Akina Mashinji tuliwapa nafasi ktk hatua za kutaka kufita ile notion ya ukabila unaona alichofanya??
Akina Zitto waliewa nafasi ili kuondoa kile mnachoamini kama udini lakini unaona alichofanya??
Watu shupavu na wenye ujasiri wanafanikiwa sana. Wakishafanikiwa wanaitwa wakabila na wabaguzi sio kweli.
Miaka ya Nyuma wachaga walikuwa wanalaumiwa sana kuwa wanapeana ajira kwa undugu.
Nilipotembea nikasoma na kukutana nao pande nyingi nilikuta hawa jamaa ni wapambanaji sana. Wanajituma. So ikitokea nafasi mathalani Ajira utakuta wana sifa na vigezo vya kutosha. Wakipaya hiyo fursa utaona waoa tu ndio wanajaa ni rahisi kudhani wanapendeleana.
Mama wa kichaga mjane anafuga ng'ombe watatu wa maziwa na mbuzi kadhaa lakini anasomesha watoto wake wawil St Mary's wakati mnyamwezi mwenzangu ana ng'ombe 200 na watoto 30 hakuna hata anayesoma form four.
Kijana wa kiume au wa kike mpatie Laki tano aende mjini baada ya miaka 5 atakukabidhi duka la milioni tano. Wakati kijana wa kike au kiume mhehe mwenzangu baada ya miezi miwili hana hata mia. Akiwa wa kike anarudi nyumbani na mimba au watoto wawili wasiojulikana baba zao.
Mifano inatosha.
Umesema sahihi, na mimi naomba ku declare interest kwamba siku zote nimekuwa nikipigania equal distribution of opportunities but based on qualifications rather than kujaza namba.
Katika msingi wa mifano yako, haina maana kwamba huko St Mary's wanaosoma kule ni Wachaga tu, au wapambanaji niwao peke yao, ili uhalalishe kwamba hakuna uwezekano wa kupata watu wenye sifa kutoka sehemu zingine.
Hakuna mpambanaji kama Mkinga nchi hii. Na kwa umoja wa kitaifa, mara nyingine inahitajika mikakati maalumu ya kupromote kule kuliko backwards ingawa si kuwapa vyeo kama lizimonko alivyobadilishwa na Lukuvi.
La mwisho ambalo umesema, ukweli kabisa "MLIWAPA", kina zito, mashinji n.k. Huko kuwapa ndiko tunakokutaaa. Hata wao walijiona "WAMEPEWA", na hivyo wakajiona bado ni wakuja ndani ya chama. Hiyo dhana ndiyo mnapashwa kuindoa. Hampashwi kujiona ninyi ndio first class na mnaowapa Wanakuwa 02nd class, third nakuendelea.
Huko "kuwapa", inasura, rangi na harufu ya ubaguzi... Na hii inawafanya wajisikie wakuja, strategic tools na hawana haki. Sasa mnachopashwa kukifanya siyo kuwapa.
Ninyi "mnaowapa" ni nani kwanza? Wanagundua kwamba mnawatumia kuwafunika na kusukuma agenda zenu kama objects. Kwa kutokujisika at home, ndiyo sababu waliondoka.
Sasa acheni hiyo "notion", ya kujiona ninyi ndio wenye chama, wengine "mnawapa".Ondoeni huo u "mimi", muone chama ni cha Watanzania wote na kila mwanachama anapoingia ajisikie "Nyumbani", na si mgeni. Achieni madaraka si kwa bendera, bali kwa uhalisia kwa watu wengine.
Mfano Mkti atoke Mtwara, Katibu atoke kaskazini, Na wengine watoke central, coastal n.k. n.k. na wawe na sauti na treatments sawa ndani ya chama. La sivyo, hizo itikadi za kusema "tuliwapa", ndizo haswa zinazofanya watu wa waone hamfai kuongoza taifa.
"Kuwapa watu vyeo halafu remote mnabaki nayo ninyi ambao "mnawapa", ndio huo ukabila, na kufanya chama kama mali ya kundi fulani wengine ni wakuja, ama nyenzo tu".