CCM kukata Majina, alichokisema Mh. Rais, demokrasia na hatma ya Tanzania

Ndio maana wanajitoa ufahamu wa kumuitq Yesu[emoji3][emoji3]
 
Haya kumbe ni ya chama,Ngoja nisitie neno.Nilifikir ya kiserikali.
 
Ndio siasa za tanzania. Bora nitafte rubesa kazaa nisage kuliko hizi siasa.
 

Maandishi yamewekwa ukutani kila mmoja kusoma na kuelewa. Kura za maoni siyo kitu; uamuzi wa mmwisho ni wa mwenyekiti wa chama na wala siyo vikao. Ingawa kuna ukweli kwenye kauli, hatujazoea kuambiwa hivi hadharani. Siku zote tumeaminishwa kuwa kwenye chama cha siasa maamuzi hufanyika kwa vikao na kwa kutumia nguvu ya hoja. Nadhani kwa mtaji huu mtu hatakuwa amekosea akisema: "kwaheri demokrasia, kwaheri uhuru". Ndiyo kusema, kila anayetaka kugombea kupitia ccmsharti kwanza apime uhusiano wake na mwenyekiti. Na katika miaka hii mitano imeshabainika kuwa mwenyekiti anataka nini kutoka kwa mtu anayejinasibisha naye kiuongozi. Wanaotamani mfumo wa vyama vingi ufe wajitafakari upya; mbadala wake siyo chama dola kama ilivyokuwa huko nyuma. Badala yake tutapata kitu kingine ambacho hakijapata kushuhudiwa katika nchi hii.
 
Ndio siasa za tanzania. Bora nitafte rubesa kazaa nisage kuliko hizi siasa.
Hapana huku tulipo tumerud Nyuma Sana bhana, tungeacha watu wachaguliwe na Kamati kisha waende Kwa wananchi waombe ridhaa huko, Kamati zibaki kuwa na maaamuzi Kama zamani na wananchi wapewe nafasi Ya kuamua huku tunakoenda ni kurud Nyuma mno
 

Hata Mollel, naibu waziri wa afya, alipitishwa kwa busara sampuli hii?
 
Hapana huku tulipo tumerud Nyuma Sana bhana, tungeacha watu wachaguliwe na Kamati kisha waende Kwa wananchi waombe ridhaa huko, Kamati zibaki kuwa na maaamuzi Kama zamani na wananchi wapewe nafasi Ya kuamua huku tunakoenda ni kurud Nyuma mno
Ohoo. Hakuna cha kamati wala tume. Hapa ni mtindo wa kuamka vibaya na kuwakata. Ole wako uwe bungeni uache kusifia
 
mkuu Phillemon Mikael unakubali kwamba matatizo yatokanayo na demokrasia kulingana na hali ya Afrika kama ilivyotolewa mifano kwenye uzi wa msingi yapo kweli? kama yapo kweli, wewe unadhani ni namna gani ya kuyadhibiti?
Ni kweli nakubaliana na wewe kuwa uelewa wa wapiga kura ni kiungo muhimu sana ili demokrasia ya kweli ikamilike. Tanzania ukiamua kuwapa watu demokrasia ya asilimia 100 unaweza kujikuta bunge limejaa watu walionunua ubunge kwa fedha, chakula na vinywaji. Lakini kwa upande mwingine unapokuwa na kiongozi kama Magufuli ni hasara kubwa kwa sababu anatumia ile turufu aliyonayo kuwa-manipulate wale wanaopitia kwenye chekecheo lake kwa manufaa yake binafsi au maono yake (ambayo wakati mwingine yanakuwa potofu kabisa). Mimi naamini kwenye utaratibu wa kuwa na system ambayo inatumika kuwachuja hao wagombea bila kuweka hisia au matakwa ya mtu mmoja mbele. Kwa mfano kwenye uchujaji au uteuzi Magufuli anapendea wale wafuasi wanaofuta kila wanaachoamriwa bila ku-challenge. Na hata teuzi zake nyingi zinaongozwa na hisia zake binafsi na siyo umahiri wa anaowateua.
 
UBAKAJI WA DEMOKRASIA
 
SIKU HIZI NI UBABE TU
 
Hakuna chama duniani chenye katiba Ya kuruhusu mtu mmoja kuwa na maaamuzi tu, hakipo Kama kipo hicho chama ni kiiini macho maaana Ya Kamati ni nini? Angejificha hata kwenye kichaka cha Kamati aseme kuwa itategemea Kamati imeamkaje
ALAFU ANASEMA TUMUOMBEE
 

Kwa maana yeye wala siyo mhimili basi yeye mwenyewe binafsi atakuwa na mizizi aliyojichimbia na kujisimika kweli kweli. Itakuwa kajichimbia kuliko hata chama chenyewe.
 
Tumerudi nyuma sana na huyu dikteta labda hata Wakoloni hawakuwa hivi. Acha baadhi ya Watanzania waseme tu bora wakoloni warudi. Msikilize Jenerali Ulimwengu hapa chini.


Hapana huku tulipo tumerud Nyuma Sana bhana, tungeacha watu wachaguliwe na Kamati kisha waende Kwa wananchi waombe ridhaa huko, Kamati zibaki kuwa na maaamuzi Kama zamani na wananchi wapewe nafasi Ya kuamua huku tunakoenda ni kurud Nyuma mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…