GE2025 CCM kufanya harambee ya Kitaifa Agosti 12,2025 kukusanya bilioni 100 za kampeni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hakuna lolote hapo zaidi ya kutakatisha pesa haramu iliyotumika kuuza mali za Watanganyika
 
Ko kweli ndo wako siriaz kiasi hicho kushindana upepo!?
 
Harambee kupambana na ACT na CHAUMA!
 
Bil. 100 kwa ajili ya Uchaguzi hewa.
Hivi mkiamua mkajenga vituo vya aya 200 kwa hizo hela si kampeni tosha?... Lakini mnajua watanganyika wanapenda kudanganywa,, ukiwekeza kwenye ukweli hawatokupa kura...
 
Mafisadi, wezi na wapokea rushwa, pamoja na wageni wasiruhusiwe kutoa michango.
 
Kwa
Kwa ajili ya kuikabili CCM B
 
Wanachangishana wafanye kampeni wakishindana na Salum Mwalim
Aibu yao Maccm
 
Wana vituko hawa, ushindani gani aliokusudia Mchimbi, hawa chauma na act??
 
Kumbe wakiamua kutokomeza umasikini wanaweza
Wakichangisha hizo kila miezi mitatu unadhani tutakosa maji masafi na salama?
Wazungu wanachangisha kila siku na kusaidia sana maisha ya kila siku

Ila sio kwenye uchaguzi
 
Wana DP World,TRA,Bandari,Mikoa na Wailaya lakini bado tu wanaenda kuomba shilingi mia tano ya mtanzania maskini ili wapate tiketi ya kwenda kumiliki mahekalu kama Ndungai na Ma V8.
 
​
Dkt. Nchimbi amesema maandalizi ya kampeni yanahitaji nguvu ya kifedha, ikiwemo ununuzi au ukodishaji wa magari, uchapishaji wa vipeperushi, mabango, tisheti, kanga, mafuta na gharama nyinginezo.
Ukiwa muongo usiwe msahaulifu. Kuna Ma-Bus tayari na T-shirt , khanga n.k. kwani zilipatikana kwa pesa zipi?
"Kwakuwa kila chama kinachoenda kwenye uchaguzi kinakuwa na maandalizi ya kampeni, na CCM inafanya hivyo na moja ya maandalizi muhimu kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kuwa na nguvu ya fedha”, amesema Dkt. Nchimbi.
Samia anapokwenda mikoani anatumia pesa za CCM?
Milioni 13 kila mmoja akichangia 1000 ni Bilioni 13. Nchimbi, huko vijijini na mikoani wapo wasioweza kuchangia hata 200. Tofauti ya B 80 mnaipata wapi!
Harambee hiyo inatarajiwa kushirikisha wanachama wa CCM kutoka maeneo mbalimbali nchini pamoja na wadau wa chama hicho, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na ushindani wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Wanachama ni akina nani na Wadau ni akina nani!
Kwanini usiseme Wafanyabiashara wakubwa(siyo wadau) wanaosubiri fadhila za Serikali kutoka rasilimali zetu

JokaKuu Tindo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…