CCM kukata Majina, alichokisema Mh. Rais, demokrasia na hatma ya Tanzania

Membe asisitiza - Formular ya 5 - 3 - 1 (FIVE -THREE - ONE )

 
Amani iwe kwenu,
Tunaweza kuwaacha watu wachaguliwe na kamati huko, lakini ni kweli kamati ndizo zimewachagua au rushwa? Kuna mambo yanafikirisha sana.
 
Kwa bahati mbaya ni kwamba Afrika bado tupo watu wengi sana/wapiga kura ambao uelewa wetu juu ya mambo na uwezo wetu wa kuchanganua vitu na kufanya maamuzi sahihi ni mdogo. Kwa mfano, % kubwa ya watanzania hatuelewi falsafa, itikadi, misingi na sera ya vyama achilia mbali kuzifuata. Jiulize mfano ukisema chama cha mrengo wa kushoto, mrengo wa kati kushoto, mrengo wa kulia ujamaa wa kidemokrasia na vitu kama hivyo, ni watanzania wangapi wanaelewa unasema nini?

Naomba elimu kidogo kwenye falsafa hizo hapo juu.
 
Wagombea wa CCM msiokuwa kwenye upepo wa Mwenyekiti wenu haya kazi kwenu.!!
Ushauri: Tumia muda huu mchache uliobakia kumfurahisha Mwenyekiti kwa njia yoyote ile uijuayo...mwingine kasema Mwenyekiti ni kama Yesu!! na wewe buni yako muda si rafiki.
 
Vvyama vya Upinzania vikifa , demokrasia ya ccm itakufa ...na madhara ya demokrasia ccm kufa ....na wanaoojiona hawasikilizwi hawana pa kusemea ...ni kuzalisha uasi wa kimya kimya kwa kushirikiana na walio nje ya chama ....na kuzalisha MAPINDUZI

MTAGUNDUA toka mfumo wa vyama vingi umeanza TISS haijanusa dalili yoyote ya mapinduzi , wakati wa chama kimoja palikuwa na zaidi ya mipango kamili ya mapinduzi zaidi ya Saba , huku mipango midogo midogo iliyodakwa au isiyo na nguvu ilikuwa haina idadi , na tulivuka salama ...
Baada ya vyama vingi kuanza imekua rahisi sana mtu yeyote ndani ya chama au serikali ambaye haridhiki ana uwanja mpana wa kujitoa kwenda upinzani au hata kama hataki kujitoa ....anapenyeza jambo linalomkwaza kwa wapinzani wanaliongea halafu linarekebishwa .....
 
Hatuzungumzii perfection, tunazungumzia complimentarism. Hakuna perfection.

Kwa mfano tunapozungumiza check and balance kwa mihimili ya dola, sio kwamba kuna mmoja ni perfect zaidi, bali tunazungumzia checks, vinginevyo ni hatari
 
Umejitahidi kujenga hoja yako vema,ila inasisimua na kuibua maswali mengi.Kama hautojali na bila mihemko uyajibu ili hoja yako iwe na mashiko.
Ni ukweli kwamba wapiga kura wengi siyo waelewa wa mbinu za manipulation,wewe unafikiri nini kingefanyika zaidi ili waweze kufanya maamuzi bila kuwa manipulated? Bila shaka ni suala LA elimu ya uraia kuwafanya wawe na informed choice.
Kuhusu complimentary system, je ni mfumo gani wa kisheria uliopo kufanya hilo?Uadilifu wa hiyo Complimenters unasimamiwaje?Ni watia nia gani hao mnaodhani lazima complimentary board iwaondoe kwa sababu yoyote ni wabovu kiasi gani?Kama Kibajaji,Mlingwa,Lugola,Sanga,Msukuma,Ndugai nk waliweza ubunge nami atashindwa?Hatari iliyo wazi ni complimentary system kutumika kukandamiza wasiopendwa na...
Ukijibu haya maswala machache,ndipo nitaelewa logic ya ushauri wako na tutaweza kusupport mantiki yake.
 
Ukitaka kuamini kuwa kilichoa dikwa kwenye bandiko ni kweli angalia comment hapa. Utajua upo ushabiki wa kindezi sana haufuati mantiki, sera , hoja bali aliyesema ni nani yuko upande gani
Mkuu tuna tatizo kubwa sana linalowakabili wengi na bila mechanism hiyo, itayokea mambo ya ajabu zaidi kuliko ambayo yamekuwa yakionekana. Na comment za wadau tu ni ushahidi tosha kama unavyosema.
 
Hatuzungumzii perfection, tunazungumzia complimentarism. Hakuna perfection.

