CCM Fahamuni kabisa: Kilichofanywa na Asha Rose Migiro ni uhaini na atakilipia

CCM Fahamuni kabisa: Kilichofanywa na Asha Rose Migiro ni uhaini na atakilipia

Jiulize hivi kimantiki:

CHAMA KIMEMFUKUZA, halafu BUNGE LIKAKATAA KUMTOA MAKAMU, nini kitatokea ???

Tena jiulize hivi:

Raisi/Makamu wamechaguliwa na watanzania hata wasiokuwa na chama, unapomfukuza uanachama unawaambia nini watanzania wasiokuwa wana-CCM, kwamba leo hii CCM ikiamua tu ndiyo basi ???

HAKUNA KITU CHA NAMNA HIYOOOOO!
​
Hawawezi wakakataa Kwa Sababu Asilimia 98% ya wabunge ni wanachama wa chama Cha mapinduzi

Wakikataa inamaanisha wanapingana na Maamuzi ya NEC (kamati kuu CCM)
 
Hawawezi wakakataa Kwa Sababu Asilimia 98% ya wabunge ni wanachama wa chama Cha mapinduzi

Wakikataa inamaanisha wanapingana na Maamuzi ya NEC (kamati kuu CCM)
Kwahiyo leo tufanye uchaguzi kwa gharama ya zaidi ya Trillioni 1 kuteua Raisi.

Kesho CCM waamue kuwavua Raisi/Makamu uanachama ndiyo wanapoteza Uraisi ???

Anachokisema Bwana Hamza Johari na wewe ni kwamba kile kipengele cha Impeachment hakina maana yoyote kwasababu zifuatazo:

Mosi, CCM inaweza kufukuza Raisi/Makamu uanachama na akapoteza cheo chake.

Pili, Bunge lote limejaa wabunge wa CCM as a majority.

=================================================================
​
 
Jiulize hivi kimantiki:

CHAMA KIMEMFUKUZA, halafu BUNGE LIKAKATAA KUMTOA MAKAMU, nini kitatokea ???

Tena jiulize hivi:

Raisi/Makamu wamechaguliwa na watanzania hata wasiokuwa na chama, unapomfukuza uanachama unawaambia nini watanzania wasiokuwa wana-CCM, kwamba leo hii CCM ikiamua tu ndiyo basi ???

HAKUNA KITU CHA NAMNA HIYOOOOO!
​

Hapa nimekuelewa, VP ni kiongozi was umma, sio was chama pekee, huku ni kuwanyima haki wananchi wasio wanachama was CCM.
Hii haikubaliki.
 
Hakutakuwa na Rais.
Yaleyale mkuu, nchi itakuwa Haina control sababu wahuni wachache wanaweza pindua meza muda wowote.
Hii mitifuano inaonyesha udhaifu wa mambo mengi sana kwenye mifumo.
 
Kwanza hakuna mahala CCM wamekosea Wala kumvua mtu cheo chake ,wao wame deal na mwanachama wao.

Pili Kwa kutambua huo mchakato uliousema ndio maana Makamu hajafukuzwa Bali amejiuzulu lakini atakuwa ofisini Hadi September 4 lengo ni kukamilisha process za kukabidhiana madaraka.

Sasa sijui umeandika nini, nadhani chuki ndio zinakusukuma kuliko uhalisia.
kwanini wasingesubili baada ya tarehe 4.9.2026 wakamvua uanachama? Mbona wameharakisha sana..Wananchi tunahaki ya kuhoji na kupata majibu.
 
Makamu wa Raisi ni mtumishi wa ummah mwenye kinga dhidi ya mashauri yote ya kisheria.

Kama mahakama tu haziwezi kumshitaki au kumuwajibisha Makamu wa Raisi kwa kosa lolote lile bila idhidi ya bunge, iweje CCM ambacho ni kigenge cha wahuni wawe na nguvu zaidi ya mahakama kutuamilia watanzania milioni 60 hatma yetu ???
​

Duuuh hii mbona inashangaza sana? Yanawezekanaje haya??
 
Makamu wa Raisi akishapelekwa kwenye uchaguzi mkuu na kupita, basi CCM haina nguvu dhidi yake kwa namna yoyote ile. Sababu ni za kisheria kabisa na ziko dhahiri:

Mosi, makamu wa Raisi ni mtumishi wa ummah siyo mtumishi wa CCM.

Pili, makamu wa Raisi anateuliwa na watanzania siyo CCM.

Tatu, makamu wa Raisi anaongoza nchi ya Tanzania siyo nchi ya CCM.
​

Haswaaaa!! Jamani walioko huko kwenye system hawaoni haya??
 
Hapa nimekuelewa, VP ni kiongozi was umma, sio was chama pekee, huku ni kuwanyima haki wananchi wasio wanachama was CCM.
Hii haikubaliki.
Ni Kweli
Lakini fikiria zaidi Nini maana ya chama tawala

Na ukumbuke kuwa Viongozi wanaowekwa wanaowekwa ili wakaifanyie Kazi Ilani ya chama tawala na si vingine.

