CCM hamtawaweza walahi. Hiyo Kete ya Dudu baya na magenge mengine kama imewachota kirahisi hivyo sijui kete zingine

CCM hamtawaweza walahi. Hiyo Kete ya Dudu baya na magenge mengine kama imewachota kirahisi hivyo sijui kete zingine

Nashangaa sana mtu unawaza ccm itoke madarakani. Kwa upinzani upi tulionao ambao unaweza kuongoza endapo ccm ikitoka? Ni kweli upinzani kuna wakati unakuwa na nguvu lakini ukiwapima hawawezi kuwa mbadala wa ccm kwa sababu wao sera zao hubadilika kutokana na kiongozi wa ccm aliopo madarakani. Kifupi ni kwamba upinzani umeshindwa kujijenga na ukaeleweka wenyewe kwa sera zao badala yake umekuwa ukipendwa endapo ccm inafanya vibaya. CCM ikifanya vizuri watu wanawasahau hapo ndipo wanaanza kuzusha uzushi kwa kiongozi aliopo madarakani na propaganda kibao.

Upinzani ulipaswa ujijenge na itikadi yao na watengeneze kizazi cha itikadi yao ambacho hakitoweza kukubali sera za ccm na kuamini sera zao ndizo zinazoweza waletea wananchi maendeleo kwa haraka. Siku za nyuma kidogo chadema walijiaminisha ni wapinga ufisadi na taifa liliwajua hivyo. Alipoingia Rais JPM wakashindwa kuungana naye na vita ya ufisadi wakaanza kumpinga na kumtishia kuwa atashtakiwa mara anaonea watu hapo ndipo raia wakasanuka na kuona kumbe hawa hawapo kwa ajili yao na rasilimali za nchi.
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Nchi hii imekuwa na movement kadha wa kadha kadri zinavyojitokeza

Huko nyuma tumewahi kupigana vita vya Umasikini, Maradhi na Ujinga Kila mmoja kwa namna yake

Ikaja vita vya Demokrasia, tangu mwaka 1992 vinapigwana hadi sasa, vita hii imepanuliwa wigo na mahitaji ya katiba mpya

Mwaka 2000 tumepigana vita vya Ukimwi, hadi movement kupitia Sanaa, ndiyo wakati akina Ferouz na akina Profesa Jay wakawa sehemu ya askari

Hata hii vita vya kulinda mgongo ni movement ya kusaidia sehemu ya janga linalokumba vijana wengi

Vijana wetu wa kiume tuliowalea kuja kuingilia wanawake na kutuletea wajukuu, leo hii wamekubali kuingiliwa

Kama hamjaona hili ni tatizo, ngoja mzae watoto wenu wakiume, msikie wanainamishwa na kulilia nanii 🥲🙌
 
Ni ngori.

Wana mihemko kwenye mambo ya kijinga, lakini kwenye suala zima la mambo serious huwezi kuwaona hata chembe!

Yaani, huwa najiuliza sana hilo swali ujue 😂😂😂

Ama hakika hawa ni maiti 🫠🫠
Ni Maiti zinazotembea. 😂😂😂
 
Wewe nae ni takataka mmoja... We nae ni shoga au?. Project gani? Matako yako.
 
Lakini si dudubaya huyu huyu huwa anataka Lissu aachiwe na kwamba sio muhaini. Sasa CCM ikimpa coverage dudubaya si itaipa coverage pia kuachiwa kwa Lissu?

Hivi si serikali ya CCM imempiga fine dudubaya huoni ndio inafanya waonekane wao serikali ndio washabiki wa ushoga? Ambayo inakua mtazamo mbaya kwa wapiga kura?

Huu uchambuzi wako ni walakini sana, bora ungesema waTanzania wana tabia ya kurukia matukio ila sio kwamba CCM ndio wana engineer kila tukio.

Ni either unaikuza sana nguvu ya CCM kuliko uhalisia au kama kweli wanapanga basi hawana uwezo huo wa kutengeneza propaganda zenye quality.

CCM ndiye mratibu wa huyo Dudu baya. Ni vile tuu wengi mnashindwa kuona hilo.

Kwani kumtetea Lisu ndio kunamfanya mtu awe ccm au chadema?
Kila mtu anasema jambo fulani akiwa na agenda fulani.

