CCM Dodoma: Hakuna haja ya Katiba Mpya Tanzania kwa sasa, Katiba ya Mwaka 1977 bado inafaa

CCM Dodoma: Hakuna haja ya Katiba Mpya Tanzania kwa sasa, Katiba ya Mwaka 1977 bado inafaa

Waambie pia ni wapumbavu maana Samia akisema anataka katiba ibadilishwe wao watakuwa wa kwanza kumpongeza kwa sababu ni wapumbavu...
Hapa ndio upumbavu wenu ulipo,,!

Chaguzi zote mlizoangukia Pua Magufuli alikuwa rais?

Nyie ni wapumbavu mana hamjui shida yenu ipo wapi
 
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, imesema hakuna haja ya kuwa na Katiba Mpya kwa sasa kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 bado inafaa.

Please elaborate in details!

Propagandaz are parts of us! Let’s help each other!?!
 
katiba sio ndo solution ya mambo.inshu ni nchi na wananchi kuwa kitu kimoja.utaifa na uzalendo.Taifa likiwa na spirit ya utaifa kwanza na uzalendo ,watu watawaza kulijenga taifa na kulilinda kwa udi na uvumba,just like China.Naamini hiyo katiba inayoliliwa na wachache sio kwa muktadha wa kulilinda taifa ,Bali kwa muktadha wa namna ya kupenyeza maslahi ya wazungu.

Bado hujatoa muafaka!! Tunalimalizaje hili??!?
 
Watashinda tu! Na wataendelea kutawala tu!

Kwa maana hiyo kuna kitu wanaohitaji katiba wanatakiwa kufanya.

Kama kweli wanahitaji mabadiliko kwenye katiba inabidi waache siasa za zimamoto, wajikite kwenye kujenga vyama imara vyenye misingi imara kwa wananchi.

Mabadiliko ya kisiasa yanahitaji watu na kuwapata hao watu kunahitajika kujitoa kwelikweli kwa muda na pesa sio wale ruzuku na kusubiria mtu akatwe CCM wamdake ili kuongeza kura, wala sio kusubiri kampeni wapige blahblah halafu wakishindwa wakimbie nchi.

Upinzani ni muhimu sana kwa afya ya taifa lakini uwe upinzani kwa vitendo na sio upinzani wa viongozi kujipatia ulaji huku vyama vikizidi kudumaa.
 
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, imesema hakuna haja ya kuwa na Katiba Mpya kwa sasa kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 bado inafaa.
Pumbavu zaidi Sana, warudishe pesa zetu zilizotumika kuanzi time ya warioba mpaka bunge la katiba
Aliyeruhusu mchakato ni mwenyekiti wao taifa wakati ule
 
Ukiachana na unafiki utafikia malengo yako!

Hakuna wanafiki zaidi ya wale wanaoanzisha chama pinzani halafu wanakosa mikakati mbinu na kuishia kulaumu chama kilichokua madarakani ati kinawaonea

Kwani hamjui upinzania ni mpambano!?

Hebu jiongezeni bhana... kama hamuwezi acha kulialia basi acheni upinzani msiouweza
 
katiba sio ndo solution ya mambo.inshu ni nchi na wananchi kuwa kitu kimoja.utaifa na uzalendo.Taifa likiwa na spirit ya utaifa kwanza na uzalendo ,watu watawaza kulijenga taifa na kulilinda kwa udi na uvumba,just like China.Naamini hiyo katiba inayoliliwa na wachache sio kwa muktadha wa kulilinda taifa ,Bali kwa muktadha wa namna ya kupenyeza maslahi ya wazungu.
Upumbavu nao no mzigo
 
Naunga mkono hoja,CCM ni chama mama kukitoa madarakani itakuwa ngumu,ikitokea siku hiyo dunia itasimama,hitaji la wananchi sio katiba Bali ni Maisha bora kwa kila Mtanzania...
Kuna siku nyinyi ndo mtalilia katiba mpya. Kumbuka wakati Ni ukuta . Ipo siku mtasema laiti kama tungekubali siku zile walipokuwa wakituomba kwa katiba mpya
 
Kuna siku nyinyi ndo mtalilia katiba mpya. Kumbuka wakati Ni ukuta . Ipo siku mtasema laiti kama tungekubali siku zile walipokuwa wakituomba kwa katiba mpya
Haitatokea hii mkuu,ikitokea ni baada ya miaka 1000 yaani millennium moja .
 
