CCM imegawanyika; CHADEMA wajifunze kutoka Zambia. Mbowe ampishe Tundu Lissu Uenyekiti

CCM imegawanyika; CHADEMA wajifunze kutoka Zambia. Mbowe ampishe Tundu Lissu Uenyekiti

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038
Mgombea wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema anaongoza katika matokeo ya kura za awali katika uchaguzi mkuu.

Hakainde alionyesha kuongoza siku ya jana huku chama chake cha UPND kikikusanya kura katika majimbo mengi nchini humo.

Raisi alieko madarakani Edgar Lungu mwenye umri wa miaka 64 tayari amelalamika kwamba uchaguzi huo hauko huru na wa haki.

Mgombea Hichilema amewaambia wazambia kuwa wapuuze kauli hizo za raisi Lungu na kwamba huu ndo wakati mwafaka kwa wazambia kuungana na kuimarisha umoja.

Lakini moja ya sababu kubwa ya kura nyingi kwenda kwa bwana Hichilema ni ukosefu wa ajira nchini humo miongoni mwa vijana ambao ndo nguvukazi ambayo serikali imeshindwa kuitumia katika kuijenga Zambia kiuchumi.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka tume ya Uchaguzi ya Zambia vijana wengi walojiandikisha kupira kura wana umri wa miaka 34 kwenda chini.

Katika uchaguzi wa mwaka 2016 bwana Hichilema alishindwa na hata baadae kutumiwa vikosi vya usalama nyumbani kwake baada ya kutangaza kuwa matokeo ya uchaguzi ule yalichakachuliwa.

Safari hii wapiga kura wamejitokeza kwa wingi kupita maelezo na wote wameazimia kumpa kura bwana Hichilema mwenye umri wa miaka 59.

Hichilema anajielezea katika video zake Youtube kuwa ni mtoto wa maskini, na amekwenda shule bila viatu hadi kufikia chuo kikuu.

Kitaaluma bwana Hichilema ni mhasibu na alikuwa afisa mtendaji mkuu katika kampuni yake mwenyewe ya uhasibu kabla ya kufikria kuingia kwenye ulingo wa siasa.

Sera za bwana Hichilema ni kutaka kuimarisha uchumi wa nchi hiyo na kuimarisha soko la ajira ambalo limeathiri vijana wengi.

Matatizo yanayoikabili Zambia yanafanana kwa kiasi kikubwa na matatizo ya Tanzania, vitendo vya rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya fedha, maendeleo duni mijini, mazingira mabovu ya biashara na uwekezaji, deni la taifa na mengine lukuki.

CCM ndicho chama kinachoongoza serikali na mpaka sasa kila ishara iko wazi kuwa CCM imegawanyika katika makundi zaidi ya moja.

Miaka mitano imepita tumesikia kuwa CCM iligawanyika kati ya kundi linalojiita CCM asili na CCM mpya, na sasa tunasikia kauli tofautitofauti na zinazokinzana kutoka kwa wanachama waandamizi wa chama hicho.

Pia hata gazeti maarufu linalomilikiwa na chama hicho gazeti la UHURU nalo limetumika katika malumbano yanoendela ndani ya chama hicho na kwa kuandika vichwa vya habari kumhusu mwenyekiti wake na kuzusha fataki ndani ya chama hicho.

Kama si umakini wa wazee wa chama hichi kikongwe kuingilia kati na kumtuma katibu mkuu wake bwana Daniel Songoro kwenda kuzawazisha mambo, basi hali ingeendelea kuwa tete hadi leo hii.

Songoro bado hajajibu masuali makuu mawili kwanza, je CCM imegawanyika au la, na pili je CCM ina msimamo upi wa pamoja kama chama kuhusiana na chanjo ya UVUKO-19 kwa,mba ni lazima watanzania wachanjwe au chanjo hiyo ni hiari?

Mgawanyiko huu ndo ilikuwa nafasi ya pekee kwa chama kikuu cha upinzani cha Chadema kujitengenezea mazingira mazuri ya ushindi katika uchaguzi ujao wa 2025.

Badala yake si viongozi wake wakuu katibu mkuu, wala uenezi ambae amejitokeza kuonyesha angalau Chadema imeanza kujenga stratejia ya ushindi.

Chadema kinahitaji kujindaa kwelikweli na kama kweli chama hiki kina dhamira ya kweli ya kushika dola, basi kina wajibu wa kuachana na siasa za matukio na kujikita katika kujenga hoja zenye tija ili kujijengea imani kwa wapiga kura.

