Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Siuoni mwelekeo mbaya, naiona Tanzania inayojishusha kiungwana. Siuoni ubaya wa maamuzi ya kufuta kesi za kubambikia tena ni mamia.
Tumeoneana sana kwa vyeo ambavyo ni dhamana, kuna vilio vingi kwenye jamii tunazoishi. Mungu huwa na njia za kumkumbusha binadamu kuwa uwepo wake juu ya ardhi ni kwa neema tu, hana kibali cha kujivuna na kujidanganya kiasi cha kujipa ukuu.
Rais Samia ni mwanamke, siku zote anakiona kile ambacho mwanaume hakioni hata kama kipo pembeni ya kiti alichokalia. Ni vyema tukubaliane na huu mwelekeo mpya wa awamu ya sita. Ni vyema tukaondokana na mazoea mabaya ya weusi wa ngozi zetu ukaenda mpaka ndani ya nafsi na kuleta weusi wa roho.