Sijui ndani ya CCM ameingia shetani gani!! Maana kwa mwenye akili, hata ile akili ya kawaida sana, hawezi kufanya yale ambayo CCM inayafanya kwa sasa.
Kiuhalisia, CCM ya sasa imewekeza sana kwenye uovu huku ikiwafukuza wananchi wote wema na wanaotaka haki ndani ya nchi.
Fikiria chama ambacho kinaongoza Serikali, Serikali yenye vyombo vya ulinzi vinavyotenda uharamia wa kiwango cha ajabu dhidi ya wananchi.
Chama ambacho kinawekeza katika kuteka na kuua wananchi, kuteka na kuwapoteza wananchi, kuwateka kisha kuwatesa na kuwatupa maporini wananchi.
Kwa fikra ya thinktank ya CCM, kuwaondoa wananchi wote wanaowakosoa au wasiowaunga mkono, ndiyo wanaamini ni kuwahakikishia ushindi. CCM haijui kuwa hata ndani ya CCM, si wote waliopo ndani ya CCM, mioyo yao inapenda na kufurahia uovu. Wapo watu ndani ya CCM kwa sababu waliaminishwa kuwa CCM ni chama cha haki. Hao wanapopata uhakika kuwa kumbe walikuwahawajui, CCM ni chama cha waovu, kamwe mioyo yao haiwezi kuendelea kuwa ndani ya CCM.
CCM haijui kuwa hao inaowateka, inaowaua na inaowatia ulemavu, wana ndugu, marafiki, majirani zao, waumini wenzao, wanavijiji au wanamitaa wenzao?
Kumwua, kumteka au kumjeruhi mtanzania mmoja kuunasababisha zaidi ya watu laki 1, waichukie CCM, waichukie Serikali, na wawachukie watawala.
CCM imevikwa upofu, ikiamini kuwa hata watanzania wote wasipoitaka, polisi na TISS wanatosha kuifanya ibakie kwenye madaraka! Hizi ni fikra za chama na watawala vipofu.
Kwa vitendo vya polisi wanaoamrishwa na CCM, kila tendo moja la kishetani linalofanywa na Polisi/TISS, linawaondoa malaki ya watanzania kutoka kuiunga mkono CCM na watawala, specifically, Rais Samia.
CCM inaamini kuwa waovu wanatosha kuipatia ushindi, wakati kiuhalisia, siku zote, binadamu wanaopenda uovu ni wachache kuliko wapendao haki.