Hapo ndio Nguvu ya chama tawala Kwa Viongozi wa Nchi ilipo.
 
kwanini wasingesubili baada ya tarehe 4.9.2026 wakamvua uanachama? Mbona wameharakisha sana..Wananchi tunahaki ya kuhoji na kupata majibu.
Kuvuana uanachama kunafuata taratiibu zao za chama sio cheo Cha mwanachama Kwa sababu haviingiliani.

Kwani walivyomtimua sio VP? Barua yake inasema tarehe 4 na Rais karidhia hivyo.
 
Famahamuni haya fika.

Mfumo wetu wa Uraisi ulioanza mwaka 1995 wa mgombea mwenza tumeuiga kutokea nchi ya Marekani, ambapo Raisi na Makamu wake wanateuliwa kwa pamoja, na wanaanza kazi siku moja. Hivyo kinga ambayo anaipata Raisi ndiyo hiyo-hiyo anaipata Makamu wake. Kitaalamu hii tunaiita Functional Immunity (From Civil & Criminal Proceedings).

Emmanuel Nchimbi, unaweza usimpende lakini analindwa na katiba kama ambavyo Raisi Samia alilindwa na Katiba mwaka 2021 wakati akiwa Makamu wa Raisi asiyekuwa anaifahamu hatma yake. Wengi hatukutaka Raisi Samia awe Raisi, lakini Kikwete na Mabeyo ndiyo walimfanya Samia akawa Raisi. Wengi hatukupinga wala kulalamika kwasababu lilifanyika kikatiba.

SASA BASI, nchini Tanzania kuna haya yafuatayo ambayo yako bayana kabisa:

MOSI, Mamlaka ya nidhani (Disciplinary Authority) ya Raisi na Makamu wake ni Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Siyo Msajili wa vyama, siyo Jaji Mkuu, siyo Jeshi na wala siyo NEC ya CCM. Makamu wa Raisi hata kama Raisi hampendi anatakiwa apeleke mashitaka kwenye chama, halafu chama wapeleke mashitaka hayo bungeni ambako wataanzisha mchakato wa kumvua nafasi makamu wa Raisi (A motion of Impeachment), ambao utaishia na azimio maalumu ya kuthibitisha kwamba makamu atolewe au asitolewe (A Resolution Confirming Impeachment).

NEC ya CCM kumvua uanachama Makamu wa Raisi Emmanuel Nchimbi, ambaye kwa barua yake amesema ataondoka kwenye nafasi yake ifikapo tarehe 4 Septemba 2026 ni UHAINI. CCM imepoka madaraka ya Bunge na kutikisa taasisi ya Uraisi.

Fahamuni fika, kwamba leo hii akifariki Raisi Samia kabla ya tarehe 4 Septemba 2026, Raisi wetu atakuwa ni Dr. Emmanuel Nchimbi na siyo mtu mwingine. Hivyo ambacho mnakifanya sasa ni uhuni utakaokuja kuwatokea puani siku siyo nyingi, maana mshajenga mfano mbaya (A Bad Precedent)

PILI, Kinga ya Raisi ndiyo kinga ya Makamu Wake. Raisi na Makamu hawawezi kushitakiwa popote pale. Lengo la kumpa Raisi na Makamu wake kinga ni kuhakikisha ofisi ya Raisi inathibitika ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu makubwa ya kitaifa. Hivyo madai yote dhidi ya Raisi na Makamu ni lazima yapitie bungeni kwanza. Mtu hawezi kuamka tu akasema leo hii hatumpendi fulani basi tumvue uanachama ili apoteze nafasi yake ya Uraisi au Umakamu. Kama hili litakuwa linafanyika, hatutakuwa na nchi bali gulio ya washenzi, ambapo kila muhuni anaamka tu na anamuondoa Raisi akijisikia.

========================================================================

JAMBO LOLOTE BAYA, likimtokea Makamu Wa Raisi, Dr.Emmanuel Nchimbi kipindi hiki hata baada ya kuachia nafasi, sisi tutalichukulia hili kama UHAINI. Kinara wa huo uhaini ni Dr. Asha Rose Migiro na wengine. Mlipoka madaraka ya bunge kwa kuifanya CCM ivumbe Ibara ya 50 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na kwasababu mshaonesha nia ovu, hata baada ya 4 Septemba 2026, tutaangalia kwamba lolote litakalotokea kwa Dr.Emmanuel Nchimbi halikuanzia bungeni, hivyo ulikuwa ni UHAINI usio na uhalali.

