CCM imechoka, upinzani umetepeta! Hii ni turufu kwa chama nitachoasisi ili kushika dola 2035!

Mikopo Consultant

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2024
Posts
2,375
Reaction score
4,784
Mwaka mmoja na nusu umepita baada ya kuandika uzi wangu huu-- ' Hekaya za George Soros na Utabiri wa Anguko la CCM,' kwenye jukwaa hili adhimu! Mwenendo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) haujaboreka, bali umeendelea kuzorota na kufifia! Hii inafanya ile 'narrative' ya 'CCM haijabakisha maisha marefu ili ife,' ambayo wana-medani wa mambo ya siasa za nchi hii, wa hapa jamvini tuliweza kuitengeneza, iendelee kuishi. Mipasuko mikubwa na midogo na makundi ambayo haipungui bali inazidi kuongezeka, ni donda ndugu kwa taasisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo imejeuka kuwa 'shamba la bibi, kila mtu anajichumia' na 'jamvi la sokoni, kila mtu anakanyaga'! Ukishakuwa na taasisi ya namna hiyo, kuchakaa na kuchuja hakukwepeki--na ndicho kinachoitokea CCM kwa sasa!

Matokeo ya kuchuja kwa CCM yameonekana kwenye masuala ya Octoba 29, 2025, ambayo lilitabiriwa na wengi hata kabla, ikiwamo mimi, na wengineo wengi wenye maono na udadisi wa mambo na mwenendo wa kisiasa na matukio ya nchi hii, kwa kupitia nyuzi kedekede hapa jamvini.

Kitu ambacho wengi hatukukiona kama kingetokea, ni kutepeta kwa haraka kwa upinzani mkuu -- nikimaanisha, 'kutepeta kwa CHADEMA,' ambacho ni ukweli usiopingika ndo 'defacto' main opposition party in Tanzania. Sihitaji kuzungumza kwa kina ni kwanini nasema CHADEMA imetepeta, ila wanaofuatilia mwenendo wa siasa za nchi hii, watakuwa wanajua moja kwa moja kwamba: kuna mambo ya msingi ambayo yamejitokeza ndani ya hiki chama kwa miezi 18 iliyopita, na yamefifisha kabisa na kuporomosha kwa kasi, ukubwa wa CHADEMA kama chama kinachotakiwa kuaminika na watanzania wengi, mimi nikiwemo. Kwa dhati kabisa, hii CHADEMA ya sasa, ukimuondoa Tundu Lissu ambaye hana chembe ya uchafu mikononi kwake, na ni mtu pekee, raia yeyote wa nchi hii anaweza kumuamini, hao viongozi wengine wote wa CHADEMA waliobakia, hawafai, makanjanja, vigeugeu, na hawaaminiki, hata ikitokea wakafa, wakazaliwa, wakafa tena, wakazaliwa!

Kwa hiyo kusema CCM itoke madarakani halafu eti ikabidhi madaraka kwa the likes of Lema, Heche, Mbowe, Msigwa !! Hiyo itakuwa ni kutoa fedha mkono wa kushoto na kuhamishia mkono wa kulia. Hakuna chochote cha kutegemewa kwa hii CHADEMA ya sasa!

HII INA MAANA YA KWAMBA: Kwa hali ya sasa ya kisiasa ya nchi hii, kuna ombwe kubwa la mustakali wa kiuongozi ambalo limetengenezwa na kudhoofika kwa CCM na kutepeta kwa vyama vya upinzani. Na kwasababu Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, ambayo mabadiliko pekee yatatokana na chama cha kisiasa kitachoshika dola ili kibadili sheria na kuleta utamaduni utaoondoa 'systems failures' aliyezisema mwanajukwaa Aminata B Ruhinda Ntare kwenye uzi wake huu wa 'Broken Systems/ Broken Lives.'

Hivyo basi, ombwe hili lililopo, kwangu ni turufu ya kuliziba kwa kushiriki kuasisi chama kipya cha kisiasa ambacho kitabeba matumaini ya watanzania wa kesho--watanzania wa Dira 2050 (Msiseme eti Dira 2050 ni mali ya CCM, mjue tu kwamba chama kitachoshika dola kitaanza kuongoza pale CCM ilipoishia, na sio eti kubomoa na kuanza upya!)

