Wakuuu, hiii kauli kuwa nitakukata na itategemea nimeamkaje, nimeifikiria Sana.
Kwa kauli hiii Tanzania kwenye democracy kumbe tumeishaweka kaburini kuanzia uongozi wa serikali had kwenye vyama, kiukweli ile kauli ni kauli mbaya Sana kwenye nchi Ya kidemocrasia yani Kwa sasa had Mbunge wa Ccm ili awe Mbunge mwenye maaamuzi sio chama, wala sio Kamati wala sio wananchi bali nimtu mmoja tu itategemea Siku hiyo atakuwa ameamkaje?
Hata hili wapo watakaokuja hapa watatetea, jamani Ccm Kwa sasa hakuna cha Kamati kumbe ila kuna mtu mmoja tu, daaah Ccm tumerudi Nyuma hatua Mia moja, hivi anavyotamka hadharani hivyo huko mafichoni si yatakuwa yanafanyika makubwa? Na iweje ubunge wa mtu uamliwe na mtu mmoja?
Wale Jamaaa wa upande wa pili walituonya kuwa akimaliza democracy upande wao atakuja kuiondoa kwetu, sasa hapa yupo wa kumtetea? Ccm ilikuwa mbali saaaana kiutendaji na kimfumo ila Kwa miaka minne hiii kwishnea, ili uwe Mbunge kuanzia sasa maaamuz yako na mtu mmoja tu.
Ebu tuangalie hiii ni hatari mwisho wa Siku hadi watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji muamuz atakuwa huyo huyo, na nikwa nini kila kiongozi atoke kwenye mikono Ya mtu mmoja?