Kwa mfano tunapozungumiza check and balance kwa mihimili ya dola, sio kwamba kuna mmoja ni perfect zaidi, bali tunazungumzia checks, vinginevyo ni hatari
Mkuu kitu kimoja muhimu kwenye checks and balances ni uwiano wa uhuru na uwajibikaji yaani independence and accountability. Bunge lisipokua huru dhidi ya influence ya serikali kuu basi hakuna uwajibikaji. Sasa how do you guarantee independence kwenye kamati kuu ili isichague viongozi kwa biasness/mihemko ilihali mwenyekiti ana clash of interest na wagombea?

Nachotaka kufaham ndio hiko yaani why wananchi wakosee kuchagua ila sio kamati kuu?

Kwanini maamuzi yafanywe na kamati kuu na sio independent body?

Hapo liweke sawa
 
Usiwaamshe,waacheni wararuane kwanza maana tutakuwa tunashughulika na majeruhi watakaoshinda mpambano.Vita ya Panzi...
 
CCM tumeamua kila mbunge wa nchii hii ni yule tutakaye amua
 
Unaposema independent body unakusudia nini mkuu? Kwa nini unadhani KK sio independent na hiyo independent body inatakiwa iweje ili iitwe independent?

Hoja ni kwamba ni vigumu mtu kutoa rushwa kwa wananchi, na pia akatoa rushwa kwa kwa KK na na wachujaji wengine. Pia ni vigumu ku manipulate kote kote, na ni vigumu pande zote kuamua kwa ushabiki. Kwa hiyo hiyo inasaidia kubalance na ku double check
 
Hatari iliyo wazi ni complimentary system kutumika kukandamiza wasiopendwa na...
Umemaliza kila kitu mkuu, suluhisho la tatizo linaweza zaa tatizo kubwa zaidi unless mchakato ungehusisha kamati iliyo huru kabisa dhidi ya ushawishi wa viongozi wakuu wa chama ili kusiwepo upendeleo kwenye kupitisha majina.
 
Unaposema independent body unakusudia nini mkuu? Kwa nini unadhani KK sio independent na hiyo independent body inatakiwa iweje ili iitwe independent?
Mkuu umeshaonesha kuwa wananchi huwa wanapiga kura sababu ya ushabiki na manipulation sio VIGEZO!

Sasa KK itahakikisha vipi inapitisha watu kwa vigezo na sio mihemko ya wana kamati?

Independence maana yake mtu ambaye hana maslahi na watia nia kabisa mfano majina yakawa coded wakapewa independent consultancies kufanya background checks na viti kma hivyo, then wanapeleka majina kamati kuu yanapigiwa sign tu.

Ila kwa hali ya sasa obvious ukiwa sio kipenzi cha mwenyekiti au mwana KK huwezi pitishwa hta kma una vigezo kwahiyo tatizo ulilolikimbia kwa wananchi linajirudia KK.
 
Mkuu tuna tatizo kubwa sana linalowakabili wengi na bila mechanism hiyo, itayokea mambo ya ajabu zaidi kuliko ambayo yamekuwa yakionekana. Na comment za wadau tu ni ushahidi tosha kama unavyosema.
Nani kasababisha?Tatizo limebuniwa ,kufanyiwa upembuzi yakinifu na kutekelezwa na hao hao mainjinia ambao sasa wanakata kata kila walikutalo.Maajabu ndiyo hayo,halafu kuna wanaoshangilia na kufuata mkumbo bila kuhoji.
Tungewaelewa kama mngekuwa mnaililia CCM ile ya Wakulima na Wafanyakazi yaani Jembe na Nyundo baadhi yetu tungewaelewa.Lakini kwa kuwa hii ya sasa ni Mpya(HIMA???) bakini nayo mng'oane kucha,macho na meno humo.
 
Umemaliza kila kitu mkuu, suluhisho la tatizo linaweza zaa tatizo kubwa zaidi unless mchakato ungehusisha kamati iliyo huru kabisa dhidi ya ushawishi wa viongozi wakuu wa chama ili kusiwepo upendeleo kwenye kupitisha majina.
Mkuu, in practice, hakuna namna unaweza kuunda kamati yoyote ndani ya chama cha siasa na viongozi wa chama husika wasiwe na ushawishi kwenye kamati hiyo. Ni sawa na kusema wazazi wazae mtoto halafu wasiwe na ushawishi kwa hiyo mtoto.

Kuhusu suala la je? Kama hao wachujaji na ni corrupt?


Ndio tunarudi kwenye tatizo la jamii sasa, kwamba kama jamii ni corrupt, na viongozi wanatokana na jamii, kurekebisha hali ya mambo inabidi kutegulate jamii "cause" na sio 'effect' na hili tumelifafanua sana kwenye mijadala ya peke yake.
 
Je consultants wakinunuliwa au kupewa maagizo? Kumbuka kuna atakayewalipa consultants na huyo ndie atakayewaambia nini anataka. Kwa hiyo tunarudi pale pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…