****

IPO HATARI KUBWA MBELENI KAMA WATANZANIA WATAKOSA UWEPO WA CHAMA KIPYA CHA UPINZANI CHENYE NGUVU
Kwa sababu CCM imechoka na haikubaliki na upinzani umetepeta! Baada ya miaka 10 ijayo (yaani 2035) ambapo CCM itatoka madarakani rasmi, kutahitajika kuwe na chama cha upinzani imara, kinachokubalika na wengi ili kipokee madaraka kutoka kwa CCM, ili nchi iendelee kuwa na muunganiko na amani ya kudumu!

Endapo hakutakuwa na mageuzi ambayo yataleta chama kipya mbadala cha upinzani -- either kutokana na tabia ya CCM kuendelea kuminya demokrasia, au kwa bahati mbaya ikiwa watanzania (yaani sisi), tutakosa maono ya kuanzisha chama/vyama imara na vya kuaminika na watanzania (sio hivi vya sasa), basi hatari yake inaweza kuwa kubwa kwenye mustakabali na amani ya nchi hii.

KWANINI NASEMA HIVO?
Mwaka 2035, Tanzania itakuwa na idadi ya watu wapatao milioni 90 -- ambapo vijana wa umri wa miaka 18 mpaka 35 watakuwa kati ya milioni 28 mpaka 30. Na kutokana na uraibu wa kukataa ndoa na u-single mother, takribani asilimia kama 65 ya vijana hawa watakuwa hawapo kwenye familia, na watakuwa ni vijana ambao kuna uwezekano mkubwa wakawa jobless kutokana na uhalisia na mwenendo wa uchumi wa nchi yetu ambao unakuwa vizuri at macro level lakini hautengenezi fursa za ustawi kwa mtu mmoja mmoja (kuna low trickle-down-effect kutoka kwenye macro kwenda kwenye micro). Na pia, kutokana na deni letu la taifa kuwa kubwa na kuendelea kukua kwa kasi, matumizi ya serikali yanayokuwa kwa kasi, kunahatari ya mamlaka za mapato za nchi hii kuendeleza mbinyo kwa raia wake kupitia ongezeko kubwa la kodi kwa raia, kitu kitachoendelea kuongeza pilipili kwenye kidonda cha taifa la watanzania. Haya yote yatapelekea kuwe na ‘grievances’ kubwa ndani ya raia wa-kitanzania -- kubwa maradufu ya ile ya kuelekea Octoba 29, 2025.

Njia pekee ya kupoooza grievances ni kupitia sanduku la kura, ambapo watu watataka kubadili upepo wa kisiasa kama mategemeo ya kuziponya grievances zao. Sasa endapo kutakuwa na uminywaji wa demokrasia ya watu kuwa huru kushiriki uchaguzi wa halali kwenye boksi la kura kama ilivyotokea Octoba 29, 2025, au kama raia watakosa chama wanachoamini kipo kwa maslahi yao; basi inaweza kupelekea kujirudia kwa yaliyotokea Octoba 29, 2025--kwa watu kutafuta namna wanayohisi inafaa ili kuponya grievances zilizopo mioyoni mwao.

****

ILI KULIPONYA TAIFA NA HATARI KUBWA ILIYOPO MBELENI: mimi MC nimeamua kuwajibika kwa kuanzisha mchakato wa kuasisi chama kipya, kikubwa, cha kisiasa, kitachokubalika na watanzania, kisicho na makandokando kama ya vyama vilivyopo vya upinzani-CCM, ambacho kitakuwa na sura ya kitaifa, na kikiwa na lengo kubwa mahsusi la kupokea kijiti cha kushika dola kutoka kwa Chama cha Mapinduzi ifikapo 2035, ambapo ndio itakuwa mwisho kwa CCM kuwa madarakani kwenye taifa hili la Tanzania.

Najua uzi huu utasahaulika mapema ndani ya wanajamii, lakini kwa ambao mtajaliwa kumbukumbu, ifikapo mwaka 2028, chama hiki kitachobeba matumaini ya watanzania, kitaasisiwa rasmi.

Ee Mwenyezi Mungu, Tusaidie!

MC
​
 
Mwaka mmoja na nusu umepita baada ya kuandika uzi wangu huu-- ' Hekaya za George Soros na Utabiri wa Anguko la CCM,' kwenye jukwaa hili adhimu! Mwenendo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) haujaboreka, bali umeendelea kuzorota na kufifia! Hii inafanya ile 'narrative' ya 'CCM haijabakisha maisha marefu ili ife,' ambayo wana-medani wa mambo ya siasa za nchi hii, wa hapa jamvini tuliweza kuitengeneza. Mipasuko mikubwa na midogo na makundi ambayo haipungui bali inazidi kuongezeka, ni donda ndugu kwa taasisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo imejeuka kuwa 'shamba la bibi, kila mtu anajichumia' na 'jamvi la sokoni, kila mtu anakanyaga'! Ukishakuwa na taasisi ya namna hiyo, kuchakaa na kuchuja hakukwepeki--na ndicho kinachoitokea CCM kwa sasa!