Wewe unaweza kumtetea Lisu kwa sababu ya HAKI.
Mwingine anaweza kumtetea Lisu kwa Sababu ni CHADEMA mwenzake. Haki sio msingi.

Mwingine wa CCM anaweza kumtetea Lisu kwa sababu sio ya haki tuu bali anajikosha, anaagenda zingine anazodijua yeye
 
Na walivyo hamnazo wanamchangia. Wakidhani wanapambana na CCM au serikali kumbe ukute dudu naye anatumwa kupoteza watu maboya
 
CCM ndiye mratibu wa huyo Dudu baya. Ni vile tuu wengi mnashindwa kuona hilo.

Kwani kumtetea Lisu ndio kunamfanya mtu awe ccm au chadema?
Kila mtu anasema jambo fulani akiwa na agenda fulani.

Wewe unaweza kumtetea Lisu kwa sababu ya HAKI.
Mwingine anaweza kumtetea Lisu kwa Sababu ni CHADEMA mwenzake. Haki sio msingi.

Mwingine wa CCM anaweza kumtetea Lisu kwa sababu sio ya haki tuu bali anajikosha, anaagenda zingine anazodijua yeye
Yes agree. Spinning hizo. Hapo atapiga pesa za wajinga aendelee kulewa 24 hrs
 
Ndo kusema dudu ni project ya mbogamboga ???
Asingekuwa Project yao wangeshamdhibiti kitambo tu. By the way walishaaamua anyamazwe, ila wakaona kuna namna anaweza akatumika bila hata yeye kujua kuwa anatumika, by now wangeshamfungia Mirembe
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Bado Niko Kanda ya ziwa huku!

Aiseeh! Hii CCM kuiondoa madarakani ni kazi kwelikweli.

CCM haipo tuu midomoni. CCM ilipandwa kwenye akili za watu. Yaani asilimia 90% ya Watanzania wanaakili za kiccm CCM.

Wengi unaowaona wanapinga CCM wengi wao ni Njaa tuu. Wala hawapingani na uccm ambao utaukuta kwenye mambo mengine. Yaani unakuta mtu sio CCM kichama lakini kijamii ni CCM, kimichezo ni CCM, kiburudani ni CCM, kifamilia ni CCM, kiuchumi ni CCM. Hata namna anavyofikiria ni kiccm.

Sisi macho ya Bundi tunajua watu aina ya Dudubaya ni kina nani. Tunajua wapo kwaajili ipi.
Tunajua wanatumika na nani kwa misingi ipi.

Dudu baya kimbinu unaweza kumuita Ghost ball. Ambaye ni kama invisible Card ambaye anasukuma kete zinazoonekana bila maadui kufahamu.

Raha ya watu kama Dudu baya, ambao ni Ghost Ball au invisible kete huwachota mpaka upande wa pili na wao kujikuta wanachana na agenda ya msingi zilizopo.

Sisi Watibeli tunajua, nchi hii inamatatizo makubwa na makuu na hatarishi kuliko suala la ushoga. Anaousema Dudubaya.
Ukifanya utafiti utagundua kuwa katika familia kumi ni chache sana zenye mashoga. Chache sana. Kwanza kuna koo ambazo hakuna hata shoga mmoja wala hakuna mtu aliyewahi kuwa na kashfa ya ushoga. Na hizo koo zipo nyingi sana.

Msomaji unaweza kuungana na mimi katika ukoo wenu au mzunguko wako kuna shoga yoyote? Nina hakika asilimia 90% ya watu wakianza kuangalia watagundua koo zao hakuna mashoga.

Matatizo makubwa ndani ya nchi hii ambayo kila familia yanakabiliana nayo ni kama ifuatavyo;

a) Umaskini.
Kila ukoo na familia. Unapambana na umaskini. Asilimia 90% ya familia na koo za watanzania nchi ni maskini. Kumiliki pato la 5,000/= kwa siku kwa kila members wa familia ni kipengele. Kumaanisha ni maskini.
Mfano kama unafamilia ya watu watano, yaani Baba, mama na watoto wa tatu. Wastani wa kiasi kwa kila mtu hapo inatakiwa muwe na 5k yaani 25k ndilo pesa ya matumizi kwa siku

b) Ukosefu wa Haki.
Kila familia wanauzoefu kwa namna moja ama nyingine kudhulumiwa haki. Iwe ni haki ndani ya familia, kwenye jamii, kichumi na serikalini.

