Uchaguzi 2020 CCM bado imekumbatia mfumo dume? Kati ya majimbo 200+ ni wanawake 14 tu ndo wamepenya kugombea Ubunge

Uchaguzi 2020 CCM bado imekumbatia mfumo dume? Kati ya majimbo 200+ ni wanawake 14 tu ndo wamepenya kugombea Ubunge

Hivyo vigezo unavyosema wanavyo umevipamaje? Wana vigezo kulinganisha na nani?
Kuna walioomba na vigezo wamekidhi lakini wameachwa!

Fahamu hicho ndicho kilichotokea kama ulikuwa hujui!
 
Hivyo vigezo unavyosema wanavyo umevipamaje? Wana vigezo kulinganisha na nani?

Nilishakuandikia huko juu kuwa Kigezo cha msingi kimojawapo ni pamoja na elimu na kwa mujibu wa Katiba ni kujua kusoma na kuandika,
Nikakuandikia kuwa lakini wao wako mbali zaidi ya kujua kusoma na kuandika na kwamba wana elimu za juu na wamebobea ,
Achilia mbali vigezo vingine ikiwemo uzoefu wa utumishi wa Umma kwa miaka mingi lakini bado wameachwa,

Sasa utakuwa umenielewa? Au bado?

Au uniambie hao wanaume wengi walioteuliwa wenyewe wana vigezo gani vya kiwazidi hao wanawake waliokatwa?
 
Kusoma na kuandika ni kigezo kimojawapo lakini pia kubobea kwenye elimu sio kitu pekee cha kumfanya mwanamke ateuliwe au achaguliewe kwenye nafasi aliyoomba.
Inawezekana akawa bora zaidi kwa maslahi ya nchi pale alipo zaidi ya alichoomba au akachaguliwa aliye bora zaidi yake, waliowaweka kwenye mizani wanajua.
Sio kila anayetaka kuwa mbunge atapata sababu ni mwanamke, wacha vyake vichague kwa taratibu zake kwa maendeleo ya taifa
 
Jitahidi kutafuta maarifa uweze kuimarisha kiwango chako cha ufahamu wa mambo itakuwa kwa faida yako na wengine kwenye jamii na Taifa kwa ujumla!

Tafakari!
 
Hatuangalii mfumo tunaangalia uwezo wa kuongoza. Mbona uarabuni hawana wanawake mabungeni lakini wanaendelea? Hayo ni mambo ya wazugu hutoyaweza!
 
CCM ya Meko sio rafiki kwa akina mama .
1. Ummy
2. Gekul
3. Ndalichako
4. Stella Manyanya
5. Doroth Kilave
6. Jesca Msamvatavangu
7. Hamida
8. Salma Kikwete
9. Jenister
10. Leah Komanya
11.Tulia
12. Anne Kilango
13.Bonna Kamoli
14.Angelina Mabula

Hakika inasikitisha CCM badilikeni. Wapeni akina mama nafasi.
katika siasa vya vyama vingi, kila chama hujitahidi kuingiza kikozi cha kuchukua ushindi
Usawa wa kijinsia huangaliwa zaidi kwenye chama kimoja au kwenye nafasi za Uteuzi
 
CCM ya Meko sio rafiki kwa akina mama .
1. Ummy
2. Gekul
3. Ndalichako
4. Stella Manyanya
5. Doroth Kilave
6. Jesca Msamvatavangu
7. Hamida
8. Salma Kikwete
9. Jenister
10. Leah Komanya
11.Tulia
12. Anne Kilango
13.Bonna Kamoli
14.Angelina Mabula

Hakika inasikitisha CCM badilikeni. Wapeni akina mama nafasi.
Wanawake jumla wapo 27 lakini bado Ni wachache sana ,zidumu fikra za mwenyekiti wa ccm ? Zidumuuuu.
 
Jitahidi kutafuta maarifa uweze kuimarisha kiwango chako cha ufahamu wa mambo itakuwa kwa faida yako na wengine kwenye jamii na Taifa kwa ujumla!

Tafakari!
Ufahamu wako usikufanye ukaona wenzio hawana ufahamu.
Umepungukiwa sana na ufahamu wa kufahamu kwamba kile Usichokijua kuhusu kuwepo idadi ndogo ya wagombea wanawake ndicho kinachokufanya uone rais Magufuli ana mfumo dume ambao unashindwa kuuthibitisha
Wanawake hawajabagulia kwenye uchaguzi wala hawajanyimwa haki, nenda kawaulize wajumbe kuhusu hao waliokatwa watakufahamisha sababu nawe utaongeza ufahamu
Pole
 
Samahani sana ndugu usitake kunifarakanisha na Mheshimiwa Rais!

