CCM Dodoma: Hakuna haja ya Katiba Mpya Tanzania kwa sasa, Katiba ya Mwaka 1977 bado inafaa

CCM Dodoma: Hakuna haja ya Katiba Mpya Tanzania kwa sasa, Katiba ya Mwaka 1977 bado inafaa

Katiba ya sasa bado inafaa ila kuna mambo machache yaangaliwe. Kwa mfano mshindi urais sharti apate zaidi ya asilimia 50 ya kura. Kama hakuna mshindi wawili wenye kura nyingi waende round ya pili ya kupigiwa kura. Bila hivyo kuna siku mshindi anaweza kua na hata asilimia chini ya 10 kulingana na wingi wa wagombea na mtawanyiko wa kura kwa wagombea.
 
Siyo kila mwanasiasa aliyepo madarakani, bali mwanasiasa aliyepo madarakani,asiye na akili wala hekima.
Hao walioko madarakani wenye hekima wamesema nini? Watoke wapingane na hao wapuuzi ili twende nao pamoja.
 
INA MAANA KATIBA MPYA NI HISANI YA CCM KWETU NA TAIFA?
 
Katiba ya mwaka 1977 inafaa na inaongoza mwaka 2021.... okay sawa
 
Sasa mbona hamuifuati mnaikanyaga hovyo? Mfano ni job ndugai
 
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, imesema hakuna haja ya kuwa na Katiba Mpya kwa sasa kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 bado inafaa.

====

HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, imesema hakuna haja ya kuwa na Katiba Mpya kwa sasa kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 bado inafaa.

Kimesema katiba hiyo imewezesha kufanyika kwa mabadiliko ya uongozi wa juu serikali, Rais Samia Suluhu Hassan, akishika madaraka bila kuwapo na mgogoro wowote baada ya kutokea kwa kifo cha Rais John Magufuli.

Akizungumza jana na waandishi wa habari mara baada ya kufanyika kikao cha halmashauri kuu hiyo, Mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Godwin Mkanwa, alisema:

"Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dodoma tunaona Katiba hii ya toleo la 1977 bado inafaa sana na hakuna ulazima wa kuichokonoa, hakuna ulazima wa kutafuta Katiba Mpya wakati hii imetupitisha salama."

Mkanwa alisema katika Katiba Pendekezwa, kuna kifungu kinasema kuwa endapo Rais akifariki dunia akiwa madarakani, lazima zipite siku 90 na baada ya hapo uitishwe uchaguzi wa kujaza nafasi hiyo.

"Halmashauri Kuu inaona kama Katiba Pendekezwa ingekuwa ndiyo Katiba inayotumika sasa, isingetutoa salama,” alisema.

Zikiwa zimebaki siku nne kabla ya kufanyika Mkutano Mkuu wa CCM wa kumpitisha Rais Samia kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, halmashauri kuu hiyo ya Dodoma imewaomba wajumbe wa kumpitisha kwa asilimia 100 kutokana na uwezo alionao.

Mkutano huo maalum unatarajiwa kufanyika Aprili 30 mwaka huu jijini Dodoma.

Mkanwa aliwaomba wajumbe kumchagua kwa kishindo ili kumpa nguvu ya kutekeleza majukumu yake.

"Kama ambavyo tumemsikia kwa siku hizi 37 tangu awe Rais wetu, ameonyesha mwelekeo ambao kila mtanzania amekubali, tumchague kwa asilimia 100 ili sasa tumpe nguvu ya kutekeleza majukumu yake ipasavyo," alisema.

Vilevile, alisema halmashauri kuu hiyo imetoa azimio la kumpongeza Rais Samia na kumpa pole ya kuondokewa na aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dk. Magufuli.

Chanzo: Gazeti la Nipashe
 
katiba sio ndo solution ya mambo.inshu ni nchi na wananchi kuwa kitu kimoja.utaifa na uzalendo.Taifa likiwa na spirit ya utaifa kwanza na uzalendo ,watu watawaza kulijenga taifa na kulilinda kwa udi na uvumba,just like China.Naamini hiyo katiba inayoliliwa na wachache sio kwa muktadha wa kulilinda taifa ,Bali kwa muktadha wa namna ya kupenyeza maslahi ya wazungu.
 
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, imesema hakuna haja ya kuwa na Katiba Mpya kwa sasa kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 bado inafaa.
Wao hawana haja ya mabadiliko,ila watanzania tunayahitaji Sana,kusibitisha hilo utaratibu wa kuipata Katiba mpya ulianza miaka kadhaa iliyopita,ila ulikwamishwa na wachache wanaopata maslahi kwa Katiba iliyopo sasa.
 
katiba sio ndo solution ya mambo.inshu ni nchi na wananchi kuwa kitu kimoja.utaifa na uzalendo.Taifa likiwa na spirit ya utaifa kwanza na uzalendo ,watu watawaza kulijenga taifa na kulilinda kwa udi na uvumba,just like China.Naamini hiyo katiba inayoliliwa na wachache sio kwa muktadha wa kulilinda taifa ,Bali kwa muktadha wa namna ya kupenyeza maslahi ya wazungu.
Futa kauli kuwa katiba inaliliwa na wachache,ama naweunayapata maslahi yako kupitia hii inayonganganiwa na wachache.Katiba mpya tena ya Jaji Warioba ndio mahitaji ya umma wa Watanzania.
 
Back
Top Bottom