Matokeo ya kuchuja kwa CCM yameonekana kwenye masuala ya Octoba 29, 2025, ambayo lilitabiriwa na wengi hata kabla, ikiwamo mimi, na wengineo wengi wenye maono na udadisi wa mambo na mwenendo wa kisiasa na matukio ua nchi hii, kwa kupitia nyuzi kedekede hapa jamvini.

Kitu ambacho wengi hatukukiona kama kingetokea, ni kutepeta kwa haraka kwa upinzani mkuu -- nikimaanisha, 'kutepeta kwa CHADEMA,' ambacho ni ukweli usiopingika ndo 'defacto' main opposition party in Tanzania. Sihitaji kuzungumza kwa kina ni kwanini nasema CHADEMA imetepeta, ila wanaofuatilia mwenendo wa siasa za nchi hii, watakuwa wanajua moja kwa moja kwamba: kuna mambo ya msingi ambayo yamejitokeza ndani ya hiki chama kwa miezi 18 iliyopita, na yamefifisha kabisa na kuporomosha kwa kasi, ukubwa wa CHADEMA kama chama kinachotakiwa kuaminika na watanzania wengi, mimi nikiwemo. Kwa dhati kabisa, hii CHADEMA ya sasa, ukimuondoa Tundu Lissu ambaye hana chembe ya uchafu mikononi kwake, na ni mtu pekee, raia yeyote wa nchi hii anaweza kumuamini, hao viongozi wengine wote wa CHADEMA waliobakia, hawafai, makanjanja, vigeugeu, na hawaaminiki, hata ikitokea wakafa, wakazaliwa, wakafa tena, wakazaliwa!

Kwa hiyo kusema CCM itoke madarakani halafu eti ikabidhi madaraka kwa the likes of Lema, Heche, Mbowe, Msigwa !! Hiyo itakuwa ni kutoa fedha mkono wa kushoto na kuhamishia mkono wa kulia. Hakuna chochote cha kutegemewa kwa hii CHADEMA ya sasa!

HII INA MAANA YA KWAMBA: Kwa hali ya sasa ya nchi hii, kuna ombwe la mustakali wa kiuongozi ambalo limetengenezwa na kudhoofika kwa CCM na kutepeta kwa vyama vya upinzani. Na kwasababu Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, ambayo mabadiliko pekee yatatokana na chama cha kisiasa kitachoshika dola ili kibadili sheria na kuleta utamaduni utaoondoa 'systems failures' aliyezisema mwanajukwaa Aminata B Ruhinda Ntare kwenye uzi wake huu wa 'Broken Systems/ Broken Lives.'

Hivyo basi, ombwe hili lililopo, kwangu ni turufu ya kuliziba kwa kushiriki kuasisi chama kipya cha kisiasa ambacho kitabeba matumaini ya watanzania wa kesho--watanzania wa Dira 2050 (Msiseme eti Dira 2050 ni mali ya CCM, mjue tu kwamba chama kitachoshika dola kitaanza kuongoza pale CCM ilipoishia, na sio eti kubomoa na kuanza upya!)

****

IPO HATARI KUBWA MBELENI KAMA WATANZANIA WATAKOSA UWEPO WA CHAMA KIPYA CHA UPINZANI CHENYE NGUVU
Kwa sababu CCM imechoka na haikubaliki na upinzani umetepeta! Baada ya miaka 10 ijayo (yaani 2035) ambapo CCM itatoka madarakani rasmi, kutahitajika kuwe na chama cha upinzani imara, kinachokubalika na wengi ili kipokee madaraka kutoka kwa CCM, ili nchi iendelee kuwa na muunganiko na amani ya kudumu!

Endapo hakutakuwa na mageuzi ambayo yataleta chama kipya mbadala cha upinzani -- either kutokana na tabia ya CCM kuendelea kuminya demokrasia, au kwa bahati mbaya ikiwa watanzania (yaani sisi), tutakosa maono ya kuanzisha chama/vyama imara na vya kuaminika na watanzania (sio hivi vya sasa), basi hatari yake inaweza kuwa kubwa kwenye mustakabali na amani ya nchi hii.

