CCM imempa Mbowe nguvu isiyokuwa na mfano

CCM imempa Mbowe nguvu isiyokuwa na mfano

Mwingereza

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2014
Posts
1,115
Reaction score
2,771
Wajuzi wa mambo wanaeema kwamba, kumuweka Mh. Freeman Mbowe ndani kwa kesi ya ughaidi, imemuongezea Nguvu kubwa mno kisiasa.

Mbowe amepata nguvu kubwa mno na huruma kubwa mno kutoka kwa wananchi ambao wengi wao wanaamini kesi dhidi yake, ni kesi ya mchongo ambayo imeshabuma.

Atakapotoka Jela, mtaji wake kisisasa utakuwa ni mkubwa wa kutisha , na bila Shaka akiendeleza moto wa katiba mpya, bila Shaka watawala wataachia katiba moya

Hawatakuwa na jinsi. Mbowe nguvu alimony sasa hivi, ni nguvu aliyopewa na watawala waliotaka kumsulubu. Kifupi ni kwamba, watawala wakubaliane na ukweli.

Badala ya kumdhoofisha, wamempa nguvu za kutisha. Wakubaliane na ukweli wa kuishi na nguvu ya mbowe na Chadema
 
Wajuzi wa mambo wanaeema kwamba, kumuweka Mh. Freeman Mbowe ndani kwa kesi ya ughaidi, imemuongezea Nguvu kubwa mno kisiasa...
Mbowe kama asingelikuwa Mchaga, watu wangelikuwa wanafikiria kumpa nchi kwa namna wanavyompigia promo.

CHADEMA wangelikuwa makini, wangekaa waondoe rangi mbofu mbofu katika muundo wao ili akitoka waunganishe hadi Magogoni.

Lakini wakiendelea kushikilia kwamba wako sahihi, wataishia kutetewa, kupewa pole na kuombwa ushauri tu, kwa serikali makini itakayokuwepo.
 
Yaani majuzi niko Mbagala napamda daladala, ikaja swala la Mbowe, daladala nzima ikalipuka. Huyu mama hafai kabisa, hataki kukosolewa anambambikia mbowe kesi sababu anadai katik mpya. Amejiharibia na CCM yake..hayo ni maneno ya wananchi ndani ya daladala
 
Wajuzi wa mambo wanaeema kwamba, kumuweka Mh. Freeman Mbowe ndani kwa kesi ya ughaidi, imemuongezea Nguvu kubwa mno kisiasa...
Alisema pia Dr Chegeni, alisema Ulimwengu? alisema Zito kabwe na alisema Antony Diallo
 
Yaani majuzi niko Mbagala napamda daladala, ikaja swala la Mbowe, daladala nzima ikalipuka. Huyu mama hafai kabisa, hataki kukosolewa anambambikia mbowe kesi sababu anadai katik mpya. Amejiharibia na CCM yake..hayo ni maneno ya wananchi ndani ya daladala
Wacha ibaki hivyo.

Mawakili wa Jamhuri wakiambiwa hivyo wanashtuka tumekosea wapi mbona Kibatala anasema hivyo?
 
Mbowe kama asingelikuwa Mchaga, watu wangelikuwa wanafikiria kumpa nchi kwa namna wanavyompigia promo.
CHADEMA wangelikuwa makini, wangekaa waondoe rangi mbofu mbofu katika muundo wao ili akitoka waunganishe hadi Magogoni. Lakini wakiendelea kushikilia kwamba wako sahihi, wataishia kutetewa, kupewa pole na kuombwa ushauri tu, kwa serikali makini itakayokuwepo.
Mkuu mbona unaleta ukabila. Hii nchi yetu sote.
 
Mkuu mbona unaleta ukabila. Hii nchi yetu sote.
Ni kweli kiongozi wangu. Lakini kumbuka kwamba Tanzania ni nchi yetu wote. Hatutakubali mtu yeyote anayeendekeza mambo ya ukabila wala udini. Chama chochote chenye mrengo wa kuimarisha udini na ukablia na wengine kuwatupia tupia tu kama mapambo, hakifai kuongoza nchi yetu kwa sababu hatutaki kupanda magari ya ukabila huo.

