Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma, Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri James ameeleza kumshangaa Mshauri mkuu wa chama cha ACT-Wazarendo Maalim Seif Sharif kutoka na maoni yake kuwa chama chake kinakubalika visiwani Zanzibar.
Bw. Kheri amesema chama cha Maalim Seif ni chama kisicho na wafuasi bali kinachotegemea majina ya watu kuwa maarufu.
Aidha ameongeza kuwa Visiwa hivyo vitabaki kuwa ngome imara ya Chama cha Mapinduzi.
Haya yamekuja baada ya Maalim Seif Sharif Hamad, kuzungumza dhidi ya kile anachosema ni maandalizi ya fujo yanayoratibiwa na viongozi wa ngazi za juu wa serikali na chama cha CCM.