KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Mwanafilosofia na mwanahistoria Niccolo Machiavelli kutoka nchini Italia aliwahi kusema " the end will justify the means" ambapo tukipeleka Kwa tafsiri isiyo rasmi alimaanisha " hata jambo baya likiwa na matokeo mazuri basi jambo hilo "morally" linakuwa ni zuri".
Kinachoangaliwa na kutazamiwa kama ubora wa jambo lolote ni matokeo ya jambo husika. Matokeo ndio yatatoa ukweli wa uzuri au ubaya wa jambo husika.
Kulingana na nukuu ya kauli ya Machiavelli, CCM itumie kauli katika utekelezaji wa mkakati wa uwekezaji katika bandari hususani kipindi hiki ambacho kuna mitazamo tofauti kuhusu uwekezaji huo.
Kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi kimeamua kwenda na uwekezaji wa bandari kulingana na tathmini kuonesha uwekezaji kwenye bandari una faida na Kwa kuwa faida hizo hata zikisemwa Sasa Kwa baadhi inakuwa ni ngumu kuziona mpaka waone matokeo basi ni vema CCM ikajikita kwenye kufanikisha matokeo ya uwekezaji huo.
Matokeo yanatakiwa kufanikishwa ni zile faida zote tunazoambiwa Sasa zitatokana na uwekezaji huo. Ni matokeo ndio yataonesha nia na dhamira njema iliyonayo CCM kwenye uwekezaji wa bandari.
Hili ni ombi Kwa CCM hakikisheni matokeo ya uwekezaji huo yanafikiwa ili wanaopinga leo wasipate sababu ya kuongea baadaye kama malengo yasipofikiwa.
Suala hili la uwekezaji wa bandari halitakwisha mpaka pale matokeo yatakapoonekana. Matokeo chanya ni "asset" Kwa CCM ila matokeo mabovu ni "liability" na kufanya watu waje kuamini Kila anayepinga uwekezaji yupo sahihi.