Suala la mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kuwa na kesi ya ugaidi inayoendelea mahakamani lisiwe sababu ya Chadema kama chama ambacho kina miaka 29 sasa kwenye ulingo wa siasa za vyama vingi kukosa mwelelekeo na kuonekana hakina mikakati.

Huu ndo ulikuwa wakati wa makamu mwenyekiti Tundu Lissu kuwa mastari wa mbele kukiongoza chama hicho na pengine kupewa nafasi ya uenyekiti wa chama hicho ili akiandane uzuri chama kwa uchaguzi ujao.

Ni maoni yangu binafsi kuwa Tundu Lissu kwa sasa amejifunza kuwa mwanasiasa badala ya mwanaharakati na kwa uwezo wake, ujasiri wake na kauli zake ambazo atakuwa sasa amefahamu namna ya kuzipanga uzuri, anafaa kabisa kuwa mwenyekiti wa Chadema.

Ni wakti sasa kwa Tundu Lissu kurudi nyumbani Tanzania na kuanza kazi ambayo nadhani bado hajaimaliza.

Vyombo vyote vya ulinzi na usalama havina budi sasa kujifunza kutoka Zambia na Malawi kuwa kuna wakati wananchi wanaamua kuwa chama kilichopo madarakani kimefikia tamati na wanataka chama mbadala.

Serikali ina wajibu wa kuhakikisha maisha ya Tundu Lissu yanalindwa na wale wote wasio na nia njema kwake na anasimama kwa uhuru katika jukwaa la kisiasa.

Tundu Lissu akiwa mwenyekiti wa Chadema taifa atakipanga chama atakavyoona yeye inafaa, kuteua timu yake ambayo ina watu makini na kutengeneza sera na ilani mpya ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa 2025.

Kama raisi wa Malawi Chikwera na mgombea wa sasa wa uraisi Zambia bwana Hakainde Hichilema waliweza, sioni tatizo Chadema washindwe uchaguzi wa 2025.

Mgombea wa chama cha upinzani akipata kura za kutosha na watu wakijitokeza kwa wingi kama walivyofanya Zambia kiasi cha tume ya Uchaguzi ya Zambia kutia akili kuwa Hichilema anashinda kwa kura za kutosha.
 
Kwa Tanzania bado saaanaah, hata vijana wenyewe Ni wanyonge, ndo maana wanaitwa wanyonge, maana yake magoigoi au legelege'

Kwa aina ya mfumo wa utawala unaotumia mabavu, vitisho, vipigo, kamatakama na kutokomezwa kabisa usijulikane uliko, unaweza elewa Ni kwa Nini vijana hawana ajira lakin Tanzania ikawa Ni nchi ya kijani kwenye uchaguzi 2020!

#Tanzania itaokolewa na wananchi wenyewe, waliochoshwa na utawala wa mabavu na ukandamizwaji, kinyume na hapo kukiendelea kuwepo vijana rojorojo, laini laini, goigoi, wanaoitwa wanyonge wanachekelea tutasubir saanaah!
 
Sera za kijamaa ndio zimetufikisha hapa tulipo mkuu

Sifa ya sera hii n uoga na unafiki na hiz sifa kati ya watanzania 10 basi 8 kati yao wanavuashiria vya tabia hizi

La pili ubinafsi uliopo miongoni mwa viongozi wetu mfano kijana wakike anapambania chama kwa nguvu zote lakn mwisho wa siku hapat chochote tumejionea lundo la wabunge wa viti maalum wakipewa ambao hawana sifa hizo ambazo wanatakiwa kuwa nazo

La mwisho TUME HURU YA UCHAGUZI hapa ndipo maslah ya CCM yalipo watacheza kote lakn tume hawawez kubali ibadirishwe MUUNDO WAKE

NINI KIFANYIKE

Vijana ndio wanaoleta mabadiriko katika nchi tuwe tayari kuvuja damu kwa ajili ya vizazi vijavyo tusijiangalie sisi n muda wa kupambana hadi tone la mwisho la damu ili tupate mabadiriko tunayohitaji TUSIOGOPE KUKAMATWA tuweke makongano ambayo yataelezea Hali halisi nchini ilivyo ili kila mtu atambue wajibu wake
 
... Mbowe alishatangaza rasmi kwamba, kwa mapenzi ya Mungu, mwisho wake kama Mwenyekiti Chadema ni 2023. Baada yake chama kitaamua nani wa kumrithi.
 