c) Uzinzi.
Hili ni janga ndani ya nchi. Madhara ya uzinzi kwenye nchi hii yamegusa kila familia, kila koo.
Hakuna ukoo hata mmoja ambao hauhangaiki na madhara ya Uzinzi.
Uzinzi ni chanzo cha single mothers.
Uzinzi ni chanzo cha watoto kukosa Baba na malezi ya wazazi.
Uzinzi ni chanzo cha magonjwa kama ukimwi.
Uzinzi ni chanzo cha migogoro ya kifamilia na kuvunjika kwa ndoa nyingi.
Uzinzi ni chanzo cha umaskini.
Uzinzi ni chanzo cha vifo vinavyosababishwa na Wivu wa mapenzi.
Uzinzi ni chanzo cha ukatili kama ubakaji. N.k.
Hakuna familia au ukoo ambao hauna matokeo ya Uzinzi.
Ila zipo koo maelfu elfu zisizo na ushoga.

Najaribu kusema Ushoga sio tishio kama ilivyo kwa changamoto zingine.

Dudu baya wengi hawatamuelewa kwani yeye ni ghost Ball, invisible kete ambaye kazi yake ni kusukuma agenda kinyume nyume.

Kwa wale ELITE wanajua nazungumzia nini.

Wenye upeo mdogo ni rahisi kutoelewa ishu kama hizi.

Mtu unamuuliza unapinga ushoga ni sawa. Je kwenye familia na ukoo wako mnachangamoto ya ushoga? Kuna shoga yeyote. Anajibu hakuna.

Unamuuliza, vipi kuna single mothers? Je kuna vijana wanaozalisha watoto wawatu hovyohovyo? Anajibu wapo wengi sana.
Unamwambia kwa nini asipambane na matatizo yanayomkabili kuliko kupambana na matatizo ya mbali? Anakuangalia.
Zaidi atakutukana kwamba wewe naye ni shoga.

Haya!

TaikonMaster
Kwa sasa Kahama, Shinyanga
Ushoga ni kama UKIMWI , ulianza na mtu mmoja ukaenea kwa wengi leo watu zaidi ya 36M wamezikwa na zaidi ya 40M wengine wanaishi na UKIMWI, TZ pia tulianza na mtu mmoja leo wapo zaidi ya 4M wanaishi na UKIMWI.

Ushoga ulianza na watu wawili huko Marekani badae wakaanza kudai haki zao , Wamarekani wakawapuuza wakasema hao ******* hawajielewi leo mashoga ni wengi kuliko idadi ya watu Tz.
Ushoga sio utamaduni wa Mwafrika, ni kweli kuwa unaweza kumtafuta shoga ukoo ukakosa ila kwenye jamii ukapata.
Leo ukienda Arusha mashoga ni wengi sio kwamba walipenda, wengine walinywesha pombe wakafirwa wakalawatiwa, leo kuna hawa watoto wanasoma bording school(s) wanalawatiana mtoto akizoea mchezo akikua anakua shoga.
Ushoga sio ugonjwa wa kurithi sio ugonjwa wa kuambukizwa ni tabia ya kuiga, kulazimishwa nk.
Ulishajiuliza wale Wasiojulikana (ambao ni maaskari, ni wanajeshi, ni maafisa usalama, walianzaje kuwajua kuwa huyu tukienda naye kuteka mtu kazi kubwa itakua kufira na kumlawiti mtu)
Is better watch your back
 
Mnajifananisha na Urusi tena? Wenzenu wakati wanapambana kufika hapa walipo leo waliacha kila kitu na kupambania walichonacho Leo.
Sasa hivi ndio wanapambana na kitu kingine km huo ushoga.

Sisi hapa bado sanaa, kuacha matatizo mbali mbali ya msingi na kuanza kupambania ushoga. Lol
Cocastic, nadhani tunatofautiana perspective. Aidha tupambane na maendeleo ya kiuchumi tuachana na matatizo ya kijamii, au twende na vyote? Wewe unaona ushoga sio jambo hata la kupoteza nalo muda, mimi naona jamii inapaswa kwenda na yote.

Huwezi pambana kujenga uchumi, ukaacha kujishughulisha na masuala ha kijamii, utajikuta siku umeendelea kiuchumi, halafu jamii iko hovyo kuweza kuhandle hayo maendeleo.

Yes, hatupaswi kukubali propaganda zitumie ushoga kuhadaa raia, huo utakua ni mtego ambao tunapaswa kuushtukia.

Mimi binafsi, mtu mzima kwa maamuzi yake mwenye akiamua kuwa shoga huyo ni yeye maana anajua nini afanyacho. Kwa vijana wadogo hawa under 18 walio mashuleni, majumbani au vyuoni, hawa ni under age, wanahitaji kuwa protected hadi wakiwa watu wazima waamue wenye kwa uhuru wao. Ila sio washenzi wanaendesha campain kwa vijana wadogo, eti jamii ikae kimya tuseme tuweke vipaumbele kwa maji, umeme na barabara. No tunaenda na vyote, ndio maana hata serikalini, ziko wizara zinazodeal na sectors mbalimbali, kwa sababu tunadeal na yote.
 
Nashangaa sana mtu unawaza ccm itoke madarakani. Kwa upinzani upi tulionao ambao unaweza kuongoza endapo ccm ikitoka? Ni kweli upinzani kuna wakati unakuwa na nguvu lakini ukiwapima hawawezi kuwa mbadala wa ccm kwa sababu wao sera zao hubadilika kutokana na kiongozi wa ccm aliopo madarakani. Kifupi ni kwamba upinzani umeshindwa kujijenga na ukaeleweka wenyewe kwa sera zao badala yake umekuwa ukipendwa endapo ccm inafanya vibaya. CCM ikifanya vizuri watu wanawasahau hapo ndipo wanaanza kuzusha uzushi kwa kiongozi aliopo madarakani na propaganda kibao.

Upinzani ulipaswa ujijenge na itikadi yao na watengeneze kizazi cha itikadi yao ambacho hakitoweza kukubali sera za ccm na kuamini sera zao ndizo zinazoweza waletea wananchi maendeleo kwa haraka. Siku za nyuma kidogo chadema walijiaminisha ni wapinga ufisadi na taifa liliwajua hivyo. Alipoingia Rais JPM wakashindwa kuungana naye na vita ya ufisadi wakaanza kumpinga na kumtishia kuwa atashtakiwa mara anaonea watu hapo ndipo raia wakasanuka na kuona kumbe hawa hawapo kwa ajili yao na rasilimali za nchi.
Wewe bro, 1950 kina Nyerere wangewaza kuwa hawana uzoefu wanahitaji wajifunze, hadi leo bado tungekuwa koloni. Hivi wewe unadhani upinzani ukishika nchi, wao wataongoza maeneo gani ambayo unadhani personel watakosekana? Upinzani unakosa watu 60 wa kuunda wizara? Tatizo CCM imejenga mfumo wa kijinga ambao unafanya watu waamini wanasiasa wanashika posts zote.

Duniani kote kwenye nchi zinazojielewa kidemokrasia, ambazo ziko huru kisiasa, Chama kama CHADEMA, Kingeattract watu wengi sana kujiunga nacho. Nazungumzia watu wakubwa kijamii. Kwa sababu ya hofu, watu wenye wadhifa wao kijamii wanakuwa waoga kuwa wazi. Lakini, upinzani una watu wengi sana. 2010 na 2015 watu wengi sana walijiunga na upinzani wazi, sababu hofu haikuwepo. Leo kuna watu wana support upinzani kimya kimya.

Halafu unaposema wajijenge, unaishi sayari gani wewe mzee, serikali inazuia Opposition isifanye kazi, ina hujumu Opposition halafu unasema ijijenge, unataka ijijenge vipi? Hivi CUF ilko wapi. NCCR iko wapi? Vilipoteaje? Katika mazingira ambayo dola inahujumu Opposition unategemea vikue vipi? Hapa tuipongeze sana CHADEMA. Wamehitahidi sana kufanya resistance.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Nchi hii imekuwa na movement kadha wa kadha kadri zinavyojitokeza

Huko nyuma tumewahi kupigana vita vya Umasikini, Maradhi na Ujinga Kila mmoja kwa namna yake

Ikaja vita vya Demokrasia, tangu mwaka 1992 vinapigwana hadi sasa, vita hii imepanuliwa wigo na mahitaji ya katiba mpya