Hawa wanataka siku nchi ikifikisha maraisi 20 basi tutegemee ama kuwa na viwanja ishirini vya ndege vijijini ama mabenki ishirini ama mataa ya kuongozea wanyama endapo maraisi hao wametoka vijijini,, ninachokisema ni kwamba katiba iliyopo inahitaji busara sana ila raisi aweze kutenda haki katika kugawa rasilimali za taifa na mengineyo.

Umoja aliotuachia baba wa Taifa ambao ndio unaotufanya tuheshimike katika mataifa mbalimbali duniani umevurugwa na katiba hii.sasa ili walau turejeshe umoja na mshikamano wetu basi busara ya hali ya juu inahitajika,,lakini kwa jinsi wengi wa viongozi wetu ni vigeugeu na wasaka fursa basi hatuna budi kuiangalia upya katiba yetu maana wengi hatupo kwa maslahi mapana ya taifa bali kwa maslahi yetu na vyama vyetu.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Futa kauli kuwa katiba inaliliwa na wachache,ama naweunayapata maslahi yako kupitia hii inayonganganiwa na wachache.Katiba mpya tena ya Jaji Warioba ndio mahitaji ya umma wa Watanzania.
Umefanya lini research na kugundua wengi wanataka katiba mpya.
Mimi binafsi sihitaji katiba mpya, iliyopo inatosha
 
Waambie pia ni wapumbavu maana Samia akisema anataka katiba ibadilishwe wao watakuwa wa kwanza kumpongeza kwa sababu ni wapumbavu.

Lakini nawaonya tu msigina katiba ashaondoka katiba itakuwa kaa la moto kwenye uchaguzi wa 2025.

Ccm wajue hakuna tena wa kuwabeba hiyo 2025 uchaguzi utakuwa mgumu kupindukia katika historia ya Taifa letu.
Haya maneno mbona yamekuwa kila uchaguzi?
 
Katiba mpya inaombwa Sana na wanasiasa, ukiuliza watakuambia tunahitaji time huru

Hiyo tume wanayoitaka haitoweza wapatia dola kama hawana vyama imara vyenye misingi imara kwa wananchi.

Hivi kwanini hawa watu hawajui kukuza mtaji wao?

Chadema acheni blablah tuajirini tuwape mbWinu za kutoboa🤣🤣
 
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, imesema hakuna haja ya kuwa na Katiba Mpya kwa sasa kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 bado inafaa.
Kama wangekuwa wanaiheshimu katiba hii tungewaelewa kidogo, lakini ni kwamba hata hii iliyopo hawaiheshimu sasa hawa ni watu au mapimbi?
 
katiba sio ndo solution ya mambo.inshu ni nchi na wananchi kuwa kitu kimoja.utaifa na uzalendo.Taifa likiwa na spirit ya utaifa kwanza na uzalendo ,watu watawaza kulijenga taifa na kulilinda kwa udi na uvumba,just like China.Naamini hiyo katiba inayoliliwa na wachache sio kwa muktadha wa kulilinda taifa ,Bali kwa muktadha wa namna ya kupenyeza maslahi ya wazungu.

Ukiwa kiazi ni kiazi tu!! Kwani rasimu ya katiba iliyopoa haina uzalendo, utaifa?? Hivi mnakuacha na akili ndogo hivi halafu mnataka kuendeleza nchi?? Katiba ndio hutoa mwongozo wa haki, stahiki, taratibu za uendeshaji nk. Ndio mwanzo wa kila kitu.

Moja ya tatizo la katiba hii ni namna uongozi unapatikana! Je ni sahihi kwa Rais kuendesha atakavyo? Kuteua viongoz atakavo? Rais anayetawala serikali, bunge na mahamaka? Madaraka ya Rais wa nchi hii ni makubwa sana. Hupendi siku moja uchague mkuu wa wilaya yako badala ya kuletewa na Rais kwa matakwa yake?

Kama wewe ni kiwakilishi cha wengi katika nchi hii - tuna kazi sana kutoka hapa. Hujui kuwa kuna rasimu ya katiba ambayo sio CCM wanaopaswa kuamua ipite au la. Ni kura ya maoni ya raia wa nchi hii.

Kama unadhani wanaopaswa kuamua ni CCM - sishangai kuwa mbaogopa kuwapa wengine haki na stahiki zao! Uonevu dhidi ya wasio na nguvu!!
 
Kweli Siasa huizidi Elimu,ingawa kuexpire kwake ni kwa dakika kulikobebwa na majuto makubwa
 
Back
Top Bottom