. CCM ni Chama cha kijadi. Yaani kwa sehemu kubwa kina mawazo ya kijadi na kitamaduni. Ingawaje mfumo wanaotumia wa democrasia wameukopa kwa Wakoloni lakini fikra na mitazamo yao ipo kijadi.
4. Ujadi huo ndio unaopelekea vurugu zote unaoziona hivi Leo. CCM inaparangana kupingana na Usasa. Huku Wakati ni Ukuta.
5. Kwenye siasa za jadi. Mkubwa hakosei. Kwenye siasa za jadi. Hakunaga haki na usawa baina ya Mkubwa na Mdogo. Kanuni ni Mkubwa hakosei. Na utatakiwa kumheshimi kilazima ima amekosea au hajakosea. Hizo ndio siasa za kijadi.
6. Siasa za kijadi, Chama Dola ndio serikali, ndio Chama Baba. Na ujadi unasema sikio halizidi kichwa. Pia aliyetangulia kuona jua(Baba) ndiye ataongoza daima.
7. Siasa za kijadi, Paja la kuku atapewa Baba Huku Mama na watoto wakijua watagawana vipapatio, na miguu huko.
8. Kwa siasa za kijadi hakuna namna Mtoto akala Paja kama Baba. Hivyo CCM kama Baba ataendelea Kula mapaja na kuamua amgawie mtoto yupi mnofu wa kueleweka.
9. Gen Z hawaamini kwenye Siasa za jadi hapa ndipo mipishano na vurugu zinapoanzia.
10. GenZ wanaamini hata mkubwa anaweza kuwa kubwa jinga. Hata Wahuni na wapumbavu huzeeka. Na hivyo ule Msemo wa jadi kwamba Wazee ni hazina na wenye hekima haufanyi kazi kwa GenZ
11. GenZ Wanaamini Sikio linazidi kichwa kisayansi. Na wamethibitisha hayo mara nyingi. Na makosa ya wazee yanafanya Imani ua vijana kuwa halisi.
12. Ile kauli ya mkubwa hakosei GenZ hawaitambui. GenZ hawaongozwi kijadi na Imani zisizo na kichwa wala miguu.
Wanaona Mkubwa anakosea uwaambie mkubwa hakosei. Ni kama unawaona hamnazo. Unawaletea mazingaombwe.
13. Nimeshuhudia propaganda nyingi za CCM zikigonga Mwamba kwa GenZ kwa sababu vijana wa GenZ wanatumia zaidi akili zao na wapo huru kufikiri. Tofauti na vizazi vya nyuma ambavyo ukimwambia kupiga mlunzi usiku ni kosa au hatari wanaamini na hawapigi. Lakini GenZ huwezi waambie hiyo kitu utaishia kudharaulika.
14. GenZ huwezi tumia mambo ya kijadi kama Dini na Imani za kufikirika sijui Mungu kafanyaje, sijui Uislam sijui Ukristo kama nyenzo ya kuwavuruga na kuwagombanisha. Hizo ni mbinu za kijadi ambazo CCM walizitumia katika vizazi vilivyopita.
15. Leo niliona Clip moja ya wanaume kama wanne wakiwa wamejirekodi wakiwa wamefunga nyuso zao. Wakisema wanataka walipwe kama wenzao walivyolipwa kufanya maandamano. Na wasipolipwa watatoa sijui siri sijui wataanika vitu gani.
16. Nilipitia comments katika video hiyo kwa hakika kizazi cha sasa kimebadilika. GenZ wanajua lile ni igizo na walionyuma ya igizo ni kina Nani
17. GenZ sio kizazi chetu ambacho kilikuwa kinalia kikiona Yesu anasulubishwa. Vitoto vya Siku hizi hata vikiwa na miaka miwili hata uweke movie ya kutisha haviogopi vinajua ni filamu ya kuigiza sembuse uwaletee video za kisiasa.
18. Uhai wa CCM usitegemee vyombo cya Dola kwa sababu miaka sio mingi ndani ya vyombo vya Dola wataanza kuandikishwa GenZ. Ambao mindset zao sio za kijadi.
19. Lazima CCM iwe na Plan. Iangalie inafanya namna gani ku-copy na kizazi hiki na kijacho.
Kufikia hapo sina la ziada
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam