CCM hawakurupuki kwenye mambo yao na mtu akizingua anafinywa ndani huwezi kuta wanaparuana nje. Hapa ndio CHADEMA mnafeli

Ni kwasababu wana dola.
Mamlaka na nguvu za dola vinatumika kutatua migogoro ya chama. Ni kawaida kugawanya jimbo mara 2, kumaliza mivutano ya vigogo, kuteua mtu kshika wadhifa flani akitokea sehemu flan kwenye kwenye mivutano.
 
Ccm unaiona ina nguvu hivyo maana imejificha kwenye dola. Subiri ccm iwe nje ya madaraka ndio ujue ubora wake.
Hoja zako ziko kiushabiki wa kisiasa, yaani una upofu wa itikadi. Unataka kuonyesha ukweli ni tatizo badala ya jamii yenye tatizo la kukubali ukweli. Hiyo ccm unayoona ina ubora huo, ukweli haina ubora wowote zaidi ya kujificha kwenye kichaka cha dola. Inshort ww ni muumini wa siasa za kihuni na nidhamu za hofu.
 
Upeleke tuhuma za rushwa kwenye vikao vya wanaoogelea kwenye hiyo rushwa?
 
Kama pesa za Sabodo zilikuwa chafu sio kosa la cdm, bali ni la taasisi za kimamlaka.
 
Kwani hao CHADEMA ni mawe hawawezi kujiongeza na kujifunza? Hata ukiweka dola pembeni, CCM wanajua jinsi ya kupangilia their 'shit'
Thubutu, waweke nje ya dola hao ccm ndio utajua ni kwa kiwango gani ni kundi la washenzi, usiwape sifa wasiyokuwa nayo. Chama cha watu wenye nidhamu ya woga na unafiki wanatoa wapi sifa hiyo?
 
Mkuu mambo na taratibu zinazofanyika ndani ya chama tawala sio mtaala wa kufuatwa na vyama vya upinzani.

Mbele ya sheria vyote ni vyama vya siasa.
 
CCM DAIMA
 
Dogo unatetea na kuisifia organized crime wanayoitumia ccm kumaliza nchi kweli?

Kwa vile wanalishana Yamini na kudhibitiana kulinda ufisadi
Wewe ndo unawasifia

Nchi imejaa wajinga wengi
 
Usicho kijua kwa kushindwa kufanya Tafakari kwa ni kwamba ,Kinacho leta ukimya wa wana ccm ndani ya CCM ni hofu ya kupotezwa kwakuwa CCM imejiunganisha na serikali, hivyo watu wana madukuduku yao mengi sana mioyoni lakini wanaogopa kulipuka kwa sababu moja tu kuu, mwenyekiti wa chama ndiye Rais na amiri jeshi mkuu , hivyo kuna visa vingine vya kichama vinashughulikiwa kiserikali, wengi wamepotezwa na kutulizwa kimya kimya kiserikali wakati ni maswala ya chama.
 
Kwani hao CHADEMA ni mawe hawawezi kujiongeza na kujifunza? Hata ukiweka dola pembeni, CCM wanajua jinsi ya kupangilia their 'shit'
Tuchukulie mfano ccm ikaondoka madarakani na upinzani ndio ukashika Dola unadhani icho unachokiongea kitaendelea kuwepo ndani ya ccm licha ya ukongwe wake? Tunajua watu wanajiegesha ccm ili kulinda maslai yao kwakuwa ndio chama kilichoshika Dola kwa sasa ivyo ata upinzani ukiingia madarakani watu wale wale wataanza kuhamia kwenye chama kilichopo madarakani kwakuwa wanajua ccm aitokuwa na meno Tena ya kuwakandamiza kwa namna yoyote Ile,,siku zote wanasiasa uwa wanacheza na upepo unakoelekea ili kulinda maslai yao na unaweza kushangaa ccm ikapotea kabisa kwenye siasa za ushindani maana mifano ipo mingi ya hivi vyama vikongwe vilivyotawala nchi kwa mda mrefu pindi vinapoondolewa madarakani!
 
Haya mambo unaon ni saw , mar zote wajiman Uhuru
 
Inawezekana ikawa ndio m binu yao kubwa inayowasaidia au lah (nimesema yote hayo kwenye uzi kama umepitia vizuri), na hapo ndio CHADEMA inabidi ipate njia/mfumo wao utakaowasaidia wao kuhakikisha wanajipanga lakini pia wanasolve mambo yao in a civilized way, sio kama wamekatwa vichwa
 
Walichokosea wanachama wa chadema nikuleta mambo yao kwenye mitandao na vyombo vya habari.Matokeo yake wakajikuta wanaropoka ujinga unaowavuruga wao wenyewe.Walishindwa kujua sio kila kitu nichakuweka mitandaoni bila kuchuja.Na wengine sifa za mitandaoni zinawadanganya wanajiona ni wakubwaa au wamuhimu bila kujua watanzania ni watu wa matukio na wao siasa niushabiki kama wa simba na yanga hawajali hoja wala mantiki..ukikosa platfom yakusemea mambo yako baada ya miezi 3 umeshasahaulika.Kwahiyo wajifunze kukomaa kifikra.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…