Namheshimu sana!

Kwani wewe vipi?

Kwanini unataja majina ya watu?

Huu mjadala unafanyika kwa maudhui ya ujumla kwanini unamtaja Mheshimiwa Rais?

Wewe ngoja nifanye kukustahi tu sababu nimegundua huna uwezo wa kujadili hoja !

Mimi napenda ku urgue na wenye akili kubwa na siyo wewe!

Nimekushauri vizuri tafuta maarifa na ufahamu zaidi wa mambo fanya upembuzi yakinifu,

Nimekueleza kwa taratibu kabisa lakini bado huelewi.

Walimu wanakazi kubwa sana.
 
22 August 2020

Halima Mdee asema,''Uwepo wa Kinamama, ni kutambua nguvu zao.!

Wito kwa kina mama katika kuwania nafasi ndani ya vyombo vya maamuzi
Source : Swahili Villa
 
SHANGWE ZA SUZAN LYIMO ALIVYORUDISHA FOMU/WAMAMA WATIA FORA

25 Agosti 2020
Dodoma, Tanzania

Mgombea Urais kupitia chama cha Demokrasia Makini, Cecilia Mmanga awapa makavu waandishi wa habari

Mgombea Urais kupitia chama cha Demokrasia Makini, Bi. Cecilia Augustino Mmanga akizungumza namna atakavyoboresha baadhi ya sekta ikiwemo ya uandishi wa habari, alipofika ofisi za NEC Dom kurejesha fomu na kisha kupitishwa rasmi na Tume ya Taifa kuwa mgombea wa Urais mwezi Oktoba 2020.

Cecilia Mmanga ataitazama sekta ya afya maana haipo vizuri labda kidogo sana mjini pia anashangaa gharama za vipimo kuwa juu kuliko dawa, mgonjwa anapimwa anaambiwa kipimo tshs 400,000 kipimo cha T-Scan halafu anaambiwa negative (hakuna matatizo) ndiyo maana waTanzania wanakwepa vipimo na kufia majumbani hivyo hilo ataliangalia.

Cecilia Mmanga anasema Huduma bure za afya hakuna kwa mama, mtoto na wazee.....
 
25 Agosti 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Halima Mdee na Suzanna Lyimo warejesha fomu

Halima Mdee na Suzanna Lyimo warejesha fomu kwa msimamizi wa uchaguzi na kila kitu kipo sawa baada ya uhakiki na hivyo kuteuliwa rasmi kugombea ubunge ktk majimbo yao

Majina yao yatabandikwa rasmi, ili kama kuna pingamizi wateuliwa wayajibu mapingamizi hayo.
 
Asia Msangi mgombea ubunge jimbo la Ukonga Dar es Salaam

5 September 2020
Dar es Salaam, Tanzania

SUSAN LYMO AZINDUA KAMPENI KINONDONI / TUNAENDA NA MAENDELEO YA WATU SIYO VITU

5 September 2020
Tunduma, Songwe
Tanzania

Kina mama Tunduma waweka ahadi kura ni kwa CHADEMA ngazi ya Urais, ubunge na udiwani

7 September 2020
Geita, Tanzania

PENEZA WA CHADEMA ALIVYOJINADI GEITA MJINI || AWAHAKIKISHIA WACHIMBAJI MAENEO YA UCHIMBAJI

Mgombea ubunge kupitia Chadema jimbo la Geita mjini Upendo Peneza, amesema jambo la kwanza kufanya mara tuu baada ya kuchaguliwa ni kuhakikisha wakazi wa Geita wanaojishughulisha na uchimbaji wanapata maeneo ya uchimbaji madini ya dhahabu.

Akizungumza na wakazi wa mji wa Geita katika eneo la msufini ikiwa ni uzinduzi wa kampeni katika jimbo hilo Peneza amesema kupatikana kwa maeneo ya kuchimba dhahabu kutafungua fursa za kiuchumi kwa vijana na wanawake wa mji huo.

Amesema akichaguliwa kuwa mbunge kazi kubwa itakua ni kuwawakilisha na kuwasemea wananchi na kuahidi kutoa fedha zake kwa ajili ya mikopo ya kina mama kama alivyo fanya miaka iliyopita akiwa mbunge wa viti maalum.
Source: mwananchi digital
 
07 September 2020
Kamanda Husna katika Kampeni za Chadema, Wilaya ya Sumbawanga Mjini

7 Sep 2020
Bi Husna A. Said Mwenyekiti Bawacha Wilaya ya Chato Mkoa Geita, mgombea Ubunge Viti Maalumu Chato.
 
Back
Top Bottom