CCM kukata Majina, alichokisema Mh. Rais, demokrasia na hatma ya Tanzania

Watanzania wote huwa tunaheshimiana [emoji1241]
ninachosema ni kile ninachoona bungeni. Hawawezi kuiwajibisha serikali na kuisimamia wanakuwa mhuri wa serikali na kuigharimu nchi kwa baadhi ya maamuzi yao
 
Mifano ya changamoto za demokrasia kwenye mazingira ya Afrika zilizotajwa kama mifano kwenye mada ya msingi, unakubali kwamba zipo? kama zipo, unadhani ni namna gani ya kuzikabili? au unadhani hamna haja ya kuzikabili, na ikiwa zitachwa tu ziwe zitakavyokuwa, unadhani ni faida gani zitakazopatikana na hasara gani zitapatikana?

Nadhani kuna vitu havihitaji majibu ya juu juu, vinginevyo labda kama tukiamua tu mambo yetu yaleee
 
ninachosema ni kile ninachoona bungeni. Hawawezi kuiwajibisha serikali na kuisimamia wanakuwa mhuri wa serikali na kuigharimu nchi kwa baadhi ya maamuzi yao

Wabunge wote akili zinafanana hawako serious na mijadala ata spika nae anazingua sana
 
Walisema watu kuwa kushangilia kifo cha demokrasia kwenye vyama vya UPINZANI ni kuhalalisha walio ndani ya chama tawala kuonewa na kukosa pa kujishika kwenye nchi huru ....
Katika siasa za ushindani Mwenyekiti wa chama hawezi kutamba hadharani kuwakata watu hata wakishinda ....anafanya hivyo kwakua anajua hawana ujanja wa kuhama ...
Zamani wakati angalau kuna demokrasia Mwenyekiti wa chama hangedhubutu kutamba namna hiyo na mara zote alizofanya hivyo gharama ilikuwa kubwa sana kwa CCM ..mfano Mkapa alijaribu kumpitisha mgombea wake Patrick Qorro Ambaye alishindwa na Slaa matokeo yakawa kukuwa kwa chadema Arusha ya kusini...baada ya mgombea aliyekubalika kuhamia huko
Kikwete pia mara zote alizojaribu ilimgharimu sana na hangeweza kuongea hilo hadharani sana sana wakati anaaga alionya kuminya haki ndani ya ccm kunawapa mitaji wapinzani ..
Mgombea kama Naibu waziri wa mambo ya nje ....ambaye Magufuli alimtaka japo alikuwa wa NNE ingelikuwa kuna uhuru mgombea aliyekatwa kwa uonevu angetafuta haki chama kingine au angemuunga mkono mgombea jimbo la songea lingepotea .....
Sasa wana CCM watalilia ndani kwa ndani ......
 
mkuu Phillemon Mikael unakubali kwamba matatizo yatokanayo na demokrasia kulingana na hali ya Afrika kama ilivyotolewa mifano kwenye uzi wa msingi yapo kweli? kama yapo kweli, wewe unadhani ni namna gani ya kuyadhibiti?
 
mkuu Phillemon Mikael unakubali kwamba matatizo yatokanayo na demokrasia kulingana na hali ya Afrika kama ilivyotolewa mifano kwenye uzi wa msingi yapo kweli? kama yapo kweli, wewe unadhani ni namna gani ya kuyadhibiti?
Kwahyo hutaki Demokrasia hivyo ibaki tu mtu achague wakwe zake na mashemeji kugombea kwa kadri atakavyo kama ambavyo kasema ITATEGEMEA KAAMKAJE au
 
Wakuuu, hiii kauli kuwa nitakukata na itategemea nimeamkaje, nimeifikiria Sana.

Kwa kauli hiii Tanzania kwenye democracy kumbe tumeishaweka kaburini kuanzia uongozi wa serikali had kwenye vyama, kiukweli ile kauli ni kauli mbaya Sana kwenye nchi Ya kidemocrasia yani Kwa sasa had Mbunge wa Ccm ili awe Mbunge mwenye maaamuzi sio chama, wala sio Kamati wala sio wananchi bali nimtu mmoja tu itategemea Siku hiyo atakuwa ameamkaje?

Hata hili wapo watakaokuja hapa watatetea, jamani Ccm Kwa sasa hakuna cha Kamati kumbe ila kuna mtu mmoja tu, daaah Ccm tumerudi Nyuma hatua Mia moja, hivi anavyotamka hadharani hivyo huko mafichoni si yatakuwa yanafanyika makubwa? Na iweje ubunge wa mtu uamliwe na mtu mmoja?

Wale Jamaaa wa upande wa pili walituonya kuwa akimaliza democracy upande wao atakuja kuiondoa kwetu, sasa hapa yupo wa kumtetea? Ccm ilikuwa mbali saaaana kiutendaji na kimfumo ila Kwa miaka minne hiii kwishnea, ili uwe Mbunge kuanzia sasa maaamuz yako na mtu mmoja tu.

Ebu tuangalie hiii ni hatari mwisho wa Siku hadi watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji muamuz atakuwa huyo huyo, na nikwa nini kila kiongozi atoke kwenye mikono Ya mtu mmoja?
 
Ni tabia ile ile ya kusifu kila kitu anachoamua mh. Rais au CCM. Umekosea mno.
 

Ufalme mneutengeneza wenyewe. Hakuna demokrasia wala hawapendi demokrasia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…