KWANINI NASEMA HIVO?
Mwaka 2035, Tanzania itakuwa na idadi ya watu wapatao milioni 90 -- ambapo vijana wa umri wa miaka 18 mpaka 35 watakuwa kati ya milioni 28 mpaka 30. Na kutokana na uraibu wa kukataa ndoa na u-single mother, takribani asilimia kama 65 ya vijana hawa watakuwa hawapo kwenye familia, na watakuwa ni vijana ambao kuna uwezekano mkubwa wakawa jobless kutokana na uhalisia na mwenendo wa uchumi wa nchi yetu ambao unakuwa vizuri at macro level lakini hautengenezi fursa za ustawi kwa mtu mmoja mmoja (kuna low trickle-down-effect kutoka kwenye macro kwenda kwenye micro). Na pia, kutokana na deni letu la taifa kuwa kubwa na kuendelea kukua kwa kasi, matumizi ya serikali yanayokuwa kwa kasi, kunahatari ya mamlaka za mapato za nchi hii kuendeleza mbinyo kwa raia wake kupitia ongezeko kubwa la kodi kwa raia, kitu kitachoendelea kuongeza pilipili kwenye kidonda cha taifa la watanzania. Haya yote yatapelekea kuwe na ‘grievances’ kubwa ndani ya raia wa-kitanzania -- kubwa maradufu ya ile ya kuelekea Octoba 29, 2025.

Njia pekee ya kupoooza grievances ni kupitia sanduku la kura, ambapo watu watataka kubadili upepo wa kisiasa kama mategemeo ya kuziponya grievances zao. Sasa endapo kutakuwa na uminywaji wa demokrasia ya watu kuwa huru kushiriki uchaguzi wa halali kwenye boksi la kura kama ilivyotokea Octoba 29, 2025, au kama raia watakosa chama wanachoamini kipo kwa maslahi yao; basi inaweza kupelekea kujirudia kwa yaliyotokea Octoba 29, 2025--kwa watu kutafuta namna wanayohisi inafaa ili kuponya grievances zilizopo mioyoni mwao.

****

ILI KULIPONYA TAIFA NA HATARI KUBWA ILIYOPO MBELENI: mimi MC nimeamua kuwajibika kwa kuanzisha mchakato wa kuasisi chama kipya, kikubwa, cha kisiasa, kitachokubalika na watanzania, kisicho na makandokando kama ya vyama vilivyopo vya upinzani-CCM, ambacho kitakuwa na sura ya kitaifa, na kikiwa na lengo kubwa mahsusi la kupokea kijiti cha kushika dola kutoka kwa Chama cha Mapinduzi ifikapo 2035, ambapo ndio itakuwa mwisho kwa CCM kuwa madarakani kwenye taifa hili la Tanzania.

Najua uzi huu utasahaulika mapema ndani ya wanajamii, lakini kwa ambao mtajaliwa kumbukumbu, ifikapo mwaka 2028, chama hiki kitachobeba matumaini ya watanzania, kitaasisiwa rasmi.

Ee Mwenyezi Mungu, Tusaidie!

MC
​

Tatizo sasa huu mtandao umejaa wafuasi wa chadema wa leo hakuna hata mwenye seli mbili za ubongo zinazofanya kazi pamoja aidha kuweza kusoma hii mada yako yote au kusoma na kuelewa ulichoandika.
Ndio maana tunasema chadema ilikuwa zamani yenye ushawishi kwa wasomi pia hata kama hajihusishi na siasa
Hii ya sasa inaenda kujifia na hata kama siku moja CCM itatolewa basi sio na hawa vilaza wa chadema ya leo
 
Ni ukweli mchungu. CHADEMA ya enzi zile miaka 10 au 15 iliyopita, is no more. Kwa tafsiri yangu, ile CHADEMA ya ambayo hata wasomi walikuwa wanaipa support kimya kimya, haipo tena, na haiwezi kurejea. Japo najua kwenye hili matusi yatakuwa mengi. Mimi binafsi nachukizwa na hili, lakini ndo ukweli ulivyo. Kunahitajika mrengo mpya ambao sio CHADEMA tena.
 
hawa chadema wa sasa wana utapiamlo wa elimu, wakiona makala ndefu wanaogopa kuingia, wao wanataka taarifa fupifupi kama za kiongozi wao mange zisizo na kichwa wala miguu
 
Back
Top Bottom