Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Kitendo cha Spika wa Bunge la JMT kuandika barua yenye utata ya kujiuzulu na kisha kujitokeza hadharani kutamka kumwomba radhi raisi Samia Hassan, kina maana kubwa.
Job Ndugai ametojitokeza ameomba radhi na kisha amejiuzulu na kuondoka.
Huyu Spika si yule marehemu Adam Sapi Mkwawa na wala si Mzee Pius Msekwa maana hawa ingekuwa ni wakti ule sidhani kama haya yangetokea.
Lakini tusisahau kwamba CCM mwaka 1992 ilijibadili kuwa "Chama Dola" hivyo kuamua kuwa na akiba za mijeleji, bakora, mikwaju, fimbo, ngonjera na mashairi pamoja na mipasho ya kusutana, kutukanana kutengeeana fitna na kisha kutimuana kama mbwa koko atimuliwavyo na kukimbia mkia umelala.
CCM imetuelimisha na kutupa nafasi ya kutafakari masuala mapana ya kitaifa khasa mimi na wenzangu hapa JF tupendao kuchambua.
Isipokuwa CCM imeshindwa kutuambia kwamba kumtimua na kumuondoa Job Ndugai katika nafasi yake ambayo alichaguliwa na wabunge wenzie wa Bunge la JMT ni kwa maslahi ya taifa, ya umma au ya nani? maana hadi sasa hakuna taarifa rasmi inayoeleweka uzuri ni kwanini CCM imeamua kufanya iloyafanya kuikanyaga katiba na kuingilia na kuuteka moja ya mihimili inayosimamia nchi hii.
Lakini pia CCM imetupa somo kwamba katiba ya JMT ni mali yao na si watanzania wengine, kwamba wanaweza kuitumia watakavyo.
Kisha CCM wameonyesha kwamba taasisi ya uraisi na taasisi ya bunge hizo ni kama nyumba za kupanga na wapangaji na raisi na Spika kama sio jaji mkuu na majaji na mahakimu kwa mahakama yaani wanapanga lakini mwenye nyumba yaani "CCM Dola" ana uwezo wa kuwaingilia kwa kutumia funguo za akiba alizo nazo na kuwatimua wapangaji hao.
Bunge la JMT ni moja ya mihimili mitatu ya serikali na kazi yake ni kutunga sheria ambazo zitatafsiriwa na mahakama (mhimili wa pili wa serikali) na kutekelezwa iwe kupitia vifungo, au hukumu za aina nyingine.
Nguvu ya Bunge imelalia kwa wananchi wa Tanzania ambao kwa bahati mbaya kwa sasa wamepatwa na kiharusi cha fikra, yaani wamezubaa. Spika wa Bunge ni mwakilishi wa jimbo la Kongwa na pia anawasimamia wawakilishi wenzie walochaguliwa na wananchi wa Tanzania nzima.
Lakini pia hii yatia shaka kwamba huenda kulikuwa na jambo la kutaka kumuondoa Raisi alie madarakani kupitia Bunge ambalo kama moja ya mihimili ya serikali ya nchi hii ina uwezo huo. Hiyo pia sisi wananchi tunapaswa kuelimishwa kwamba ni sababu zipi khasa zimefanya kilichotokea kitokee.
Raisi ana uwezo wa kulivunja bunge kwa masharti maalum ya kikatiba ila ibara ya 46A yasema kwamba Bunge pia likimhusisha Jaji Mkuu na tume ya Uchunguzi linaweza kumuondoa Raisi.
Na endapo kulikuwa na jambo kama hilo Raisi ana mamlaka kupitia ibara ya 90 ya katiba ambayo yanampa madaraka ya kulivunja Bunge.
Ila ni lazima tuelewe kuwa jambo lilotokea limeonyesha kuvuka kwa mipaka ya kuheshimiana kati ya mihimili miwili ya Taasisi ya uraisi na Bunge, na hili si jambo zuri kwa maslahi mapana ya taifa.
Vinginevyo bado huku mitaani itaendelea kueleweka kwamba misingi ya katiba kulinda mihimili mitatu ya serikali imekiukwa "big time" na kudhihirsha kwamba Raisi anapochaguliwa anaenda kupanga tu kwenye taasisi ya uraisi na Spika wa Bunge pia akichaguliwa na wananchi (wa jimbo lake) na wabunge wenzie awe spika basi hupewa funguo kupanga chumba cha bunge.
Kwa kifupi ni kwamba Taasisi ya Uraisi na Bunge pamoja na kuwa ni mihimili ya serikali lakini haimpi nguvu yoyote raisi wala spika pale anaposimamia jambo fulani kwa maslahi ya CCM na si taifa.