Mwaka 2000 tumepigana vita vya Ukimwi, hadi movement kupitia Sanaa, ndiyo wakati akina Ferouz na akina Profesa Jay wakawa sehemu ya askari

Hata hii vita vya kulinda mgongo ni movement ya kusaidia sehemu ya janga linalokumba vijana wengi

Vijana wetu wa kiume tuliowalea kuja kuingilia wanawake na kutuletea wajukuu, leo hii wamekubali kuingiliwa

Kama hamjaona hili ni tatizo, ngoja mzae watoto wenu wakiume, msikie wanainamishwa na kulilia nanii 🥲🙌
kwenye hii movement, kuna mbinu zozote za kuwakabili waingiliaji ?
vipi uthibiti wa movies/series kutoka magharibi/asia ?
public inavojiconduct kupita maeneo ya masoko/stendi/vijiwe ni kawaida sana watu wakikosana kukashifiana hivyo, mashule ya yaangaliwa? ,

mapambano yanalenga uhalisia?
 
Wewe bro, 1950 kina Nyerere wangewaza kuwa hawana uzoefu wanahitaji wajifunze, hadi leo bado tungekuwa koloni. Hivi wewe unadhani upinzani ukishika nchi, wao wataongoza maeneo gani ambayo unadhani personel watakosekana? Upinzani unakosa watu 60 wa kuunda wizara? Tatizo CCM imejenga mfumo wa kijinga ambao unafanya watu waamini wanasiasa wanashika posts zote.

Duniani kote kwenye nchi zinazojielewa kidemokrasia, ambazo ziko huru kisiasa, Chama kama CHADEMA, Kingeattract watu wengi sana kujiunga nacho. Nazungumzia watu wakubwa kijamii. Kwa sababu ya hofu, watu wenye wadhifa wao kijamii wanakuwa waoga kuwa wazi. Lakini, upinzani una watu wengi sana. 2010 na 2015 watu wengi sana walijiunga na upinzani wazi, sababu hofu haikuwepo. Leo kuna watu wana support upinzani kimya kimya.

Halafu unaposema wajijenge, unaishi sayari gani wewe mzee, serikali inazuia Opposition isifanye kazi, ina hujumu Opposition halafu unasema ijijenge, unataka ijijenge vipi? Hivi CUF ilko wapi. NCCR iko wapi? Vilipoteaje? Katika mazingira ambayo dola inahujumu Opposition unategemea vikue vipi? Hapa tuipongeze sana CHADEMA. Wamehitahidi sana kufanya resistance.
hivi CUF huku bara haijageuka ACT kama kule zenji?
 
Cocastic, nadhani tunatofautiana perspective. Aidha tupambane na maendeleo ya kiuchumi tuachana na matatizo ya kijamii, au twende na vyote? Wewe unaona ushoga sio jambo hata la kupoteza nalo muda, mimi naona jamii inapaswa kwenda na yote.

Huwezi pambana kujenga uchumi, ukaacha kujishughulisha na masuala ha kijamii, utajikuta siku umeendelea kiuchumi, halafu jamii iko hovyo kuweza kuhandle hayo maendeleo.

Yes, hatupaswi kukubali propaganda zitumie ushoga kuhadaa raia, huo utakua ni mtego ambao tunapaswa kuushtukia.

Mimi binafsi, mtu mzima kwa maamuzi yake mwenye akiamua kuwa shoga huyo ni yeye maana anajua nini afanyacho. Kwa vijana wadogo hawa under 18 walio mashuleni, majumbani au vyuoni, hawa ni under age, wanahitaji kuwa protected hadi wakiwa watu wazima waamue wenye kwa uhuru wao. Ila sio washenzi wanaendesha campain kwa vijana wadogo, eti jamii ikae kimya tuseme tuweke vipaumbele kwa maji, umeme na barabara. No tunaenda na vyote, ndio maana hata serikalini, ziko wizara zinazodeal na sectors mbalimbali, kwa sababu tunadeal na yote.
Para ya mwisho uko sahihi, hata mie naunga mkono. Ila ninachokataa ni kwa watu wazima ambao wao binafsi kwa utashi wao wakaamua kuwa hivyo halafu wanatokea watu wanapinga au kuzuia, hapo hapana sitakubali, huko ni kuingilia haki za faragha ya mtu. Na haikubaliki.
 
Back
Top Bottom