JF ya miaka ile tulijadili mambo kama haya. JF ya leo inashabikia hata kama hakuna mantiki. Kuna mtu hapa JF aliuliza akitaka kuelezwa kama kweli hadi leo hii, mwaka huu, kwa mfumo huu wa nchi, kuna chama cha upinzani kinategemea kushinda uchaguzi? Wapo wapiga kelele kama hawana vichwa , wakaripuka! Wengi wao wako CHADEMA, wanaamini kila anayekosoa CDM ni CCM. Hata wabunge wao walipowakosoa, wao wakasema hameni kama munataka. Kuna umbumbumbu ndani ya chama kiasi kwamba huwezi kuwashauri. Ukweli hawatapata nafasi ya kushika dola.
Sasa wanasema tutaibiwa, ambao ni umbumbumbu pia. Kama unajua utaibiwa kwa nini uliingia kwenye uchaguzi? Unajua uwanja hauna magoli wewe unaingia na kupoteza muda wako kiasi hicho, huku ukijiandaa kulalama! Stupidity of highest order!