Hayo yote uliyosema yana maana ila hata huyo mpinzani ameshindwa kwa kuwa watu wametoka front na wengine wamekufa.
Tanzania sijui tuna nini labda kwa kuwa watu wanashiba hawaoni umuhimu was haya mambo.
 
HAWA jamaa mambo yote mema hawayapendi Waliungana wakati wa Ukawa muda kidogo tu wakavurugana huku wakijua kabisa kwamba bila kuungana wataendelea kuwa wapinzani milele.

Walikomalia sakata la katiba wakapewa fursa zikatumika Bilioni 200+ walipoona inakaribia kupita wakaisusa Leo wanataka tuanze upya ILI wapige NYINGINE alafu wasuse.!
 
Ukikuta mbweha anamshauri mwanakondoo namna ya kumtoroka hapo ndipo pa kuanzia.

Ipo jitihada kubwa sana ya kujaribu kumtenganisha Aboubakar Mbowe na Chadema.

Katika hilo kuna mijamaa itafanya yote ikiwamo kulia machozi ya mamba.

Uzi huu unawahusu sana:

Mahasimu wa CHADEMA, Mbowe na Chanjo tukutane hapa

Jamani eeh Chadema hawajahitaji ushauri wenu. Kwani ukiukwaji wa haki za msingi za watu mliupigia kelele wapi?
 
Hajashindwa ila ni jambo la mbolea kupisha wanachama wengine kulingana na mazingira.
For your information-Mbowe alishasema hatoendelea na uenyekiti baada ya 2024-Na lisu ni makamu mwenyekiti hvyo sioni changamoto. Chancellor Merkel wa ujerumani ametawala miaka mingi na siyo ishu sana kwa wananchi wa Germany kwa sababu sheria inaruhusu na ni matokeo ya demokrasia.As long as Mbowe anachaguliwa kidemokrasia na katiba ya chama chake inaruhusu-Sion tatizo hata akitawala miaka 100.
 
Chadema haina cha kujifunza kutoka Zambia. Zambia wana Tume huru ya uchaguzi ná polisi wao hawaingilii uchaguzi kufanya uhuni. Tukiwa na Tume huru ya uchaguzi na polisiccm wakikaa pembeni basi ccm hawana chao nchi hii.
 
Mbowe akimpisha Lissu uenyekiti polisi wataacha kushambulia kwa mabomu na risasi mikutano ya wapinzani ?

Mbowe akimpisha uenyekiti Lissu tume ya uchaguzi ndiyo itaacha kutangaza kura za kwenye mabegi na kutangaza kura za wananchi ?

Kwanini Mbowe ampishe Lissu kwani hakuna mwanachadema mwingine tofauti na Lissu kuwa mwenyekiti ?
 
CCM sio chama cha siasa, CCM ni chama dola, kinawategemea polisi na Tume ya uchaguzi kushinda, huko Zambia kwao hali ni tofauti, wana tume huru inayowawezesha wagombea kushindana kihalali, habari ya kumuondoa Mbowe na kumuweka Lissu haitakuwa na maana yoyote kama CCM itaendelea kulindwa na vyombo vya dola ili ibakie madarakani.
 
Chadema haina cha kujifunza kutoka Zambia. Zambia wana Tume huru ya uchaguzi ná polisi wao hawaingilii uchaguzi kufanya uhuni. Tukiwa na Tume huru ya uchaguzi na polisiccm wakikaa pembeni basi ccm hawana chao nchi hii.
Asante sana,mada sijaisoma ila nilikua nataka niandike kitu kama hiki
 
For your information-Mbowe alishasema hatoendelea na uenyekiti baada ya 2024-Na lisu ni makamu mwenyekiti hvyo sioni changamoto. Chancellor Merkel wa ujerumani ametawala miaka mingi na siyo ishu sana kwa wananchi wa Germany kwa sababu sheria inaruhusu na ni matokeo ya demokrasia.As long as Mbowe anachaguliwa kidemokrasia na katiba ya chama chake inaruhusu-Sion tatizo hata akitawala miaka 100.

Mbowe na apewe mi 10 mingine kuwakomesha wapuuzi hawa.
 
yaani mwenyekiti wa chama awe lisu ambaye anakula maisha ughaibuni?
hili litakuwa kosa jingine kwa upinzani. Bora hata huyu anaepambana akiwa nyumbani bila kujali anawekwa ndani ama la.
 
Back
Top Bottom