JINAI haiozi, wote mliohusika na hili sakata, ombeni sana MUNGU hata siku moja asiingie mtu mwendawazimu kwasababu mtanyongwa na kupigwa risasi barabarani kama wanyama. Hili wala haliitaji ushahidi, tumeona mkivunja katiba waziwazi na kufanya mambo ambayo yanatishia usalama wa Makamu wa Raisi.
========================================================================

Wajinga wengi watatoa mfano wa kuondolewa kwa Aboud Jumbe Mwinyi, lakini ukweli ni kwambwa mwaka 1984, Mwinyi alikuwa Makamu wa Pili wa Raisi, ambaye aliongoza Zanzibar iliyokuwa haina hata KATIBA yake. Tena kubwa zaidi ni kwamba alikuwa anateuliwa na Wazanzibari tu, siyo watanzia wote.

Hili la sasa litasababisha matatizo makubwa mnoooo siku za karibuni.
=========================================================================

Wiki chache zilizopita wanasheria wa Tanzania wameenda ICC wakiongozwa na mwanasheria mkubwa ambaye jina lake hatutalitaja hapa. Kinachoendelea huko duniani ni kibaya na hata hii tume ya pili haitaweza kukizuia.

Binafsi huwa nasema hivi: NI SUALA LA MUDA TU..........


​
Na Migiro ni Dr wa Sheria
 
Mada hii ni ngumu sana. Lazima uwe na ushahidi yakinifu wa kupinga ama kukataa hoja hapa.
===
Si kutaka kukutoa kwenye hoja ya msingi ya uzi huu. Lakini kwa elimu ya wengi na kwa sisi raia wa kawaida, unaweza kutusaidia kutufafanulia ni namna gani jambo hili lilitokea kuanzia Maamuzi ya Makamu wa Rais kujiuzulu hadi kikao kikuu cha chama kuamua kumvua uanachama makamu wa Rais lina faidishaje maslahi na usalana wa Taifa au lina hatarishaje maslahi na usalama wa Taifa la Jamhuri ya Muungano Tanzania?

Kama mkuu hutaweza kujibu hapa unaweza kuanzisha uzi mwingine tutakuja huko kupata majibu.

Natanguliza shukrani kwa utayari wa kutupatia majibu sisi raia wa kawaida.
 
Makamu wa Raisi akishapelekwa kwenye uchaguzi mkuu na kupita, basi CCM haina nguvu dhidi yake kwa namna yoyote ile. Sababu ni za kisheria kabisa na ziko dhahiri:

Mosi, makamu wa Raisi ni mtumishi wa ummah siyo mtumishi wa CCM.

Pili, makamu wa Raisi anateuliwa na watanzania siyo CCM.

Tatu, makamu wa Raisi anaongoza nchi ya Tanzania siyo nchi ya CCM.
​
Hapana Mkuu
Dora Ina shikwa na chama Viongozi wa Nchi ni Watu wanao teuliwa na chama ili kutekeleza Ilani ya chama tawala

Kwa hiyo Viongozi wakubwa wa Nchi lazima wafanye Kama chama tawala kinacho taka

Labla kungekuwa na wagombea Urais binafsi ndio kungekuwa hamna Mtu wa Kumwambia Raisi Kitu Wala kumtoa madarakani isipo kuwa Bunge la Jamhuli ya muungano wa Tanzania.
 
Umeandika takataka... Tena uvundo uliooza

1. Rais Samia hajamuondoa nchimbi uVP, Bali nchimbi ndiye alibandika huko instagram na akampa mh rais taarifa.
-hivyo mh. rais alithibitisha maamzi ya nchimbi (soma katiba kinukamto wewe)

2. sifa mojawapo ya kuwa makamu wa rais ni lazima uwe mwanachama wa chama cha kisiasa, alipofukuzwa uachama tayari muda huo huo alikoma kuwa VP, na hatua hyo ilifuta notis yake ya hadi tarehe 4 sept.
-hapa hakuna mutual agreement (ni tofauti kabisa na alivyoondoka mh mpango)

3. mlitaka kumtumia VP kama mashine ya kuendeleza uanaharakati ikulu, hyo imekula kwenu.

4. ikulu ina utaratibu wake, si ombi ni lazima VP awe mtii kwa bosi wake na chama chake kilichompa ridhaa.
-ikulu si makao makuu ya tecdema kwamba kila ndezi anaweza fanya harakati.

5. Hata asingejiuzulu, kwa mwenendo wake lazima angevuliwa uanachama, na hapo lazima angeachia uVP.
 
Kuvuana uanachama kunafuata taratiibu zao za chama sio cheo Cha mwanachama Kwa sababu haviingiliani.

Kwani walivyomtimua sio VP? Barua yake inasema tarehe 4 na Rais karidhia hivyo.
ok kama ni hvo sahivi ni VP asiyekuwa na Chama..Je, katika historia ya nchi yetu kumewahitokea VP asiyekuwa na chama cha kumuakilisha? KATIBA inasemaje na SHERIA za nchi zinasemaje.
 
Tanzania mwananchi hana haki, we ishi tu kusindikiza miungu watu wanaojiona wanahaki
 
Back
Top Bottom