CHaDEMa tumewaambia, waache ukabila, wagawanye nguvu na madaraka katika sehemu zote za nchi tuwape nchi. Bila hivyo, ninyi wenyewe mnaona vile walivyojazana kwenye ngazi za juu ya uongozi, na bahati mbaya tabia zao zinajulikana.

Kuwapa nchi watu wenye mitazamo hiyo, tutakuwa tunajikomboa au tunabadilisha ukoloni tu? Maana sasa tunajuta kwa nini tulipigania uhuru kutoka kwa Mwingereza. afadhli tungebaki na ukoloni wa Mzungu kuliko ukoloni wa cckm.
 
Yaani majuzi niko Mbagala napamda daladala, ikaja swala la Mbowe, daladala nzima ikalipuka. Huyu mama hafai kabisa, hataki kukosolewa anambambikia mbowe kesi sababu anadai katik mpya. Amejiharibia na CCM yake..hayo ni maneno ya wananchi ndani ya daladala
Mimi nilmchukia Sana Samia baada ya kumpa Mbowe kesi, sitaki ata kumsikia
 
Hilo lipo kila mahali. Nilikuwa naenda Mwanza, kupitia Bariadi, nikiwa Bariadi, tena siyo Bariadi mjini, eneo moja linaitwa Dutwa, watu ambao sikutarajia, nikawasikia watu wanakijiji wanaongelea suala la Mbowe.

Walikuwa wanaongelea mahindi yao yaliyokauka kwa ukame. Mmoja akasema, mwaka huu ni lazima Serikali iwasaidie baadhi ya wananchi chakula maana kuna watu, hasa waliopanda mapema, hawatavuna.

Mmoja akasema, yaani huyu mwanamke afikirie hilo? Anachojua ni kuwabambikia kesi anaoona wanamzidi akili. Kilichoendelea mjadala mzima ukawa ni kesi ya Mbowe.

Rais Samia, Serikali na CCM, katika kesi hii, kama kipo walichofanikiwa, basi ni farajabyao ya moyo kuwa wamefanikiwa kumtesa Mbowe. Lakini kwa kiasi kikubwa imempa dharau ya kila aina Samia toka kwa wananchi wengi wenye akili na uelewa, mataifa rafiki na taasisi mbalimbali za kimataifa. Kesi ua kubumba dhidi ya Mbowe, ndiyo iliyomfanya Mulamula agonge ukuta US wakati alipotaka Rais wa US akutane na Samia. Alishindwa, na mpaka leo hii hawezi kukutana naye. Ataishia kukutana na akina Museveni, na akina Kagame.
 
CCM ya awamu ya tano na sita haishauriki. Baache batalokota benyewe ku nyavu.
 
Mimi nilmchukia Sana Samia baada ya kumpa Mbowe kesi, sitaki ata kumsikia
Mimi mwanzoni nilimsifia sana Samia.

Lakini kwa huu uchafu, she deserves to be the worst President ever. Ni hypocrite. Unafanya baadhi ya mambo vizuri ili kuwahadaa watu, kumbe ndani ya moyo wako, umejaa matendo ya shetani.

Hata Yesu alipokuwa akifundisha aliwahi kunena, "ole wenu mafarisayo na waandishi wa sheria, ni wanafiki, mnajifanya watu wazuri kwa nje, ndani mmejaa uchafu (Matayo 23: 27-28). Hakuna mnafiki anayeweza kupokea neema ya Mungu bila toba.

Ikumbukeni habari ya Anania aliyefanya unafiki wa kuonesha anampenda Mungu, kumbe sivyo. Mungu alimwondolea uhai palepale. Na mkewe akaja kuutetea unafiki wa mumewe, naye akafa palepale.
 
Back
Top Bottom